Monday, August 31, 2015



Tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Uingereza, nimeona nikukumbushe wachezaji watano waliowahi kusajiliwa kwa fedha nyingi saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Mesut Ozil – 2013

Ikiwa saa kadhaa zilikuwa zimesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa Uingereza mwaka 2013, klabu ya Arsenal iliridhia kutoa pound milioni 42.4 kumsajili kiungo wa Kijerumani aliyekuwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Mesut Ozil na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Arsenal-2014-Season-in-Pictures

Fernando Torres na David Luiz 2011

Baada ya misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Liverpool Fernando Torres mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea ya London kwa pound milioni 50 kwa wakati huo ilikuwa ni rekodi kubwa ya usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza. Lakini Torres alishindwa kuonyesha makali yake Chelsea kwani alicheza mechi 110 na kufunga goli 20. Siku hiyo hiyo aliyosajiliwa Torres ndio siku aliosajiliwa beki wa Kibrazil David Luiz akitokea Benfica ya Ureno.
Roberto Di Matteo

Dimitar Berbatov 2008

Mwaka 2008 klabu ya Manchester United ilikamilisha uhamisho wa pound milioni 30.75 kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria Dimitar Berbatov kutokea klabu ya Tottenham Hotspur, hata hivyo uhamisho huo ambao ulifanywa na Man United ilikuwa ni sawa na wao walivyozidiwa kete na Chelsea kwa Pedro kwani Berbatov alikuwa ajiunge na Man City kabla ya Ferguson kumdaka Uwanja wa ndege.
Dimitar-Berbatov

Andy Carroll na Luis Suarez – 2011

Mwaka 2011 kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool  Kenny Dalglish aliwasajili kwa pamoja Andy Carrol kutokea klabu ya Newcastle United na Luis Suarez akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Andy-Carroll

Andrei Arshavin – 2009

Andrei Arshavin mshambulaiji wa kimataifa wa Urusi aliyetua katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa pound milioni 15 Zenit, licha ya Arshavin kushindwa kutamba katika klabu ya Arsenal na kitu pekee kikubwa alichowahi kufanya ni kuifunga Liverpool magoli manne.
Image_5_for_Arsenal_00_Fulham_gallery_98738532
Hiyo ndio kumbukumbu ambayo nimekukumbusha mtu wangu kwani hadi sasa tunategemea kuona lolote likitokea katika masaa machache yaliosalia ili kufungwa kwa dirisha la usajili la Ligi Kuu Uingereza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog