Friday, April 24, 2015


NI Barcelona vs Bayern Munich na Juventus vs Real MadridIlivyokuwa huko Nyon Uswisi leo wakati wa droo ya UEFA general secretary Gianni Infantino.Itakuwa patashika nguo kuchanika hapa!!BARCELONA vs BAYERN MUNICH
JUVENTUS vs REAL MADRID
EUROPA LEAGUE..LIVE DRAW
SEVILLA vs FIORENTINA
NAPOLI vs DNIPRO

Albert Soler, Amador Bernabeu, Ludovic Giuly y Jordi Mestre forman la comitiva del Barça


ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
THE ROYAL REGENCY
501 HIGH STREET NORTH
MANOR PARK

For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!
IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"
Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P


VINARA wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Ijumaa wanaingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakijua ushindi Mechi hii na mwingine hapo Jumatatu dhidi ya Polisi Moro utawapa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.

Hivi sasa Yanga wako kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 22 na Simba wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 23.
Hivyo Yanga, ambao tayari wameshakuwa moja ya Timu mbili zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao, wanahitaji Pointi 6 tu kuwa bila Bingwa bila kujali nini mpinzani wake Azam FC anakifanya.

Hata hivyo, Yanga wana wakati mgumu hivi sasa baada ya kukabiliwa na Majeruhi kwenye Difensi yao kwa kuwakosa Kepteni Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kevin Yondani pengo ambalo Juzi lilishuhudia Stand United kuwaendesha mchakamchaka na kushinda kwa mbinde 3-2.
Azam FC Jumamosi wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kukwepa Simba, ambao Jumatano waliitwanga Mgambo JKT 4-0, kuwapiku Nafasi ya Pili.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA:

Leo Ijumaa Aprili 24
Ruvu Shooting v Yanga
Jumamosi Aprili 25
Mbeya City vs Kagera City
Simba vs Ndanda FC
Azam FC vs Stand United


UROPA LIGI, Mashindano makubwa ya pili kwa Klabu Barani Ulaya, Usiku huu Alhamisi yamemaliza Mechi zake za Robo Fainali na Mabingwa Watetezi Sevilla ya Spain, Dnipro Dnipropetrovsk ya Ukraine na Timu mbili za Italy, Fiorentina na Napoli, zimefuzu kuingia Nusu Fainali.
FIORENTINA 2 vs 0 DYNAMO KIEV
Fiorentina wamefuzu kuingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI baada ya kuitandika Dynamo Kiev Bao 2-0 na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-1 katika Mechi mbili.

Mchezaji wa Fiorentina Mario Gomez akiziona nyavu za wapinzani wao usiku huu. Gomez akishangilia pamoja na mwenzake Marcos Alonso baada ya Fiorentina kusonga hatua ya Nusu Fainali
Jeremain Lens wa Dynamo alipewa Kadi Nyekundu Dakika ya 40 baada ya kulambwa Kadi ya Njano ya Pili kwa kujiangusha kwa makusudi kwenye Boksi la Fiorentina.
Dakika 3 baadae Mario Gomes akaipa Fiorentina Bao na wakapiga Bao la Pili Dakika ya 90 kupitia Juan Manuel Vargas.

NAPOLI 2 vs 2 WOLFSBURG
Napoli wameingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI baada ya kutoka Sare 2-2 na Wolfsburg na kufuzu kwa Jumla ya Mabao 6-3 kufuatia ushindi wao wa 4-1 wa Ugenini huko Germany Wiki iliyopita.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0 lakini Napoli waliingia Kipindi cha Pili wakiwa moto na kufunga Bao 2 katika Dakika za 50 na 65 kupitia Jose Callejon na Dries Mertens.

Dakika ya 71 Wolfsburg walipata Bao Mfungaji akiwa Timm Klose na Dakika 2 baadae Ivan Perisic aliifanya Gemu kuwa 2-2.
DNIPRO 1 vs 0 CLUB BRUGGE
Kufuatia Sare ya 0-0 Ugenini, Dnipro wakicheza kwao walishinda 1-0 na kuingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI.
Dnipro walipata Bao lao la ushindi Dakika ya 83 Mfungaji akiwa Yevgeniy Shakhov.


ZENIT 2 vs 2 SEVILLA

Mabingwa Watetezi wa EUROPA LIGI, Sevilla, wakicheza Ugenini huko Urusi, walitoka Sare 2-2 na Zenit lakini wamefuzu kwa Jumla ya 4-3.

Sevilla walifunga Bao la kwanza kwa Penati ya Carlos Bacca Dakika ya 5 kufuatia Rafu ya Neto na Zenit kurudisha Dakika ya 48 baada Kipa Beto kuutema Mpira na Jose Salomon Rondon kufunga na kisha kwenda 2-1 mbele kwa Bao la Hulk la Shuti la mbali katika Dakika ya 72.
Sevilla walipata Bao muhimu Dakika ya 85 kupitia Kevin Gameiro na Gemu kuwa 2-2.

waliotembelea blog