Sunday, March 9, 2014

Young Africans imetolewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na mabingwa watetezi Al Ahly kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia kumalizika kwa dakika 90 za mchezo Al Ahly ikiwa na bao 1- 0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 mchezo uliofanyika usiku wa leo katika Uwanja wa El Max jijini Alexadria.
Young Africans iliingia uwanjani ikiwa makini na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa lango la Al Ahly lakini Didier Kavumbagu alishindwa kutumia nafasi hiyo na mpira kuokolewa na walinzi kabla ya kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Al Ahly walifanya mashambulizi langoni wa Young Africans lakini walinzi wake Kelvin Yondani, Nadir Haroub walikua makini kuokoa michomo hiyo huku mlinda mlango Dida akifanya kazi za ziada kuokoa hatari lanongi mwake.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Al Ahly 0 - 0 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi na kusaka mabao ya mapema lakini bado ngome zote zilikuwa makini na kufanya milango kuwa migumu huku mwamuzi wa mchezo leo kutoka nchini Sengal akiwaonyesha kadi wachezaji wa Yanga na kupuliza filimbi kila wachezaji wa Al Ahly walipogiswa.
Dakika ya 70 ya mchezo mlinzi wa kushoto wa Al Ahly Saed Mowaeb aliipatia timu yake bao kufuatia mpira alioupiga kumzidi uwezo mlinda mlango Deo Munish na kujaa wavuni na kuhesabu bao.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Al Ahly 1 - 0 Young Africans hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 kufuatia Yanga kushinda bao 1-0 pia jijini Dar es salaam.
Mara baada ya kumalizka kwa dakika 90 mwamuzi aliamuru zipigwe penati ambapo wapigaji wa Young Africans waliopiga ni
Nadir Haroub - alifunga
Didier Kavumbagu - alifunga
Emmanuel Okwi - alifunga
Oscar Joshua - alikosa iligonga mwamba
Said Bahanuzi - alikosa ilitoka nje
Mbuyu Twite - alikosa iliokolewa na golikipa Ekramy
Al Ahly penati zao zilifungwa na
Abdalllah Said, Gedo, Trezeguet na Mohamed Nagieb huku mlinda mlango Deo Munshi akizipangua penati mbili za Saed Mowaeb na Hossan Ashour
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Domayo, 7.Msuva, 8.Ngasa/Chuji, 9.DKavumbagu, 10.Okwi, 11.Kizza/Bahanuzi



Sehemu-ya-Bunge-la-Tanzania-Dodoma1_d83f3.jpg
Ndugu zangu,
Pamoja na kuwa mie si expert wa political science, lakini, kile kidogo ninachokijua naweza kuchangia nanyi. Katika kusoma kwangu Political Science nimesoma pia kwa uchache masuala ya uundwaji ama marekebisho ya Katiba.
- Kwamba marekebisho ya Katiba yanaweza kuwa na sura nyingi. Kuu tatu ni , 1. Yenye kupitishwa na Special Majority 2. Kura za Maoni kwa maana ya referendum, na 3. Bunge la Kawaida.

Hata hivyo, iliyo ya kawaida sana na ambayo yenye kuendana na kuutafuta muafaka ( Consensus) wa kisiasa ni pale panapohitajika mabadiliko husika ya Katiba kuthibitishwa na ' Special Majority''. Hii bila shaka ndio namna ama njia ambayo akina Jaji Warioba na wenzake wanataka kutupitisha.
Njia hii inatoa fursa kwa walio wachache katika kiwango kilichopangwa kuwa na ' Kura ya Turufu' kwa maana ya ' Veto'. Minority veto hapa ni hitaji la uwepo wa ' extraordinary majority' ambapo kwa kawaida huwa ni mbili ya tatu , yaani 2/3.
Katika hili bado, kwa kuangalia Bunge letu maalum la Katiba, kuna wajumbe ambao hawajapata uelewa, kuwa uwingi wa wafuasi wa chama fulani hauna maana ya kuwa wanaweza kupitisha wanayoyataka kwa vile wengine ndani ya Bunge ni wachache.
Hii 2/3 requirement haina maana nyingine bali ni ' Veto Power' ya minority- wachache. Walio wengi bado watahitaji kujenga hoja za kuwashawishi wachache ili wafanikishe 2/3 kwenye maamuzi. Maana, hapa 2/3 inatakiwa itoke kwa wachache. Na wachache nao ni lazima wajenge hoja za ushawishi wapate 2/3 ya walio wengi katika wanachokihitaji.
Hivyo, kwenye 2/3 requirement hakuna kuburuzana bali kushawishiana na kukumbatiana kwa hoja. Vinginevyo, kama utaratibu huo utakiukwa. Na kwa vile ni utaratibu uliopewa ' immunity' ya kisheria . Kuukiuka ni kwamisha mchakato mzima wa mabadiliko ya Katiba, kisheria.
Na kuna mifano ya nchi zinazotumia utaratibu huu kwenye maamuzi yake. Nchi kama Switzerland kwa mfano, Mabadiliko ya Katiba hayawezi kupita bila kuthibitishwa kwa kura za ' Special Majority' ya majimbo madogo kabisa ( cantons) yenye kufanya chini ya asilimia 20 ya watu wote wa Switzerland, hivyo basi, wanatengeneza kinachoitwa pia, a potential vote- kura muhimu au mahsusi.
Na Marekani wamekwenda mbali zaidi, wao wana kinachoitwa ' Three-Fourths'- 3/4. Hitaji la 3/4 ili marekebisho ya Katiba yafanyike katika Marekani lina maana ya majimbo yao 13, ambayo ni madogo sana, na yenye idadi ya watu chini ya asilimia 5 ya Wamarekani wote yanaweza kuzuia mabadiliko ya Katiba katika Marekani.
Hawa nao wana ' minority veto' kwa maana ya ' kura ya turufu' ya wachache. Kwamba ili jambo lipite, kauli zao lazima nazo zisikilizwe!
Ni mchango wangu mdogo kwa leo. Wenye kujua zaidi wanikosoe na watungezee maarifa...


UEFA CHAMPIONS LIGI, inarejea kilingeni kuanzia Jumanne Usiku kwa Mechi mbili na huko Jijini Munich, Uwanjani Allianz Arena ni Mabingwa Watetezi Bayern Munich wakiwakaribisha Arsenal na huko Spain, ndani ya Estadio Vicente Calderon, ni Atletico Madrid na AC Milan.
Kwenye Mechi hizo, Timu zote za Nyumbani, Bayern na Atletico, zipo kwenye hali njema baada ya kushinda Mechi zao za Ugenini za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kuacha kazi kubwa, hasa kwa Arsenal, kukomboa vipigo vyao.
Katika Mechi ya Kwanza huko Emirates, Arsenal ilichapwa 2-0 na Bayern Munich na huko San Siro, AC Milan ilitunguliwa 1-0 na Atletico.

UCL itaendelea Jumatano kwa Mechi nyingine mbili kati ya Barcelona na Manchester City huko Nou Camp na Paris Saint-Germain kuivaa Bayer 04 Leverkusen huko Jiijini Paris, France.

Kama ilivyo kwa Mechi za Jumanne, na Jumatano pia Timu za Nyumbani, Barca na PSG, zitaingia kwa hali njema wakiwa wameshinda Mechi zao za kwanza Ugenini kwa Barca kuipiga City 2-0 huko Etihad na PSG kuivurumisha 4-0 Bayer 04 Leverkusen huko Germany.

Mechi nyingi 4 zilizobakia za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitachezwa Wiki ijayo, Jumanne Machi 18 na Jumatano Machi 19.


UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO

Jumanne Machi 11

22:45 Bayern Munich v Arsenal FC (2-0)
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan (1-0)
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City (2-0)
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen (4-0)

Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]

Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]



Mchezaji wa Valladolid Fausto Rossi akishangilia bao lake baada ya kuinyuka Barcelona leo hii.BAO la Dakika ya 17 la Fausto Rossi limewapa ushindi Real Valladolid, waliokuwa Nyumbani, wa Bao 1-0 dhidi ya FC Barcelona na kuwanyima Mabingwa hao wa Spain Nafasi ya kushika uongozi wa La Liga.
Kipigo hiki kimewabakiza Barca Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Real Madrid ambao wanacheza Jumapili na Levante.
Ushindi huu umewapandisha Real Valladolid Nafasi 1 na sasa wako Nafasi ya 17.
Baadae Leo Atletico Madrid wapo Ugeni kucheza na Celta de Vigo na ushindi kwao utawashusha Barca hadi Nafasi ya Tatu.


Rossi, Kulia akishangilia bao lake baada ya kumfunga kipa wa Barca Victor Valdes

S

J
Meneja wa  Barcelona Gerardo Martino akiwanyooshea mkono Valladolid
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Machi 8

Real Valladolid 1 vs  Barcelona 0
20:00 Real Betis vs Getafe CF
22:00 Celta de Vigo v Atletico de Madrid
23:59 Granada CF v Villarreal CF Jumapili Machi 9 14:00 RCD Espanyol v Elche CF 19:00 UD Almeria v Sevilla FC 21:00 Real Madrid CF v Levante 23:00 Valencia v Athletic de Bilbao Jumatatu Machi 10 22:00 Osasuna v Malaga CF 23:59 Real Sociedad v Rayo Vallecano
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya kufunga bao la nne na la mwisho, Bao mbili zikifungwa na Demba Ba katika dakika za mwishoni na ndani ya muda mfupi. Chelsea wameshinda bao 4-0. Ushindi huu ukiwaweka Kileleni zaidi kwa kupata pointi 66.
Eden Hazard akishangilia bao lake la mkwaju wa penati katika dsakika ya 60 kipindi cha pili baada ya Eto'o kuangushwa ndani ya 18 (ndani ya box) eneo hatari..Sense of humour: Eto'o aims his celebration at those saying he is too old for the Chelsea team
.

Kipindi cha pili dakika ya 56 Samwel Eto'o aliipatia bao safi baada ya kuwachomoka mabeki wa Spurs na kumfunga kipa wa Spurs. Dakika ya 60 mchezaji huyo huyo Eto'o ameangushwa kwa kufanyiwa rafu mbaya na Mchezaji wa Spurs Kaboul na mwamuzi wa mtanange huo Michael Oliver kumtoa kwa kadi nyekundu na mkwaju wa penati kutengwa kwenda lango la Spurs. Dakika za mwishoni dakika ya 88 na dakika ya 89 Demba Ba ameifungia timu yake Chelsea bao mbili za haraka! Bao la pili akilifunga dakika ya 89 baada ya Mchezaji wa Spurs kurudisha mpira nyuma kwa kichwa na hatimae Demba Ba kuwa kuwa karibu na kipa huyo na kumzunguka na kuupata mpira huo na kumfunga kipa wa Spurs bao hizo mbili za haraka na kwenye muda wa dakika za lala salama! Ushindi huu unawasogeza kileleni zaidi Chelsea kwa kufikisha pointi 66 wakifatiwa na Liverpool wenye alama 59.Hazard ndie aliyeutokomeza mkwaju huo ndani ya lango la Spurs na kufanya Chelsea wanaochezea kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge kuongoza kwa bao 2-0.
Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0 
Samuel Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa timu yake Chelsea.....' Meneja wa Chelsea Jose MourinhoAnimated: Chelsea boss Jose Mourinho gesticulates from the touchline during the game!Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard akikosa bao la wazi hapa huku kipa wa Spurs  Hugo Lloris akiwa nje ya lango lake.!!..
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Lampard (Oscar 46), Matic, Ramires, Hazard, Schurrle, Eto'o.
Subs: Mikel, Ba, Willian, Schwarzer, Kalas, Salah.
Booked: Lampard.
Goal: Eto'o 56, Hazard pen 60.
Tottenham: Lloris, Naughton, Dawson, Kaboul, Vertonghen, Sandro, Bentaleb, Walker, Sigurdsson (Paulinho 61), Lennon, Adebayor.
Subs: Soldado, Townsend, Chadli, Friedel, Fryers, Kane.
Booked: Bentaleb, Naughton, Sandro.
Sent off: Kaboul.
Referee: Michael Oliver

waliotembelea blog