Thursday, July 16, 2015



AEA
Tuzo za African Entertainment Awards (AEA) ni Tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa nia ya kutambua watu wanaotoa mchango mkubwa katika uliwengu wa burudani. Tuzo hizi zinalenga hasa kuonyesha ukubwa  na fursa zilizopo kwenye ulimwengu wa burudani Africa.
Tuzo hizi zinahusisha reception ya red carpet, live performace za wasanii, live performance za comedy na ofcoz kutolewa kwa Tuzo kwa wasanii wanaowania Tuzo hizi kwenye vipengele husika.
Tuzo za mwaka huu ziko njiani zikiwa na vipengele 27 na good news kwa Tanzania ni kwamba wasanii wetu wamo pia. Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ni wasanii pekee kutoka Tanzania waliopata fursa ya kutuwakilisha kwenye Tuzo hizi.
DP
Diamond Platnumz anawania tuzo ya Hottest Male Single of the Year pamoja na Best Male Artist of the Year huku Vanessa Mdee akiwania tuzo ya Best Female Artist of The Year. Tuzo zitafanyika kwenye ukumbi wa Mary Burch Theater , New Jersey.
Nimekusogezea orodha kamili ya wale wote wanaowania tuzo hizi mwaka huu hapa chini.
BEST COLLABORATION OF THE YEAR:
1. TIMAYA FT SEAN PAUL – SHAKE YOUR BUM BUM
2. STAR BOY FT LAX AND WIZZ KIDD- CARO
3. DYNASTIE LE TIGRE FT STANLEY ENOW PRENDS SOIN D’ELLE (MR ADRENALINE)
4. SARKODIE – ADONAI FT. CASTRO
5. DJ DARCIE FEAT DANIEL NASCIMENTO, PRETOSHOW AND MAYA ZUDA
HOTTEST FEMALE SINGLE OF THE YEAR:
 1. TINASHE- 2 ON
2. YEMI ALADE – JOHNNY
3. ZAHARA- LLOLIWE
4. MAYA ZUDA- KWANKWARAM
SELMOR MTUKUDZI – NGUVA YANGU
HOTTEST MALE SINGLE OF THE YEAR:
1. DAVIDO- AYE
2. FALLY IPUPA- ORIGINAL
3. DIAMOND-NTAMPATA WAPI – Tanzania**
4. DILLON FRANCIS- GET LOW
5. R2BEESE- LOBI
BEST MALE ARTIST OF THE YEAR:
1. DIAMOND PLATIMUNZ – Tanzania**
2. FALLY IPUPA
3. EDDY KENZO
4. WIZ KID
6. SARKODIE
BEST MUSIC VIDEO OF THE YEAR:
 1. YEMI ALADE- JOHNNY
2. TOOFAN- GWETA
3. EDDIE KENZO- SITYA LOSS
4. STONEBWOY – PULL UP (REMIX) FT. PATORANKING
5. JOVI – ET P8 KOI (DIRECTED BY NDUKONG)
BEST HIP HOP ARTIST AND SONG:
1. TEHN DIAMOND- HAPPY
2. A.K.A- SIM DOPE
3. REMINICE- SKILASHI
4. STANLEY ENOW – HEIN PÈRE (OFFICIAL VIDEO) BY SHAMAK ALLHARAMADJI
5. JOVI – B.A.S.T.A.R.D FT. RENISS
6. FRENCH MONTANA- JULIUS CAESAR
HOTTEST GROUP:
1. MAFIKIZOLO
2. P-SQUARE
3. SAUTI SOL
4. TOOFAN
BEST FEMALE ARTIST OF THE YEAR:
1. YEMI ALADE
2. VANESSA MDEE – Tanzania**
3. VICTORIA KIMANI
4. BUCIE
BEST GOSPEL GROUP:
1. JOYOUS CELEBRATION (PERFORMANCE BY MINISTER TAKESURE)
2. SONNIE BADU
3. BONNIE DEUSCHLE AND CELEBRATION CHOIR
4. KANVEE ADAMS
BEST MALE MODEL:
1. STANIEL FERREIRA
2. DAVID AGBODJI
3. DERICK TWUM
4. JADON ANDERSON
5. ADONIS BOSSO
BEST FEMALE MODEL
 1. LIYA KEBEDI
2. ALEK WEK
3. ATAUI DENG
4. OLUCHI ONWEAGBA
5. AJUMA NASENYANA
BEST COMEDIAN
 1. COMRADE FATSO
2. BASKET MOUTH
3. TREVOR NOAH
4. KANSIIME ANNE
5. MICHAEL BLACKSTON
BEST NEW AND UPCOMING ARTIST:
 1. STONE BWOY (PULL UP (REMIX) FT. PATORANKING
2. OFISHAL XAVIER (CHECK YOUR BALANCE)
3. OS DETROUA – BELA
4. YOK7 – BROWN SKIN GIRL
BEST PRODUCER OF THE YEAR
 1. BRIAN SOKO – DRUNKEN IN LOVE
2. KILL BEATZ – LOBI
3. DJ OSKIDO
BEST ACTOR IN A FILM OR SERIES
 1. TONGAYI CHIRISA – CRUSO
2. NONSO ANOZIE – GAME OF THRONES
3. ADHIR KAYLAN – RULES OF ENGAGEMENT
4. BENJAMIN OCHIENG – X FILES
BEST ACTRESS IN A FILM OR SERIES
 1. DANAI GURIRA- THE WALKING DEAD
2. KANDYSE MCCLURE- HEMLOCK GROVE
3. YVONNE ORJI-FIRST GENERATION
4. SOPHIE OKONEDO- SINBAD
BEST FEMALE ACTRESS IN A MOVIE:
1. BENU MABHENA – BLOOD DIAMOND
2. LUPITA NYONG’O- 12 YEARS A SLAVE
3. YVONNE NELSON- SINGLE MARRIED AND COMPLICATED
4. CHALIEZE THERON-A MILLION WAYS TO DIE IN THE WEST
BEST MALE ACTOR IN A MOVIE:
 1. DAVID OYELOWO – SELMA
2. DJIMON HOUNSOU – BLOOD DIAMOND
3. EDI GATHEGI- X-MEN FIRST CLASS
4. CHIWETELU EJIFOR-HALF OF THE YELLOW SUN
5. DAYO OKNIYI-ENDLESS LOVE
BEST FILM WITH STRONG AFRICAN PRESENCE
 1. BLOOD DIAMOND
2. SELMA
3. HALF OF THE YELLOW SUN
4. 12 YEARS A SLAVE
COMMUNITY AWARD
1. IYA BEKONDO- THE IYA FOUNDATION
2. CLAUDINE MUKAMABANO- KUKI NDIHO/ WHY DO I EXIST? RWANDA ORPHANS SUPPORT PROJECT
3. SYLVIE BELLO- CAMEROON AMERICAN COUNCIL
4. KATIE MEYLER- MORE THAN ME
5. LIYA KEBEDE FOUNDATION
6. NNAMDI ASOMUGHA- ASOMUGHA FOUNATION
ENTREPRENEUR OF THE YEAR
 1. FARAI GUNDAN- FARAI MEDEIA GROUP, ENTREPRENEUR MEDIA GURU
2. CHRISTIAN NGAN-MADLIN CZALIS
3. OLAMIDE OREKUNRIN-FLYING DOCTORS NIGERIA
5. RUPERT BRYANT- WEB AFRICA
MALE SPORTING PERSONALITIES
S 1. LUC RICHARD MBAH A MOUTE- NBA
2. YAYA TOURE-SOCCER
3. SAMUEL ETO-SOCCER
4. NNAMDI ASOMUGHA, NFL
5. MEHDI BENATIA-SOCCER
6. SERGE IBAKA-NBA
FEMALE SPORTING PERSONALITIES
 1. REGINA GEORGE-TRACK AND FIELD
2. TALISA LANOE-SWIMMER
3. MESELECH MELKAMU-TRACK AND FIELD
4. MARSHA COX (MARSHA MARESCHIA)
5. NICOLE BANECKI-SOCCER
6. NICHOLE DENBY-TRACK AND FIELD
HUMANITARIAN AWARD
HUMANITARIAN AWARD AKON
MALE FASHION DESIGNER
 1. ARMANDO CABRAL-OWN SHOE BRAND
2. STANLEY IGWILO- XTAN COUTOURE
3. MATTHEW RUGAMBA-HOUSE OF TAYO
4. LAURENCE CHAUVIN BUTHAUD- LAURENCEAIRLINE
FEMALE FASHION DESIGNER:
 1. CATHERINE HENRY-HENRIOCI
2. KIBONEN NFI- KIBONEN NY
3. AUDREY NGO MBOG-UZURI COUTURE
4. FARAI SIMOYI – DESIGNER OF THE NIKKI MINAJI FASHION COLLECTION
BEST AFRICAN RESTAURANT
 1. MASSAWA, ETHIOPIA & ERITREA (NYC)
2. LE SOUK, MOROCCO (NYC)
3. ABUJA, WEST AFRICAN (NJ)
4. B&B AFRICAN RESTAURANT-WEST AFRICA (NJ)
5. CASA LA FEMME-EGYPTIAN (NYC)
Mwisho wa kuwapigia kura VeeMoney pamoja na Diamond Platnumz ni tarehe 30 mwezi Agosti, na kuwapigia kura wawili hawa tembelea link hii hapa: https://www.surveymonkey.com/s/VOTEAEA2015 na kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea website yao: www.africanentertainmentaward.com., au kuwafollow Instagram @africanentertainmentawards.



overhead-view-hotel
Mwonekano wa juu ya chumba, kwa chini unaona mto, mashamba na barabara kwa mbalii..
Wako watu ambao kupanda jengo la ghorofa moja tu ni tatizo, unadhani atakubali kirahisi kabisa kulala hapa juujuu?
cliff-hotel
Labda ukiwa hapo utaenjoy zaidi kuona mazingira poa ya nje, Milima iliyozunguka, mto na nyumba za watu.. lakini swali ni hili moja; utakuwa na amani hata ya kupata usingizi?
Karibu sana ndani ya Peru mtu wangu, hiki ni chumba cha Hoteli ya Natural Vive, vyumba viko vingi juu ya Mlima kwenye urefu kama wa futi 400 hivi toka chini, ukilipia Dola yako 1,000 ambayo ni kama Tshs. Milioni 2 zinatosha kukabidhiwa funguo ya chumba chako na utaenjoy siku nzima kuwa hapo juu.
2015-07-12T070439Z_912071196_GF10000156697_RTRMADP_3_MEXICO-GUZMAN - Copy
Hapa ni mwonekano wa ndani ya chumba.
scary-see-through-suspended-pod-hotel-peru-sacred-valley-81



Ndani ya masaa 72 tu mahusiano mazuri kati ya golikipa wa Manchester United Victor Valdes na kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal yamevunjika, tofauti kati yao ilianza wakati Valdes alipogoma kucheza kikosi cha wachezaji wa akiba.
Maswali yalianza kutawala baada ya Valdes kuenguliwa na David de Gea kujumuishwa kikosini licha ya kuhusishwa pia na story kwamba ana mpango wa kuihama klabu hiyo, katika kikosi kilichosafiri na timu kwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya.
Valdes ameachwa na timu na wengi walianza kudhani labda kaachwa sababu ya majeruhi kabla ya Van Gaal kufichua ukweli katika kikao na waandish wa habari jumatano hii Marekani.
Lakini sasa majibu kamili ya nini kimetokea kati ya wawili hao kimejulikana, Van Gaal amemuacha Valdes kwa sababu hataki kufuata falsafa zake hivyo ni mtovu wa nidhamu na hana nafasi katika kikosi chake.
“hafuati falsafa zangu, hivyo hakuna nafasi ya mtu kama huyo”>>> Van Gaal
Van Gaal anamtuhumu Valdes kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kucheza mechi na kikosi cha wachezaji wa akiba akiba msimu uliopita. Kufuatia mvutano huo Valdes kuna uwezekano mkubwa wa kutoendelea kuvaa jezi ya Manchester United msimu ujao.


chelsea11
Chelsea ndio mabingwa wa ligi kuu ya England msimu uliomalizika..saa hivi tayari wameanza maandalizi ya kutetea ubingwa wao kwa mara nyingine na wameamua kusafiri hadi Canada kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo.
Hapa kuna Pichaz 10 jinsi wachezaji walivyowasili Canada…
chelsea
chelsea10
chelsea11
chelsea12
chelsea13
chelsea2
chelsea3 

chelsea4
chelsea6 

chelsea9


Real Madrid ndio timu tajiri zaidi kwa mwaka wa tatu mfululizo kulingana na jarida la biashara la Forbes.
Kilabu hiyo ya Uhispania ina thamani ya pauni bilioni 2.08 huku timu ya soka ya Marekani Dallas Cowboys na ile ya New York Yankees zikichukua nafasi ya pili kwa pamoja na thamani ya pauni bilioni 2.04.
Mahasimu wakubwa wa Real Madrid Barcelona wanachukua nafasi ya nne wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.02.
Kilabu ya Manchester United iko katika nafasi ya tano kutoka nafasi ya tatu mwaka uliopita.
Nafasi nyengine zilizosalia katika kumi bora zinachukuliwa na timu za michezo nchini Marekani.

Timu nyengine za ligi ya Uingereza ni Mancity iliopo katika nafasi ya 29 ikiwa na thamani ya pauni milioni 890,Chelsea ikiwa na thamani ya pauni milioni 877 inachukua nafasi ya 31 na Arsenal yenye thamani ya pauni milioni 839 ikiwa katika nafasi ya 36.


Nigeria imemchagua aliyekuwa mchezaji wa Nigeria Sunday Oliseh kocha mpya wa Nigeria.
Oliseh mwenye umri wa miaka 40 ameweka kandarasi ya miaka mitatu na anamrithi Stephen Keshi ambaye alifutwa kazi mwanzo wa mwezi Julai.
''Tuna vipawa vya kubadilisha hatma yetu ili kurudisha heshima tuliokuwa nayo na kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri'',alisema Oliseh.

''Hii ni kazi kubwa barani Afrika,tukiungwa mkono na kila mtu tunaweza kuisadia Super Eagles kupaa tena''.
Oliseh aliyeichezea Nigeria mara 63 na kuisadia kushinda kombe la Afrika mwaka 1994 pamoja na dhahabu katika mashindano ya Olimpiki mwaka 1996 anachukua wadhfa huo wakati ambapo Nigeria wanapambana kuimarika nje na hata ndani ya uwanja.


Charles Misheto anaingia katika headline tena ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kitanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania, taarifa hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tu toka aliyekuwa beki wa Simba B Emily Mugeta kujiunga na klabu ya Neckarsulm ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi daraja la tano.
Charles Misheto amejiunga katika klabu ya Rabestein ya Ujerumani inayoshiriki Ligi daraja la nne kwa mkataba wa miaka miwili… Hii sio mara ya kwanza kwa Charles kucheza soka nchini humo, aliwahi kucheza katika klabu ya Melbtiz ya nchini humo.
Hata hivyo Charles amewahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga na inashiriki ligi kuu Tanzania bara.
“Ingawa awali nilikuwa nafanya majaribio na timu nyingine, lakini sasa nimefanikiwa kusajiliwa na timu nyingine ya daraja la nne ambayo ilianza kuniwania”>>>> Charles
“Nilikuja hapa, nikafanya nao mazoezi kwa siku mbili, baada ya hapo wamekubaliana na uwezo wangu tumesaini mkataba”>>> Charles
Hii ni habari njema kwa watanzania wote wapenda soka na maendeleo hivyo anaingia katika orodha ya baadhi ya wachezaji wa kitanzania wanaocheza soka nje ya nchi, baadhi yao kama Abdi Kassim anayecheza Malaysia na Mwinyi Kazimoto anayecheza Qatar .



Unamkumbuka Rivaldo? unakumbuka alichofanya katika michuano ya World Cup 2002, Vipi unamkumbuka yule mtoto aliyemzaa miaka 23 iliyopita? unakumbuka kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi bora cha Brazil katika kipindi cha miaka kumi kikiwa kimesheheni mastar kama Ronaldinho, Cuf, R.Carlos, Lucio, Gilberto, Ronaldo, Edmilson, R .Junior, Kleberson? Basi yupo kwenye headlines tena na mtoto wake mtu wangu
Nguli wa soka wa Brazil Rivaldo (43) usiku wa jana aliingia katika headlines za soka baada ya kucheza mechi na mtoto wake Rivaldinho na wote kufunga magoli katika mechi moja.
Headlines hapo mtu wangu sio tu kufunga wote katika soka ila ni Rivaldo kurejea tena uwanjani na kuifungia bao timu hiyo baada ya kutangaza kuustafu 2014 lakini hivi karibuni alirejea tena uwanjani na klabu yake ya Mogi Mirim iliomlea toka 1992-1994 ambayo pia kwa sasa yeye ni raisi wa klabu hiyo.

Rivaldo ambaye alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya mwanaye Rivaldinho kufunga bao la kwanza kwa kichwa na baadae kufunga la tatu na kuipa ushindi timu yao wa magoli 3-1 dhidi ya Macae, yaani mtu wangu ni mchezo ambao ulitawaliwa na baba na mwana tu.
Rivaldo alimzaa Rivaldinho 1995 akiwa na umri wa miaka 23 wakati huo ambao alikuwa anaitumikia klabu ya Palmeiras ya Brazil.
Mtu wangu nimekuwekea video ya magoli waliofunga Rivaldo na mwanaye hapo chini.



Zahara Michuzi alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.
Zahara Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger na mpiga picha hodari wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamalizia muda wake sasa.
Binti wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.


Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.

Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora

waliotembelea blog