Friday, April 10, 2015


Chelsea wako mbioni kuvunja Rekodi ya Manchester United na kuweka Historia ya kuwa ndio Timu iliyojikita kileleni kwa Siku nyingi katika Msimu mmoja.
Msimu huu, Kikosi cha Jose Mourinho kimekaa karibu Siku zote kileleni mwa Ligi au kufungana na ni rasmi tangu Agosti 30 ndio walikaa kileleni na mwishoni mwa msimu huu wataweka Rekodi ya kuwa juu kwa Siku 274 ikiwa watabaki Nambari Wani.
Msimu huu, ni Tottenham Hotspur pekee iliyookaa kileleni baada ya kufungana kwa Pointi na Chelsea baada ya Mechi 2 na wao kuzidi Ubora wa Magoli.
Manchester United ndio inayoshikilia Rekodi ya kukaa Siku nyingi kileleni walipokaa Siku 262 kwenye Msimu wa 1993/94 na Chelsea wanaweza kuipita hapo Mei 13.
Nae Mourinho ametamka: "Msimu huu imekuwa kawaida kwetu kuwa kileleni. Kutwaa Ubingwa tunahitaji kushinda Gemu 5 na Sare 1!"
Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele na Mechi 1 mkononi na Jumapili wanacheza huko Loftus Road kwenye Dabi ya London ya Magharibi na QPR inayopigana kutoshuka Daraja.
Mchezaji makeke wa QPR, Joey Barton, ameeleza: "Hii ni zaidi ya Dabi kwetu. Wao wanawafikiria Manchester United na Arsenal kwani ndio wenzao. Kwetu sisi ni Mechi kubwa kutokana na hali yetu. Wao ni Mabingwa Watarajiwa lakini tumeona nini kilitokea kwa City na Crystal Palace! Wakitupa Pointi 3 tutafurahi! "

LIGI KUU ENGLAND-Rekodi ya Siku za kukaa kileleni:
-Manchester United Msimu 1993/1994 Siku 262
-Chelsea 2005/2006 Siku 257
-Manchester United 2006/2007 Siku 250
-Manchester United 2000/2001 Siku 241
-Chelsea 2014/2015 Siku 230
-Arsenal 2003/2004 Siku 216
-Newcastle United 1995/1996 Siku 212
-Chelsea 2009/2010 Siku 204
-Chelsea 2004/2005 Siku193
-Manchester United 2012/2013 Siku 191

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog