MENEJA
wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameondoa uwezekano wa kumsajili Luis
Suarez kutoka Liverpool katika majira ya kiangazi baadae mwaka huu.
Arsenal walijaribu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay wakati
wa usajili msimu uliopita huku Suarez mwenyewe akitaka kuondoka Anfield.
Lakini Wenger amekanusha tetesi mpya zilizozuka kuwa bado wanahitaji
huduma ya nyota huyo ambaye yuko katika kiwango cha juu msimu huu.
Wenger amesema uhamisho wa mara ya kwanza wa Suarez haukufanikiwa hivyo
mchezajihuyo hajawahi kuwa wa kwao na itabakia hivyo.
Suarez
mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 23 katika mechi 19 alizoichezea
Liverpool na kuwawezesha kuwepo katika nafasi nne za juu kwenye msimamo
wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Arsenal wanatarajiwa kukwaana na Liverpool
katika Uwanja wa Anfiled Jumamosi ambapo wanaweza kuongeza pengo la
alama kufikia 11 kama