Rais
wa Chama cha Waendesha Baiskeli Tanzania, Godfrey Jacks Muhagama,
ambaye pia ni miongoni mwa waendesha baiskeli kwenye msafara huo
ulioanzia Mbeya akitoa maelezo ya namna shughuli hiyo ilivyofanikiwa.
Mwakilishi wa Norwegian Church Aid nchini Tanzania, Tale
Hungnes akiwapongeza waendesha baiskeli mara baada ya kufika Dar es
Salaam wakitokea kwenye mpaka wa Malawi na Tanzania, Kasumulo Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Rashid Rutengwe akisaini madai ya haki ili
kuweka imani yake kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye
mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika
desemba mwaka huu huko Paris, Ufaransa.
Wanafunzi
wa shule za msingi Wambi na Nyamalala, James Lyimo (kulia) na Vannesa
Mgata wakionyesha mti waliokabidhiwa kwaajili ya kupanda katika shule
zao
Ofisa
Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia akikabidhi mti
kwa viongozi wa dini Mufindi, Mkoani Iringa, kutoka kulia ni Imamu wa
Msikiti Mkuu wa Mafinga na Mch. Annuai Mwinuka wa KKKT, Jimbo la Mufindi
Usharika wa Mafinga, zoezi hilo lililofanyika kwenye shule za Msingi
Wambi na Nyamalala zote za Mafinga.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dr. Rashid Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya waendesha baiskeli na viongozi wa msafara huo
Ofisa
Miradi wa Norwegian Church Aid, Nizar Suleiman akitoa maelezo juu ya
msafara wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi, baada
ya kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwenye shule ya Sekondari
Kola Hill.
Waendesha baiskeli wakiwa katika eneo la Ruaha Mbuyuni
Mwakilishi wa Norwegian Church Aid nchini Tanzania, Tale Hungnes akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha baiskeli, walipofika kwenye mji wa Ilula, Mkoani Iringa.
Baadhi
ya akina mama wa mji wa Makambako wakisikiliza kwa makini maelezo
kutoka kwa vijana wahamasishaji wa elimu ya mabadiliko ya tabianchi wa
YouthCAN Tanzania
Msafara wa waendesha baiskeli ukiingia kwenye mji wa Ilula Mkoani Iringa
Esther
Joshua ambaye ni mwanamke pekee kwenye msafara wa kuendesha baiskeli
kutoka Mbeya mpaka Arusha, hapa akiwa nje kidogo ya mji wa Mafinga
kuelekea Iringa Mjini.
Waendesha baiskeli wakielekea jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro, Muhongo Rweyemamu akipanda mti kwenye shule ya
Sekondari Kola Hill, Mkoani Morogoro ambayo ni sehemu ya kampeni hiyo
Na Dotto Kahindi
Msafara
wa Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia
uendeshaji wa baiskeli ambao ulianza Octoba 17 mwaka huu kwenye mpaka wa
Tanzani na Malawi umefika jinini Dar es Salaam ambako utasimama kupisha
zoezi zima la uchaguzi mkuu kabla ya kuelekea Namanga Arusha.
Msafara
huo ambao umekuwa ukipata mapokezi makubwa kutoka kwa viongozi
mbalimbali wa serikali, dini na wananchi kwa ujumla, ukiwa Mkoani
Morogoro ulipata mapokezi makubwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rajab
Rutengwe.
Mkuu
huyo wa mkoa amewapongeza waendesha baiskeli na kuwaita ni mashujaa na
mabalozi wazuri wa kuhamasisha jamii kutunza mazingira na kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi.
Msafara
huo ambao umeanzia Msumbiji kupitia Afrika Kusini Botswana, Zimbabwe,
Zambia, Malawi na sasa Tanzania, utafikia kilele chake mjini Nairobi
Kenya mwezi novemba mwaka huu.
Dr.
Rutengwe amesema kuwa jambo la kutunza mazingira ili kupunguza athari
za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu na ni jambo la kila mmoja wetu.
Amewakemea
viongozi wa serikali wanaoshirikiana na wananchi kuharibu mazingira kwa
kukata miti na kuuza mikaa na kuahidi kuwashughulikia baada ya uchaguzi
mkuu kumalizika.
Akizungumzia
umuhimu wa milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru anasema ni muhimu kwa
kuwa ni moja ya vyanzo vya maji ambayo huwanufaisha watu wa mikoa ya
Morogoro, Dodoma, Pwani na Dar es Salaam.
“Sisi
watu wa Morogoro tukiwa wabinafsi kwa kuharibu vyanzo vya maji kwa
kufanya uharibifu kwenye milima ya Uluguru, Nguu na Ukaguru tutakuwa
tunawaua wenzetu wanaotegemea milima hiyo” anasema Dr. Rutengwe
Akitoa
taarifa ya msafara huo, Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Nizar
Suleiman anasema kuwa lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii
juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupitia uendeshaji wa baiskeli na
kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini kufikisha elimu
hiyo.
Anasema
msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka
imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa
kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika desemba mwaka
huu huko Paris, Ufaransa.
Msafara
huo unatarajiwa kuendelea tena novemba 3 mwaka huu, ukitokea jijini Dar
es Salaam kuelekea Namanga Mkoani Arusha ambapo utakabidhiwa kwa
waendesha baiskeli wa Kenya.