Thursday, July 16, 2015



Unamkumbuka Rivaldo? unakumbuka alichofanya katika michuano ya World Cup 2002, Vipi unamkumbuka yule mtoto aliyemzaa miaka 23 iliyopita? unakumbuka kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi bora cha Brazil katika kipindi cha miaka kumi kikiwa kimesheheni mastar kama Ronaldinho, Cuf, R.Carlos, Lucio, Gilberto, Ronaldo, Edmilson, R .Junior, Kleberson? Basi yupo kwenye headlines tena na mtoto wake mtu wangu
Nguli wa soka wa Brazil Rivaldo (43) usiku wa jana aliingia katika headlines za soka baada ya kucheza mechi na mtoto wake Rivaldinho na wote kufunga magoli katika mechi moja.
Headlines hapo mtu wangu sio tu kufunga wote katika soka ila ni Rivaldo kurejea tena uwanjani na kuifungia bao timu hiyo baada ya kutangaza kuustafu 2014 lakini hivi karibuni alirejea tena uwanjani na klabu yake ya Mogi Mirim iliomlea toka 1992-1994 ambayo pia kwa sasa yeye ni raisi wa klabu hiyo.

Rivaldo ambaye alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya mwanaye Rivaldinho kufunga bao la kwanza kwa kichwa na baadae kufunga la tatu na kuipa ushindi timu yao wa magoli 3-1 dhidi ya Macae, yaani mtu wangu ni mchezo ambao ulitawaliwa na baba na mwana tu.
Rivaldo alimzaa Rivaldinho 1995 akiwa na umri wa miaka 23 wakati huo ambao alikuwa anaitumikia klabu ya Palmeiras ya Brazil.
Mtu wangu nimekuwekea video ya magoli waliofunga Rivaldo na mwanaye hapo chini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog