Tuesday, September 1, 2015


Manchester United wametoa Taarifa kuhusu Uhamisho ulioshindikana Dakika za mwisho kwa Kipa wao David De Gea kuhamia Real Madrid baada ya kulaumiwa na kukana kabisa kuwa si kosa lao. Mapema Leo Real Madrid walitoa Taarifa yenye Vipengele 10 wakiwashutumu Man United kwa kuchelewesha Uhamisho hadi Dirisha la Uhamisho kufungwa huko Spain.
Kutokana na hilo, De Gea anabaki Mchezaji wa Man United hadi mwishoni mwa Msimu huu Mkataba wake utakapomalizika.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA MAN UNITED:
Manchester United inafahamu kuhusu Taarifa ya Real Madrid kuhusu jaribio lao kumsaini David De Gea na kumuuza Navas kwa Manchester United. Klabu imepata msukumo kutoa ufafanuzi kwa ukweli ufuatao:
-Manchester United haikuwatafuta Real Madrid kuhusu kumuuza David. David ni Mchezaji muhimu kwa Klabu na matakwa ya Klabu ni kutomuuza.
-Hakuna Ofa yeyote iliyopokelewa kwa ajili ya David hadi Jana.
-Jana Mchana, Real Madrid walitoa Ofa ya kwanza kumnunua David. Dili ikakubaliwa kati ya Klabu mbili ambayo pia ilihusu Navas kuhamia Old Trafford. Dili hii ilitegemea vitu hivyo viwili.
-Katika Masaa ya mwisho, Navas akiwa kambi ya mazoezi ya Real Madrid, wao ndio walikuwa wakihodhi Makabrasha yote ya David, Navas na Real Madrid. Manchester United wao walikuwa tu na Makabrasha ya Manchester United.
-Manchester United walituma Makabrasha ya Uhamisho kwa Wachezaji wote Wawili kwa Real Madrid Saa 20:42, Saa za Uingereza. Mikataba ya David ikarudishwa na Real Madrid bila ya kuwa na Ukurasa wa Saini Saa 2232, Saa za Uingereza.

-Saa 2240, Saa za Uingereza, zikibaki Dakika chache kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa huko Spain, yakaja mabadiliko makubwa kwenye Mikataba na kuhatarisha kukamilika kwake.

-Ilipofika Saa 2255, Saa za Uingereza, ndipo Mikataba yote iliyokamilika kuhusu David ikatumwa kwetu na Real Madrid.

-Wakati huo, Mikataba ya Navas ilikuwa haijarudishwa na Real Madrid.


KINDA wa umri wa miaka 19, Anthony Martial amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 36 kujiunga na Manchester United kutoka Monaco katika dili ambalo dau linaweza kupanda hadi Pauni Milioni 58.
Mchezaji huyo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ufaransa amesaini Mkataba wa miaka minne katika siku ya leo ya mwisho ya usajili.
Aliwasili mjini Manchester jana kwa vipimo vya afya  kabla ya kusaini Mkataba leo na kukabidhiwa jezi namba tisa Manchester United, huku Mkataba wake ukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja.
Manchester United imemtangaza rasmi Anthony Martial kutoka Monaco aliyesaini Mkataba wa miaka minne

The 19-year-old completed a £36m move to Old Trafford from French Ligue 1 club Monaco
The 19-year-old completed a £36m move to Old Trafford from French Ligue 1 club Monaco


Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3, mwaka huu. Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa TFF, Twiga Stars haikuondoka leo kuelekea nchini Congo – Brazzavile, Shirikisho bado linasubiri mwongozo wa Wizara ya Habari,Viajana, Utamaduni na Michezo. Imani ya TFF ni kuwa timu itasafiri na kuwahi mechi ili kuepuka hatari ya kuadhibiwa na CAF ikiwa ni pamoja nan a kulipishwa fainai au kuondolewa kwenye michuano


 Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. 
 MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.

NA K-VIS MEDIA
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema.
“Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua.

Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na gharama ya shilingi 174,392,000. 
Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.
Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka mgodi huo.
“Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.












Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba motto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Kikundi cha Kwaya ya Tujikomboe kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kamapeni uliofanyikakatika uwanja wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba mtoto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar Said Issa Mohamed (kushoto) akimtambulisha mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  kupitia Chadema, Juma Duni Haji wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Wafuasi wa Ukawa wakisukuma gari la mgombea Mwenza wa Ukawa kupia Chadema, Juma Duni Haji baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba motto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea wa ubunge  jimbo la Lindi mjini ikupitia CUF, Salum Barwani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi 
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kupitia Chadema, Juma Duni Haji (kulia), akimtambulisha mgombea wa ubunge wa jimbo la Liwale kupitia CUF, Zubery Kuchauka wakati wa mkutano wa kampeni ulifanyika kwenye uwanja wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kupitia Chadema, Juma Duni Haji (katikati) akiwaaga wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar Said Issa Mohamed (kushoto) akimtambulisha mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  kupitia Chadema, Juma Duni Haji wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akipokea kadi ya CCM kutoka kwa bibi, Razina Mwandachi baada ya kujiunga na Ukawa na kukabidhiwa kadi ya CUF wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akipokea kadi ya CCM kutoka kwa bibi, Razina Mwandachi baada ya kujiunga na Ukawa na kukabidhiwa kadi ya CUF wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Wafusi wa Ukawa wakiwa katika mkutano wa kampeni zamgombea mwenza wa urais wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji uliofanyika katika uwanja wa Maulidi uliopo wilayani Nachingwea.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwaaga wafuasi wa Ukawa mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Masasi kwenye uwanja wa Bomani ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
 Wakazi wa Masasi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini humo,Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Masasi kwenye uwanja wa Bomani ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
 Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoani Mtwara Ndugu Mohamed Sinan wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wakazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara. 
 Wananchi wa Nanyumbu wilayani Masasi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
  Wananchi wa Nanyumbu wilayani Masasi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo wilayani humo.
 Wananchi wa Nanyumba wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili na kuwahutubia
 Umati wa watu ndani ya uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia ndani ya mji huo.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwatambulisha wagombea udiwani wa Jimbo la Namtumbo.
  Wakazi wa Matemanga wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
  Wananchi wa Tunduru wakifurahia jambo kwenye mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Klabu ya soka ya Chelsea imefunga dirisha la usajili msimu huu kwani, kwa Uingereza dirisha la usajili lilikuwa limefungwe jioni ya Septemba 1 wakati kwa upande wa Hispania na Ufaransa wao dirisha la usajili lilifungwa usiku wa August 31.
1
Chelsea imemalizia usajili wake kwa kumsajili beki kutoka katika klabu ya Reading Michael Hector lakini imemsajili na kumuacha aendelee kucheza kwa mkopo katika klabu hiyo, Chelsea imeendeleza utamaduni wake wa kutoa wachezaji wengi kwa mkopo.
Michael Hector mwenye umri wa miaka 23 hadi anasajiliwa na Chelsea, alikuwa ameichezea klabu ya Reading mechi 49 katika mashindano yote, ikiwa ni pamoja na dakika 120 za mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA na kufungwa na klabu ya Arsenal.

Klabu ya Manchester United ya Uingereza ipo karibuni kumsajili mshambuliaji chipukizi kutokea Monaco ya Ufaransa, licha ya kuwa bado haijathibitika kuwa wamemsajili ila tayari Anthony Martial ameripotiwa kufanya vipimo vya afya katika klabu ya Manchester United.
453081752-e1407478205505
Anthony Martial anaripotiwa kusajiliwa na Man United kwa dau la pound milioni 36, kulingana na umri wake kuwa mdogo, kiasi hicho kinatajwa kuwa sio cha kawaida kiasi kwamba kimepelekea nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney kushituka kidogo na kumuuliza Morgan Schneiderlin kuhusiana na mshambuliaji huyo.
Martial-nvo
“Kiukweli wakati tupo katika ndege Wayne Rooney alikuja kuniuliza Martial ni nani? kwa sababu magazeti ya Uingereza yalikuwa yakimzungumzia, nilimwambia ni mchezaji mzuri ana uwezo mkubwa  na alicheza mechi kadhaa na Monaco msimu uliyopita na mwanzoni mwa msimu huu”>>>Morgan Schneiderlin
“Nilimwambia Rooney kiufundi yupo vizuri na anafananishwa na Thierry Henry hata hivyo ni kwa mujibu wa magazeti ndio yanayomfananisha na Henry”>>> Morgan Schneiderlin
Anthony-Martial-Monaco
Anthony Martial ni mchezaji mwenye umri wa miaka 19 hivyo wengi ulinganisha kiasi cha fedha na umri wake, kwani mara nyingi mchezaji anaye nunuliwa kwa dau kama hilo ni mchezaji mkubwa au kama mdogo ni lazima awe na uwezo mkubwa, hivyo ndio maana Rooney amebidi aulize kuhusiana na mchezaji huyo.

waliotembelea blog