Friday, May 29, 2015



Mabondia Francis Cheka kushoto na Kiatchai Singwancha wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa May 30 utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A sabasaba .
PICHA NA SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Francis Cheka kushoto na Kiatchai Singwancha wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi ya May 30 utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A sabasaba

Mabondia Selemani Zugo naq Twaha Kiduku wakitunishiana misuli

BONDIA JOSEPH SINKALA AKITUNISHIANA UBAVU NA IBRAHIMU MAOKOLA BAADA YA KUPIMA UZIDO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO W MEI 30 KATIKA UKUMBI WA P.T.A SABASABA.

BONDIA EPSON JOHN AKIPIMA UZITO


Sepp Blatter ametetea vyema kiti chake cha Urais wa FIFA kwa mara ya 5 baada ya kushinda Uchaguzi uliofanyika Leo huko Uswisi baada ya Mpinzani wake kutoka Jordan kusalimu amri katika Raundi ya pili ya Kura.
Ushindi huu wa Blatter umekuja baada ya kugubikwa na Kashfa ya Rushwa iliyotokana na hatua ya Marekani kufungua Mashitaka kwa Maafisa wa FIFA kwa tuhuma za rushwa Siku moja tu kabla Uchaguzi huo kufanyika.

Ingawa katika Raundi ya Kwanza ya Kura si Blatter wala Mpinzani wake Prince Ali bin Al Hussein alieshinda Theluthi mbili ya Kura ili kushinda Uchaguzi huo wa Uraisi baada ya Blatter kupata Kura 133 na Prince Ali kupata 73, kitu ambacho kingepeleka Kura kupigwa tena, Mjordan huyo aliamua kubwaga manyanga na kukubali kushindwa.Akipokea ushindi wake kwa vifijo Ukumbini, Blatter alitamba: "Twende FIFA, Twende FIFA!" Mapema hii Leo, akiongea kwenye Mkutano wa Kongresi ya FIFA, Blatter alisema kama Uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Miaka ya 2018 na 2022 ungeenda kwa Nchi nyingine na si Russia na Qatar basi kashfa hiyo ya Rushwa isingekuwepo.


Jumamosi Mei 30, Uwanjani Wembley, Jijini London kuanzia Saa 1 na Nusu Usiku, Arsenal na Aston Villa zitagombea FA CUP kwenye Fainali na tayari vijembe vishaanza kutembea.
Mchezaji wa Aston Villa, Ashley Westwood, ameonya kuwa Wachezaji wa Arsenal hivi sasa hawapati usingizi kwa kumwota Straika hatari wa Villa Christian Benteke.

Benteke ni Straika wa Ubelgiji mwenye Miaka 24 na ameshapiga Bao 12 katika Mechi zake 12 zilizopita baada ya kupona maumivu yake.
Westwood amesema: "Benteke sasa amerejea katika ubora wake. Arsenal hawatapenda kucheza nae."
Mwanzoni mwa Msimu, chini ya Meneja alietimuliwa Paul Lambert, Benteke alififia na kisha kuandamwa na Majeruhi lakini sasa chini ya Meneja mpya, Tim Sherwood, Straika huyo ameibuka upya.

Lakini Westwood ameonya pia kuwa Timu yao si Benteke peke yake kwani wanao Fabian Delph, Tom Cleverly, Mchezaji wa Mkopo kutoka Man United, na Chipukizi Jack Grealish mwenye Miaka 19 ambae aling'ara mno kwenye Nusu Fainali ya FA CUP Villa ilipoibwaga LIverpool 2-1.Christian Benteke










Dkt Fidelis Owenya akikabidhi jezi kwa vilabu nane vilivyo fuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya kombe la Mbunge lijulikanalo kama Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini.




Jezi maalumu kwa ajili ya timu zilizo fuzu hatua ya robo fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.



Wachezaji wa Arsenal akiwemo  Robert Pires wajifanya mazoezi yao tayari kwa Fainali ya kesho jumamosi dhidi ya Aston Villa kwenye FA Cup

Walcott anataraja kufanya vyema zaidi ya Olivier Giroud Wembley baada ya kupiga hat-trick dhidi ya West Bromwiki iliyopita.

Mesut Ozil akimiliki mpira

Meneja Arsene Wenger akimcheki kijana wake  Alexis Sanchez wakati wa mazoezi huko London Colney

Danny Welbeck kuikosa Fainali hiyo ya FA Cup kesho jumamosi

Alexis Sanchez,  Francis Coquelin na kushoto ni Mikel Arteta

Mathieu Debuchy karudi na hapa alikuwa akimkaba  Theo Walcott

Walcott na Pires wakiteta jambo kwenye uwanja wao wa mazoezi wa London Colney

Santi Cazorla akikabwa na  Laurent Koscielny pamoja na  Francis Coquelin
 Per Mertesacker akiangaliwa nae na Meneja


Sepp Blatter akiongeaTaswiraMichel Patini nae ndani kwenye Mkutano huo wa 65 wa FIFA 2015Sepp Blatter akiongeaMwenyekiti Roger Neininger FiFa Financial Director MarkusGreg Dyke mwenyekiti wa chama cha mpira EnglandSepp Blatter akiendelea kuongea 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja

waliotembelea blog