UDAKU WA USAJILI
Winga wa nchi ya Wales Gareth Bale, 24,
alipanda ndege kurudi
toka Hispania na kuzungumza na
Manchester United kabla ya kukamilisha
uhamisho
wake wa kuvunja rekodi wenye thamani ya £86m kwenda Real
Madrid.
Manchester United, Chelsea, Arsenal na
Tottenham wanaweza
kuhusishwa na wasiwasi wa
hatma ya Andrea Pirlo akiwa Juventus
. Kiungo
huyo Muitaliano, 34, anaweza kuruhusiwa
kuondoka mwezi januari endapo
Klabu
hiyo yaya jijini Turin haitamwongezea mkataba.
Chelsea wanataka kumsajili Beki
wa Porto Eliaquim Mangala,
22, katika dirisha
la usajili la mwezi Januari. Klabu ya Monaco
pia
wameonyesha nia ya kutaka
kumsajili Beki huyo wa kati wa Kifaransa.
Beki wa Manchester United Rafael,23,
anafikiria kurudi
Brazil, akiwa na Corinthians
klabu ambayo Beki huyo wa kulia anaweza
kuhamia.
Athletic Bilbao wameonyesha nia ya kutaka
kumsajili beki wa
Chelsea Cesar Azpilicueta
mwezi Januari. Beki huyo wa Kihispania, 24,
amecheza mechi moja tu akitokea benchi msimu huu.
Arsenal na Juventus wameonyesha kuvutiwa na
Beki wa Red Bull Salzburg mwenye
asili ya Austria Martin Hinteregger, 21.
UDAKU MWINGINE
Meneja wa zamani wa Brighton Gus Poyet amefanya
mazungumzo
na Mmiliki wa Sunderland Ellis
Short kuhusu kuwa mbadala wa
Paolo Di
Canio ndani ya dimba la Stadium of Light. Steve McClaren na
Tony Pulis
pia wako katika mbio za kugombania hiyo kazi.
Kocha wa zamani wa Manchester City
Roberto Mancini yupo kayika nafasi nzuri kuwa
mbadala wa Fatih Terim ndani ya Galatasaray.
Meneja wa Norwich Chris Hughton anaweza
kufukuzwa kazi ikiwa timu yake itafungwa na Stoke Jumapili.
Mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 31
, atakuwa
anapata mshahara wa jumla ya kitita cha
£12.6m kwa mwaka, badala ya
mshahara wa £11.6m,
baada ya kuongeza mkataba na Paris St-Germain.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema hatasita
kumtumia
Mshambuliaji Luis Suarez dhidi ya
Manchester United ndani ya Old
Trafford siku ya
Jumatano baada ya kufungiwa mechi kumi.
Gareth Bale amepanga kwenye nyumba ya Kaka nchini
Hispainia.
Real Madrid walimpatia Bale mkataba wa
makubaliano na Kiungo huyo
wakibrazili, 31, ambaye amerudi AC Milan.