Friday, April 10, 2015


Chelsea wako mbioni kuvunja Rekodi ya Manchester United na kuweka Historia ya kuwa ndio Timu iliyojikita kileleni kwa Siku nyingi katika Msimu mmoja.
Msimu huu, Kikosi cha Jose Mourinho kimekaa karibu Siku zote kileleni mwa Ligi au kufungana na ni rasmi tangu Agosti 30 ndio walikaa kileleni na mwishoni mwa msimu huu wataweka Rekodi ya kuwa juu kwa Siku 274 ikiwa watabaki Nambari Wani.
Msimu huu, ni Tottenham Hotspur pekee iliyookaa kileleni baada ya kufungana kwa Pointi na Chelsea baada ya Mechi 2 na wao kuzidi Ubora wa Magoli.
Manchester United ndio inayoshikilia Rekodi ya kukaa Siku nyingi kileleni walipokaa Siku 262 kwenye Msimu wa 1993/94 na Chelsea wanaweza kuipita hapo Mei 13.
Nae Mourinho ametamka: "Msimu huu imekuwa kawaida kwetu kuwa kileleni. Kutwaa Ubingwa tunahitaji kushinda Gemu 5 na Sare 1!"
Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele na Mechi 1 mkononi na Jumapili wanacheza huko Loftus Road kwenye Dabi ya London ya Magharibi na QPR inayopigana kutoshuka Daraja.
Mchezaji makeke wa QPR, Joey Barton, ameeleza: "Hii ni zaidi ya Dabi kwetu. Wao wanawafikiria Manchester United na Arsenal kwani ndio wenzao. Kwetu sisi ni Mechi kubwa kutokana na hali yetu. Wao ni Mabingwa Watarajiwa lakini tumeona nini kilitokea kwa City na Crystal Palace! Wakitupa Pointi 3 tutafurahi! "

LIGI KUU ENGLAND-Rekodi ya Siku za kukaa kileleni:
-Manchester United Msimu 1993/1994 Siku 262
-Chelsea 2005/2006 Siku 257
-Manchester United 2006/2007 Siku 250
-Manchester United 2000/2001 Siku 241
-Chelsea 2014/2015 Siku 230
-Arsenal 2003/2004 Siku 216
-Newcastle United 1995/1996 Siku 212
-Chelsea 2009/2010 Siku 204
-Chelsea 2004/2005 Siku193
-Manchester United 2012/2013 Siku 191

 Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.(KWA HISANI YA MICHUZIBLOG)
 Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
 Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.
 
IMG-20150410-WA0026 
Artist:Lady jaydee Ft Mazet&Uhuru
Song: Give me love
Producer:Uhuru
Support Jaydee, Support Our Own


DSC_0616
Aneth Kushaba AK 47(katikati) akiimba na waimbaji wenzake wa bendi ya Skylight ambao ni Ashura Kitenge(kushoto) na kulia ni John Music kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kucheza moja ya Sebene la Kikongo pamoja Sony Masamba.
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kulia ni Sam Mapenzi na kushoto ni Joniko Flower
Waimbaji wa Skylight Band wakiimba kwa moja ya nyimbo za bendi yao kwenye kiota cha Thai Village ijumaa iliyopita.

Sugua sugua mpaka itakate……Waimbaji wa Skylight Band wakicheza moja ya style zao zinazobamba mujini.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Burudani ikiendelea kutolewa na wasanii wa Skylight Band.
Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK 47(kushoto) pamoja na John Music (kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa hisia pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sugua Sugua mpaka utakate njoo leo ujifunze kusugua kama hawa mashabiki wa Skylight walivyojua mmoja ya Style ya kusugua
Sam Mapenzi akiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight band (hawapo pichani) huku akisaidiwa na waimbaji wenzake wa kwanza kushoto ni Ashura Kitenge akiwa smambamba na Sony Masamba(wa pili kutoka kushoto) pamoja na John Music (wa kwanza kulia) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akikabidhiwa Jezi ya Bacelona namba 14 ya mchezahji wa zamzni akiwa kocha Johan Cruyff (kushoto)wakati wa hafla fupi ya chakula jioni  iliyofanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar timu hiyo ilipokutana na Rais.[Picha na Ikulu) CRU2


Robin van Persie amejitangaza kuwa yupo vizuri kwa mchezo wa jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester city.
Van Persie amekosekana michezo sita ya Manchester united kutokana na kuumia enka wakati Man Utd walipopoteza kwa 2-1 dhidi ya Swansea tarehe 21 mwezi wa pili.

Kocha Louis van Gaal wiki iliyopita alisema hakutegemea Van Persie kupona kwa haraka hivyo na kua vizuri kupambana na city jumapili ijayo pale Old Traffod,lakini Van Persie mwenyewe alijitangaza kwa mashabiki na kuwaambia yupo vizuri.
Hata kama van Gaal akifikiria kumpa nafasi katika mechi yao ya upinzani wa jadi dhidi ya city bado ni ngumu sana kuona jinsi gani ataendana na kasi na mfumo wa sasa ya kitika kikosi cha kwanza
Pengo la mholanzi ambae amefunga magoli 10 tu msimu huu halikuonekana kabisa pale alipoumia,na tangu alipoumia man united imepoteza mchezo mmoja tu tena dhidi ya mabosi wake wa zamani Arsenal kombe la FA.

United walipata ushindi katika ratiba ngumu dhidi ya Tottenham na Liverpool na jumamosi iliyopita ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa ushindi uliofanya kuwa juu ya city kwa pointi moja.
Wayne Rooney alifunga goli moja matata kwa mkwaju wa haja,kapteni huyo wa united amekua na kiwango bora kabisa pale mbele katika mfumo wa 4-3-3 akisaidiana na Ashley Young na Juan Mata ambae aliingia nyavuni mara mbili katika ushindi wa 2-1 pale Anfield wiki mbili na nusu zilizopita.
Marouane Fellaini pia anatoa mchango mkubwa katika majukumu ya kiungo na ushambuliaji sehemu ambayo kwa sasa imetulia sana kwenye kikosi hicho cha Manchester united.
 Ushindi dhidi ya city iliyopoteza mwelekeo na kuwa chini ya kiwango utaongeza wigo wa pointi kufikia nne na kuongeza matumaini ya Van Gaal kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.Mata na Ander Herrera

waliotembelea blog