Tuesday, April 14, 2015



Arturo Vidal aliipatia bao dakika ya 57 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati na kuitanguliza bao 1-0 dhidi ya As Monaco. Ricardo Carvalho alioneshwa kadi ya njano baada ya kumfanyia rafu mbaye eneo la penati Álvaro Morata.VIKOSI:
Juventus 11: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Vidal, Pirlo, Marchisio, Pereyra, Tevez, Morata
Akiba: Storari, Barzagli, Padoin, Sturaro, Pepe, Llorente, Matri
Monaco 11: Subasic, Raggi, Carvalho, Abdennour, Kurzawa, Fabinho, Kondogbia, Moutinho, Carrasco, Martial, Dirar
Akiba: Stekelenburg, Elderson, Wallace, Matheus, Silva, Berbatov, Germain

Monaco boss Leonardo Jardim
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Robo Fainali-Mechi za Kwanza
Jumanne Aprili 14

Atlético Madrid vs Real Madrid
Refa: Milorad Mažić (Serbia)

Uwanja: Estadio Vicente Calderón, Madrid, Spain
Juventus vs AS Monaco
Refa: Pavel Královec (Czech Republic)

Uwanja: Juventus Stadium, Turin, Italy

Vuta ni kuvute katika kipindi cha pili...Kipindi cha kwanza kimemalizika hakuna aliyeliona lango la mwenzake licha ya Timu ya Real kuliandama kwa wingi lango la Atletico Madrid.VIKOSI:
Atletico Madrid Wanaoanza:
Oblak, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira, Gabi, Mario Suarez, Koke, Arda, Griezmann, Mandzukic
Atletico Akiba: Moya, Gamez, Gimenez, Tiago, Raul Garcia, Saul Niguez, Torres
Real Madrid Wanaoanza: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Kroos, Modric, James, Bale, Ronaldo, Benzema
Real Akiba: Navas, Pepe, Arbeloa, Khedira, Isco, Illarramendi, Jese


Ronaldo
chumaaChid Benz ameamua kuonyesha ukali wake kwa mara nyingine tena na hii kawahusisha wakali wengine wa hiphop Nikki Mbishi na One,wimbo huu umeanza kutengenezwa ka Lamar kisha umemaliziwa kwa Songa.
7
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa




 Kagera Sugar imeshinda mechi tano Uwanja wa Kambarage tangu ihamishie maskani yake mjini Shinyanga ikitokea Mwanza ilikopoteza mechi tatu mfululizo na kulazimika kuhama.’ KAGERA Sugar FC imesahihisha makosa ya kufungwa 2-1 dhidi ya Simba SC wiki iliyopita baada ya kuilaza Ruvu Shooting Stars mabao 2-0 katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
 OKWI

Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar FC inayonolewa na Mganda Jackson Mayanja, imeendelea kubaki nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikifikisha pointi 31 baada ya mechi 22, pointi nne nyuma ya Simba SC inayokamata nafasi ya tatu baada ya mechi 21.
Kikosi cha Mkenya Tom Olaba cha Ruvu Shooting Stars kimeendelea kubaki nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kikiwa na pointi 26 baada ya mechi 22.
Victor Hangaya amefunga bao la kwanza la Kagera dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Atupele Green kuongeza la pili katika dakika ya 51 na kuihakikishia Kagera Sugar FC ushindi wa tano Uwanja wa CCM Kambarage msimu huu tangu wahamishie maskani yake mjini Shinyanga ikitokea Mwanza Januari mwaka huu.
Kagera Sugar FC imelazimika kuishi mithili ya kumbikumbi kwa kuhamaha msimu huu kutokana na ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, unaofandhiliwa na FIFA.
Katika mechi ya leo kikosi cha Kagera kimemkosa mshambuliaji wake tegemeo mwenye magoli 10 msimu huu, Rashid Mandawa kutokana na mchezaji bora huyo wa mwezi Novemba wa ligi hiyo kuwa na kadi tatu za njano.
Simba
Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC, imepigwa faini ya sh. 300,000 na TFF kupitia kamati yake ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu mara baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.  Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao. Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.  Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi.
Katika hatua nyingine pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.


Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa Mchezaji wao Raheem Sterling hakuonyesha nidhamu ya Mwanamichezo baada ya kuibuka Picha akivuta Mtemba maarufu kama Shisha ambao unadhaniwa kuwa na Gesi inayolewesha 'Nitrous Oxide.'
Picha za Sterling akivuta Shisha zilizagaa Jana huko England kwenye Vyombo vya Habari na baadae kuibuka Picha nyingine zikimwonyesha Staa huyo wa Miaka 20 ambae pia huchezea England akiwa 'amezimika.'
Akiongea mara baada ya Jana Liverpool kuifunga Newcastle 2-0 na kupanda hadi Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England huku Sterling akifunga Bao la kwanza, Rodgers amesema: "Ukiwa Mwanamicheza wa kiwango cha juu hupaswi kufanya hivyo. Nitaongea nae na kumsikia anasemaje."
Rodgers amekiri kuwa Wachezaji Vijana Siku zote hufanya makosa lakini kikubwa ni kujifunza toka makosa hayo.

cde42378-2688-46e1-a4cc-8e558cbbe70f-1020x612 
Zimefanyika kampeni mbalimbali duniani kote kupinga tukio la wasichana waoaminiwa kutekwa na kundi la kigaidi la Boko haramu nchini Nigeria, wasichana ambao walitekwa wakiwa shuleni.
Leo Jumanne ya April 14 2015 watu mbalimbali Nigeria wameandamana kimya kimya huku wakiwa wameziba midomo katika jiji la Abuja pamoja na mabango yenye #BringBackOurGirls.. leo ni mwaka mmoja tangu wasichana  247 wa shule  moja Chibok watekwe na  kundi la Boko Haram huku wakiwa na mabango yenye ujumbe uliosomeka
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema ingawa hawezi kuthibitisha kama wasichana hao wataweza kuokolewa lakini Serikali itafanya kila njia kuhakikisha wasichana hao wanapatikana.
Hapa nina hizi PICHAZ ambazo zinaonesha maandamano hayo leo NIGERIA.
bb1 


BB4-600x450

BB5 



BB2-600x450



BB4 




BB7-600x450

waliotembelea blog