Monday, August 31, 2015



Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Oliver Giroud ambaye wengi wamekuwa wakimlaumu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuwa hawezi kutwaa ubingwa akiwa na mshambuliaji huyo pekee, wengi walikuwa wakishinikiza Wenger amsajili Karim Benzema.
August 31 Oliver Giroud amekutana na maswali ya waandishi wa habari kuhusu klabu yake ya Arsenal kuhusishwa kutaka kusajili mshambuliaji mpya. Oliver Giroud ana majibu haya kuhusiana na Arsenal kutaka kumsajili mfaransa mwenzake Karim Benzema na yeye mtazamo wake kuhusu usajili huo.
gun__1412060818_social_giroud
“Ni kweli kila mwaka huwa kuna tetesi za kusajiliwa mshambuliaji mpya, kuna msimu ambao tulimsajili Sanchez, Welbeck na wengine lakini tulikuwa tukizungumza kuhusiana na Suarez, ni kawaida kwa klabu kuna mengi ya kutarajiwa, najua mashabiki wanataka tusajili kwa fedha nyingi”>>> Giroud
“Hilo sio swali ninalopaswa kujibu mimi, kocha anajua vizuri nini anafanya, wakati mwingine hutakiwi usajili tu ili mradi na wakati mwingine kuna kuwa hakuna mchezaji unaye muhitaji, tukiachana na hayo itakuwa vizuri kama Karimu angesajiliwa”>>> Giroud
Olivier-Giroud-Karim-Benzema-601898
Klabu ya Arsenal ya Uingereza ilikuwa ikihusishwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, ambapo Arsenal walikuwa wapo tayari kutoa pound milioni 50 ili kumpata staa huyo kabla ya siku kadhaa nyuma, staa huyo kuthibitisha kuwa hayupo tayari kuondoka Real Madrid.



Tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Uingereza, nimeona nikukumbushe wachezaji watano waliowahi kusajiliwa kwa fedha nyingi saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Mesut Ozil – 2013

Ikiwa saa kadhaa zilikuwa zimesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa Uingereza mwaka 2013, klabu ya Arsenal iliridhia kutoa pound milioni 42.4 kumsajili kiungo wa Kijerumani aliyekuwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Mesut Ozil na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Arsenal-2014-Season-in-Pictures

Fernando Torres na David Luiz 2011

Baada ya misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Liverpool Fernando Torres mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea ya London kwa pound milioni 50 kwa wakati huo ilikuwa ni rekodi kubwa ya usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza. Lakini Torres alishindwa kuonyesha makali yake Chelsea kwani alicheza mechi 110 na kufunga goli 20. Siku hiyo hiyo aliyosajiliwa Torres ndio siku aliosajiliwa beki wa Kibrazil David Luiz akitokea Benfica ya Ureno.
Roberto Di Matteo

Dimitar Berbatov 2008

Mwaka 2008 klabu ya Manchester United ilikamilisha uhamisho wa pound milioni 30.75 kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria Dimitar Berbatov kutokea klabu ya Tottenham Hotspur, hata hivyo uhamisho huo ambao ulifanywa na Man United ilikuwa ni sawa na wao walivyozidiwa kete na Chelsea kwa Pedro kwani Berbatov alikuwa ajiunge na Man City kabla ya Ferguson kumdaka Uwanja wa ndege.
Dimitar-Berbatov

Andy Carroll na Luis Suarez – 2011

Mwaka 2011 kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool  Kenny Dalglish aliwasajili kwa pamoja Andy Carrol kutokea klabu ya Newcastle United na Luis Suarez akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Andy-Carroll

Andrei Arshavin – 2009

Andrei Arshavin mshambulaiji wa kimataifa wa Urusi aliyetua katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa pound milioni 15 Zenit, licha ya Arshavin kushindwa kutamba katika klabu ya Arsenal na kitu pekee kikubwa alichowahi kufanya ni kuifunga Liverpool magoli manne.
Image_5_for_Arsenal_00_Fulham_gallery_98738532
Hiyo ndio kumbukumbu ambayo nimekukumbusha mtu wangu kwani hadi sasa tunategemea kuona lolote likitokea katika masaa machache yaliosalia ili kufungwa kwa dirisha la usajili la Ligi Kuu Uingereza.



Mtoto wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na nahodha wa klabu ya Manchester United Kai Rooney alionekana mwenye furaha, katika mapumziko ya mwisho wa wiki na mama yake mzazi Coolen Rooney wakiwa Hispania kwani alipata bahati ya kukutana na wachezaji wa FC Barcelona.
CNuEGMjWIAA71TR
Kai Rooney ambaye ni mtoto wa Wayne Rooney alionyesha kuwa na furaha kupata bahati ya kukutana na Lionel Messi, Suarez, Neymar na Pique hivyo mama yake aliamua kuiweka picha aliyopiga mtoto wake na mastaa hao katika mtandao wa twitter na kumshukuru beki wa zamani wa Man United

Sunday, August 30, 2015


Yakiwa yamebakia masaa takribani 72 kabla ya dirisha la usajili barani ulaya kufungwa, winga wa kibrazil Neymar ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na Man United hatimaye ametoa kauli yake.
 
Akizungumza baada ya mchezo wa ushindi wa 1-0 wa Barcelona dhidi ya Malaga, Neymar alisema: ‘Ningependa na nataka kuendelea kubaki Barcelona, haijalishi ofa ya mamilioni mangapi ya paundi kutoka England,’ aliiambia TV3.
‘Watu wangu wa Barca wanaweza kutulia na kuwa na amani.
‘Pale ninaposikia tetesi za kuhama kwangu, huwa sifikirii chochote. Huwa nasikiliza kisha naendelea na shughuli zangu. Nina furaha sana kuwepo Barca na wachezaji wenzangu.’ 
Neymar, 23, anatarajia kuongezewa mkataba wa miaka 5 huku akiwa kipengele cha kuuzwa endapo timu inayomtaka italipa kiasi cha  €250million (£182m).



Klabu ya Manchester City ya Uingereza ambayo ilikuwa ni moja kati ya vilabu vingi vilivyo kuwa vikihusishwa na kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Vfl Wolfsburg ya Ujerumani Kevin De Bruyne, August 30 imetangaza kumsajili rasmi.
Kevin-De-Bruyne-signs-for-Manchester-City
De Bruyne ambaye ana umri wa miaka 24 alisajiliwa muda mchache baada ya kufanyiwa vipimo vya afya, amejiunga katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka sita, Kuwasili Etihad kwa Kevin De Bruyne kunaweka rekodi mpya ya klabu hiyo kwani ndio atakuwa mchezaji wa gharama zaidi katika klabu hiyo.
PAY-Kevin-De-Bruyne-signs-for-Manchester-City (1)
De Bruyne amejiunga na Man City kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 54 na kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kwani kabla ya kuwasili klabuni hapo, Raheem Sterling ndio alikuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi zaidi, dau la pound milioni 49 lilitosha kumtoa Liverpool na kumleta Etihad.
Kevin-De-Bruyn-on-his-way-to-Manchester-from-Germany
Uhamisho wa kiungo huyo wa kibelgiji bado unakuwa haujavunja rekodi ya usajili ya wachezaji Uingereza kwani hadi sasa Man United ndio klabu pekee ambayo bado inashikilia rekodi ya usajili kwa dau kubwa baada ya kutumia pound milioni 59.7 kumleta Angel di Maria akitokea Real Madrid ya Hispania msimu uliopita.



Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo tayari kuwavaa Nigeria Septemba 05, 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017.

Mkwasa ambaye yupo nchini Uturuki na kikosi cha timu ya Taifa kambini kwa mazoezi ya takriban wiki moja, amesema vijana wameonyesha mabadiliko makubwa baada ya kupata wiki moja ya mazoezi ya pamoja.
“Mazoezi wanayofanya hapa yamewajenga stamina, unaweza kuona wanacheza kwa nguvu muda wote, wanakaba na kushambulia kwa pamoja, hii ni dalili nzuri ya vijana kuelekea katika mchezo huo dhidi ya Nigeria”amesema Mkwasa.
Kocha huyo wa timu ya Taifa amesema timu yake imefanya mazoezi katika nyanja zote ikiwemo mazoezi ya kujenga mwili na kucheza mpira wa kasi.
Aidha Mkwasa amesema kambi hiyo imekua na faida kubwa sana kiufundi, kufuatia kupata nafasi ya kukaa sehemu tulivu na wachezaji kuwapa mazoezi ambayo waliyapanga katika program hiyo ya kambi nchini Uturuki.

Taifa Stars imeendelea na mazoezi leo asubuhi, na inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kesho siku ya jumatau, kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
2-1Ayew akikatiza baada ya kuifunga bao la kusawazishaGomis  dakika ya 65 aliwapachikia bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Man United.
Kama ilivyokuwa Msimu uliopita, Leo tena Swansea City wametoka nyuma kwa Bao 1 na kuifunga Manchester United Bao 2-1 na kuishushia kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Kuu England kwa Msimu huu mpya.
Hadi Mapumziko, Mechi hii iliyochezwa huko Liberty Stadium, ilikuwa 0-0.
Dakika 3 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza Juan Mata aliipa Man United Bao ikiwa ni zawadi kwa kuitawala Mechi hii yote.
Hadi Daki ya 60 Man United walionekana ni washindi lakini Dakika 1 baadae Mchezaji wa Kimataifa wa Ghana, Andre Ayew, akaisawazishia Swansea na Dakika 5 baadae, Mtu wao hatari, Bafetimbi Gomis akawapa Bao la Pili na la ushindi.

A. Ayew kipindi cha pili aliwasawazishia bao Swansea kwa kichwa dakika ya 61 na kufanya 1-1.

Kipindi cha pili dakika ya 48 juan mata aliwapachikia bao la kuongoza Man United na kufanya 1-0 dhidi ya Swansea City. Shaw alipiga krosi iliyompata Rooney kwa kuugusa na hatimae Juan Mata kuunganisha moja kwa moja ndani ya nyavu za Swansea City.Cgupuchupu Swansea wapate bao hapa kipindicha kwanza! Kipindi cha kwanza kimemalizika hakuna aliyeliona lango la mwenzake, Ngoma ilimalizika 0-0 s Man United wala Swansea.
Swansea City wanahitaji Ushindi tena leo hii dhidi ya Man United, Je wataweza?
Depay akiendesha mpira.
Ligi Kuu England sasa inasimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea tena Septemba 12 na Man United wapo kwao Old Trafford kupambana na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool ambao Jana wakiwa kwao Anfield walinyukwa 3-0 na West Ham.VIKOSI:
Swansea wanaoanza 11:
Fabianski, Naughton, Fernandez, Williams, Taylor, Cork, Shelvey, Sigurdsson, Ayew, Routledge, Gomis
Akiba: Nordfeldt, Rangel, Bartley, Tabanou, Ki Sung-Yueng, Dyer, Eder
Manchester United wanaoanza 11: Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Schweinsteiger, Mata, Herrera, Memphis, Rooney
Akiba: Johnstone, McNair, Valencia, Carrick, Young, Fellaini, Chicharito




Yaya Toure analipwa pauni 220,000 akiwa na kikosi chake cha Manchester, hali ambayo inaonyesha kuumiza mioyo mingi ya Wazungu hasa Waingereza ingawa hawana kipaji kama chake.


Toure analipwa pauni 17,251 kwa siku ambayo ni sawa na Sh milioni 51 kwa shilingi ya Tanzania.


Si kwamba Toure analipwa tu, kazi yake ni ngumu kweli na imeendelea kuwa bora. Picha hizi mbili katika mechi dhidi ya Watford jana, zinaweza kuwa uthibitisho kwamba Braza anapambana kweli na anastahilia anacholipwa.


Angalia anavyochukua mkwanja kwa wiki, siku, saa. 


 MSHAHARA WA YAYA TOURE ULIVYO

 £220,000 kwa wiki
 £121,758 baada ya kodi kwa wiki
 £17,251 kwa siku
 £718.80 kwa saa
 £11.98 kwa dakika



MANCHESTER CITY (4-2-3-1): Hart 6; Sagna 6.5, Mangala 6, Kompany 6, Kolarov 6; Fernandinho 6, Toure 6.5; Sterling 7.5 (Iheancho 90), Silva 8 (Delph 75 6), Navas 5.5 (Nasri 45 6); Aguero 6.5 
Subs not used: Caballero, Demichelis, Roberts, Maffeo Becerra, Iheanacho
Scorers: Sterling 47, Fernandinho 56
Booked: Kompany

WATFORD (4-2-3-1): Gomes 6; Nyom 7, Prodl 6, Catchcart 6.5, Holebas 6.5; Behrami 7, Capoue 7 (Watson 76 6), Abdi 6 (Anya 63 6); Ighalo 6 (Layun 72 6), Jurado 6, Deeney 6
Subs not used: Arlauskis, Hoban, Diamanti, Vydra
Booked: Nyom, Prodl
Referee: Mark Clattenburg









30 Aug 2015



Na Saleh Ally, Kartepe
Kikosi cha Taifa Stars sasa kitaendelea na mazoezi mara moja tu kwa siku kwa siku zote zilizobaki za kambi yake hapa nchini Uturuki.


Stars imeweka kambi ya siku nane hapa Kartepe, Uturuki kujiandaa na mechi yake dhidi ya Nigeria itakayopigwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema watakuwa wakifanya mazoezi mara moja kwa siku wakiwa wamelenga zaidi masuala ya ufundi.

“Sasa tunaangalia ufundi zaidi huku kidogokidogo tunatunza fitness. Pia hatuwezi kufanya mazoezi makali sana kama ilivyokuwa mwanzo kwa kuwa tunakwenda kwenye mechi,” alisema Mkwasa.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akiwahutubia wananchi katika mkutano huo leo
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, alipohutubia katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo. 
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
w1
Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.w2
Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya  baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.w5w6
w3
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao.

waliotembelea blog