Tuesday, July 29, 2014

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (kulia), akimakabidhi Bendera ya Taifa, mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Chess, Hemed Mlawa (wa pili kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuondoka kesho kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa nchini Norway. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, kushoto ni mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. Safari hiyo imedhaminiwa na Tanzania Chess Foundation na Kasparov Foundation.
Hapa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini (kulia), mchezaji Hemed Mlawa (kushoto) na Emmanuel Mwaisumbe (wa pili kushoto), wakifurahi baada ya kucheza mchezo huo wakati wakiwaonesha waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari.
Wachezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa (kulia) na Emmanuel Mwaisumbe wakiwa kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa bendera ya Taifa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania, Henry Lihaya.
Kulia ni Mratibu wa Chess Tanzania, Johnson Mshana akifuatilia kwa karibu tukio hilo. Kushoto ni Mwanahabari
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na mchezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa wakionesha umahiri wa kucheza mchezo huo mbele ya wanahabari.Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi na mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com- simu namba 0712-727062, 0786-858550)
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
 
TIMU ya Taifa ya Chess imeagwa Dar es Salaam leo asubuhi kwajili ya kwenda kushiriki mashindano ya chess 41 ya kimataifa Olympiads yatakayofanyika nchini Norway.
 
Jumla ya wachezaji watano wataondoka nchini leo usiku kwenda kushiriki mashindano hayo.
 
Wachezaji hao ni Geofrey Mwanyika, Hemed Mlawa, Emmanuel Mwaisumbe, Nurdin Hassuji na Yusuph Mdoe.
 
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi timu hiyo bendera ya taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi alisema kuwa kuwakabidhi bendera hiyo ni ishara ya kuwatakia safari njema na ushindi katika mashindano hayo.
 
Malinzi alisema anashukuru wale wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kusimamia mchezo huo nchini hadi kufikia kushiriki mashindano ya kimataifa.
 
”Namshukuru sana Mr Vinay kwa msaada wake anaoutoa kusapoti mchezo huu Tanzania na kwa moyo wake wa kutoa, maana waswahili husema kutoa ni moyo na sio utajiri maana kuna matajiri wegi lakini sio watoaji” alisema
 
Aliongeza kuwa anamatumaini kuwa wachezaji hao watakwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuitangza Tanzania.
 
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet na Mwanzilishi wa Mchezo wa Chess Tanzania, Vinay Choudary alisema kwa yeyote atakayeweza kuibuka na ubingwa shilingi milioni mia moja zitatolewa kwa ajili yake.
 
Choudary alisema hadi sasa walipofikia ni pazuri kwa Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa hivyo anawatakia safari njema na ushindi katika mchezo huo.
 
Mchezaji Hemed Mlawa alisema wataiwakilisha vema Tanzania na watahakikisha wanafanya vizuri.
 
”Hii ni mara ya kwanza sisi kushiriki hivyo hatuwezi kusema kuwa tutarudi na ushindi moja kwa moja bali tutafanya vizuri na tunaamini tunaweza kuzishinda baadhi ya nchi”alisema
 
Mashindano hayo ni ya wiki mbili na yameratibiwa na Shirikisho la Chess Duniani(FIDE)
na kudhaminiwa na Tanzania Chess Association na Kasparov Association.


D92A2961
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
D92A2982
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
D92A3004
D92A2839
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)



CRISTIANO Ronaldo ameshinda tuzo ya Goal 50 ya mchezaji bora wa dunia baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2013-14.
Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu kama sehemu ya kuheshimu kazi aliyoifanyia Real Madrid kutwaa taji la 10 la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo mwenye miaka 29, pia alishinda kombe la mfalme (Copa del Rey) na kufunga magoli 51 katika mashindano yote ya klabu na taifa lake.

WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50 mpaka sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu sambamba na Luis Suarez na mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia na kushinda tuzo ya 2013 FIFA Ballon d`Or.
Baada ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Kiukweli nimefurahi sana”.
“Nashawishika kusema nisingeweza kutwaa tuzo hii bila sapoti kutoka watu wa Real Madrid”.
Goal 50 ni moja ya tuzo za heshima kwenye mchezo wa soka kwasababu wanaochagua wanatoka katika mitandao mikubwa ya soka duniani.
Kura zinapigwa baada ya kumalizika kwa misimu ya ligi za ndani na mashindano ya kimataifa na wanaopiga kura wanatoka mataifa mbalimbali.
Zaidi ya waandishi wa habari 600 kutoka katika machapisho 35 wanachagua wachezaji 50 wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo ameongoza mwaka huu akifuatiwa na Arjen Robben, aliyeifanyia makubwa Uholanzi katika fainali za kombe la dunia na kuisaidia klabu yake ya Bayern kutwaa makombe manne msimu wa 2013-14.
Mshindi wa mwaka jana, Lionel Messi alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya katika klabu yake ya Barcelona na kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.



Manchester City imetangaza vifaa vyao vipya vya msimu ujao ambavyo vijana wa Manuel Pellegrini watakuwa wakitupia wakati wakijaribu kutetea taji lao la Premier League.
Mbingwa hao wameutangaza uzi wa rangi ya buluu iliyo iva kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike zikiwa zimesalia siku 16 kabla ya uzinduzi wa msimu mpya ambao utatanguliwa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Arsenal.


Pablo Zabaleta akiwa katika pozi la jezi mpya ya msimu ikiwa na vionjo vya rangi ya njano

Jezi mpya itaanza kuuzwa July 29 ambapo unaweza kuagiza kuanzia sasa.


KLABU za Jiji la Machester, Mabingwa wa England Manchester City na Manchester United waliovuliwa Ubingwa na City, wanaongoza Makundi ya Mashindano ya International Champions Cup. Upo uwezekano kwao kukutana kwenye Fainali ya Mashindano haya hapo Agosti 4 ikiwa wataendeleza wimbi lao la ushindina hivyo kuhamisha uhondo wa Dabi ya Manchester huko Sun Life Stadium, Miami, Florida.Man United, ambao wako Kundi A, walianza kwa kuichapa AS Roma Bao 3-2 na Man City, walio Kundi B, kuishindilia AC Milan Bao 5-1, na matokeo hayo yamewafanya waongoze Makundi yao.
Kila Kundi lina Timu 4 na hivyo kila Timu kucheza Mechi 3 na Mechi zinazofuatia kwao ni Man United kucheza na Inter Milan kwenye Uwanja wa FedEx Field ndani ya Washington DC Jumatano Asubuhi na City kucheza na Liverpool Siku inayofuata huko Yankee Stadium, New York.
Kanuni za Mashindano haya ni tofauti kidogo kwani wakati Mshindi wa kila Mechi hupewa Pointi 3, ikitokea Timu kuwa Sare mpaka mwisho wa Dakika 90, Mikwaju ya Penati 5 hupigwa ili kupata Mshindi ambae hupewa Pointi 2 na aliefungwa Pointi 1.


Kocha wa United Louis van Gaal  akiwacheki vijana wake kwenye mazoezi.

 Shaw (katikati) na wenzake wakijifua tayari kwa mchezo wao na Inter Milan hapo kesho  Agosti 30

Juan Mata na Darren Fletcher wakisubiri maelekezo kutoka kwa mwalimu wao jana wakati wa Mazoezi

 Louis van Gaal na Chris Smalling kwenye Mkutano na Vyombo vya habari huko  Maryland

Jonny Evans, Danny Welbeck na Wilfried Zaha a wote wakijifua

 Evans, Will Keane na Michael Keane (kulia) wakijiweka sawa tayari kwa mtanange wao wa kesho na Inter Milan.

Wachezaji wa  Manchester United wakisikiliza nen kutoka kwa Kiongozi

Kipa David de Gea

 Juan Mata na Tom Cleverley

Wayne Rooney

Rooney na Evans wakisikilizia wakati wa mazoezi yao kujiweka sawa tayari kukwaana na Inter Milan Washington D.C. – FEDEXFIELD

RATIBA
Ijumaa Julai 25

Olympiacos CFP 3 AC Milan 0

Jumamosi Julai 26
Manchester United 3 vs AS Roma 2
Jumapili Julai 27
Real Madrid CF 1 vs Inter Milan 1 [Penati 2-3]
AC Milan 1 Manchester City 5
Jumatatu Julai 28
Liverpool 1vs  Olympiacos CFP 0

Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan [Washington D.C. – FEDEXFIELD]
05:15 Real Madrid CF v AS Roma [Dallas, Texas - COTTON BOWL]


Mourinho: It feels like Drogba never left Chelsea

JOSE Mourinho amefurahishwa na urejeo wa Didier Drogba na anatarajia mshambuliaji huyo ataisaidia Chelsea msimu uliopita. 
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alisaini mkataba wa mwaka mmoja ijumaa ya wiki iliopita kufuatia mkataba wake kumalizika na klabu ya Galatasaray ya Uturiki. 
Drogba alifurahia miaka nane akiwa darajani, kuanzia mwaka 2004 hadi 2012. 
Nyota huyo mwenye miaka 36 alijiunga na kikosi  cha Chelsea siku ya jumapi ambapo walishinda mabao 2-1 dhidi ya Olimpiji katika mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu, lakini hakucheza.

“Awali ya yote, alipokuja, ilionekana kama hajawahi kuondoka klabuni,”  Mourinho aliwaambia waandishi wa habari. “Ilikuwa kawaida sana, hakukuwa na jipya kwasababu anamjua kila mtu na kila mtu anamjua”.

“Siku zote alikuwepo hapa hata kama hakuwepo hapa. Chelsea ni klabu yake,  hata miaka miwili ambayo alikuwa mbali na kuzichezea klabu za Galatasaray na Shanghai (Shenhua)”.


“Kwahiyo inaonekana kama alikwenda kwenye mapumziko mafupi na kurudi tena, kila kitu ni kawaida. Lakini kweli, nadhani tunamhitaji sana. Tunamtaka kaka mchezaji wa kikosi chetu ili kiwe kama ninavyotaka”.



KATIKA historia yake, klabu ya Simba haijawahi kuwa na uwanja wake wa mazoezi, hivyo kujikuta anahangaika miaka nenda rudi.

Lakini kwasasa unaweza kusema imedhamiria kujenga uwanja wa mazoezi maeneo ya Bunju jijini Dar es salaam.

Ismail Aden Rage alipokaribia kumaliza muda wake alianza mchakato wa kujenga uwanja wa Bunju akisema wanataka kupata sehemu ya kufanyia mazoezi.

Pia alisema wanakusudia kujenga hosteli za kuishi wachezaji ikiwa ni mkakati wa kupunguza gharama ya kuweka wachezaji hotelini.

Uongozi mpya chini ya Rais Evans Elieza Aveva alisema uko tayari kuendeleza ujenzi huo ulioanzishwa na Rage.

Mpaka sasa nyasi zilishapandwa na muonekano wa uwanja uko kama unavyoonekana pichani juu.

Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama leo alifuturisha wasanii, ndugu,jamaa na marafiki zake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka marehemu mama yake mzazi ambaye alishatangulia mbele ya haki. Akitoa shukrani zake kwa waalikwa, alisema ameona vyema kuandaa chakula cha pamoja ili waweze kumuenzi mama yao mzazi kwa vile alipenda sana watu hasa kukutana na kupata chakula pamoja.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiendelea kutoa shukrani zake za pekee.

Mjomba wa Msanii chipukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akitoa shukrani zake za pekee.

Msanii wa runinga, Michael Deodatus Sango ‘Mike’ akitoa shukrani kwa niaba ya rais wa Bongo Movie Steve Nyerere ambaye hakuweza kufika.
Wasanii, ndugu jamaa na marafiki waliofika wakipata futari.
Kila mmoja hakuwa nyuma kupata futari.
Huduma zikiendelea kutolewa.
Kumbu Kumbu.
Picha ya pamoja na wasanii wenzake mara baada ya kupata futari.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama (kati) akiwa na Dada yake kushoto na mdogo wake wakipata ukodak.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiwa na wajomba zake.

waliotembelea blog