Tuesday, April 14, 2015


Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa Mchezaji wao Raheem Sterling hakuonyesha nidhamu ya Mwanamichezo baada ya kuibuka Picha akivuta Mtemba maarufu kama Shisha ambao unadhaniwa kuwa na Gesi inayolewesha 'Nitrous Oxide.'
Picha za Sterling akivuta Shisha zilizagaa Jana huko England kwenye Vyombo vya Habari na baadae kuibuka Picha nyingine zikimwonyesha Staa huyo wa Miaka 20 ambae pia huchezea England akiwa 'amezimika.'
Akiongea mara baada ya Jana Liverpool kuifunga Newcastle 2-0 na kupanda hadi Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England huku Sterling akifunga Bao la kwanza, Rodgers amesema: "Ukiwa Mwanamicheza wa kiwango cha juu hupaswi kufanya hivyo. Nitaongea nae na kumsikia anasemaje."
Rodgers amekiri kuwa Wachezaji Vijana Siku zote hufanya makosa lakini kikubwa ni kujifunza toka makosa hayo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog