Sunday, July 14, 2013


Uchaguzi uliofanyika jana  Jumapili, Julai 14, 2013 wa kuwapata madiwani wa Kata Nne --Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai-- za mkoani Arusha umemalizika.

Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne kama ifuatavyo:

KATA YA THEMI: CHADEMA 678; CCM 326; CUF 313

KATA YA KIMANDOLU: CHADEMA 2,665; CCM 1,169

KATA YA KALOLENI: CHADEMA 1,019; CCM 389; CUF 169

KATA YA ELERAI: CHADEMA 1,715; CCM 1,239; CUF 213

Vyama vingine vilivyoshiriki vilikuwa ni TLP, CCK na Demokrasia Makini.


                                Xavi akiwa na mkewe Nuria Cunillera 

Htimaye kiungo wa Klabu ya Barcelona ya Hispania Xavi Hernandez ameamua 
kuachana na ukapela kwa kumuoa mchumba wake wa muda mrefu Nuria Cunillera, 
ndoa iliyofungwa siku ya jumamosi usiku huku ikihudhuriwa na wachezaji wenzake akiwemo gwiji Lionel Messi.
Shuhudia jinsi mambo yalivyokuwa katika picha
MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu, Ijumaa Wikienda lina mtiririko wote.

Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
 

Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.
HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.

UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.
Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’ anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana.

KIBOYA NA JUMA NATURE
Nature akimpa mkono Jay

AY aki mpa pole Jay

Jose Mara akimpa pole Jay

Stive Nyerere Akimpa Pole Jay

Joh Makini

Roma Mkatoliki

Dude

Fid Q

Wakazi


Majani

Izzo Bizness

Quick Rack

Mwana FA

Shetta

B-12

Bob Junior

Kala Jeremiah

Wachezaji wa Miembeni wakisalimia waamuzi pamoja na wachezaji wenzao wa timu ya kagondo
Salama!! karibu Kagasheki Cup 2013: Timu zikisalimiana na kufamiana
Kagondo nao wakisalimiana na waamuzi
Kikosi cha Timu ya Miembeni
Benchi la Miembeni na wachezaji wa akiba
Benchi la Kagondo

Waamuzi wakiteta na timu kapteni hapa kuhusu jambo fulani na kuona wapi wanaelekea.
:


Shilole alipata nafasi ya kutengeneza video ya wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina 'NAKOMAA NA JIJI' baada ya kumaliza majukumu yaliyo mleta U.S.A.
Sehemu ambayo aliipendekeza video hiyo itengenezwe ni New York na ndoto hiyo ilitimia baada ya kupata studio ya kumtengenezea video yake.
Pita taswira za location zilizotumika katika video hiyo akiwa katika jiji la New York.



Hapa Shilole akiwa ndani ya usafiri uliotumika katika video yake hiyo mpya
Akijiandaa kwa 'make up' mitaa ya Downtown Brooklyn Barclays Center




Shilole akifanya mambo yake mbele ya Video Camera
Masanja akiwa sambamba na Camera Man kuhakikisha Shilole anapata kitu kilicho bora kabisa.
Habari ndiyo hiyoo kaeni mkao wa kula video hii itakuwa baaaaabukubwa ......
Shilole ndiyo habari ya mujini
Kwa picha zaidi za location zilizotumia katika video hiyo bofya read more
Wimbo wake mpya huo unatamba sasa katika radio station za Tanzania.
Hapa Shilole alipata company ya mtoto huyo aliomba kucheza na Shilole baada ya kuvutiwa na jinsi Shilole alivyokuwa akicheza
Shilole akicheza na mtoto alie omba kucheza nae mtoto huyo alivutia na jinsi Shilole alivyo kuwa anacheza. Baadae katoto ka watu kalilala na kuomba afanyiwe massage maana alijinyonga nyonga utadhania kashikwa na kichomi.
Hapo Shilole akipata ukodak na jamaa ambae alivutiwa na jinsi alivyo kuwa ana cheza katika harakati za kutengeneza video yake
.
Hapa Shilole anaonekana amechoka utadhani kakimbizwa na kinyonga mwenye kwikwi vile. Hapa ilikuwa location ya mwisho Time Square New York City.



waliotembelea blog