Friday, October 18, 2013

1. DIAMOND 
 
KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU TIMU NZIMA YA THECHOICE ILIWEZA KUFANYA UTAFITI KWA KINA JUU YA KUFAHAMU WANAMUZIKI WA BONGO FLEVA WENYE MAFANIKIO ZAIDI KUTOKANA NA MUZIKI HUO,TIMU YA THECHOICE IMEWEZA PATA WANAMUZIKI WATANO WENYE MAFANIKIO ZAIDI KUTOKANA NA MUZIKI HUO.
NI MSANII ALIYE LETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MUZIKI HASAHASA KATIKA SHOW ZA STEJINI YAANI LIVE PERFORMANCE .NI MSANII ANAYE LIPWA PESA NYINGI KWA SASA TANZANIA KWA SHOW MOJA ANAYO FANYA.PIA NI MSANII MWENYE SHOW NYINGI KWA MWEZI KULIKO WOTE,.HII IMECHANGIA KUWEZA KUPATA PESA NYINGI KATIKA MDA MFUPI.ANAMILIKI NYUMBA KADHAA,VIWANJA,MAGARI,MADUKA.
DIAMOND

GARI ANAYO MILIKI YENYE THAMANI YA TSH.MIL 60

GARI ALIYO KUWA ANATEMBELEA MWANZO

2. LADY JAY DEE
NI MSANII MWENYE HESHIMA SANA TANZANIA KUTOKANA NA KUJIHESHIMU KWAKE,KAPATA MAFANIKIO SANA KATIKA KAZI ZAKE ZA MUZIKI NA KUWEZA KUWA MFANO WA KUIGWA KWA WASANII WENGINE.KWANI UCHAPA KAZI WAKE NDO SABABU YA MAFANIKIO YAKE KIMAISHA.
MALI ANAZOMILIKI NI PAMOJA NA -GARI AINA YA MURANO THAMANI YA 
TSH.MIL 45, BASI AINA YA COSTA TSH.MIL.30, PRADO, NYUMBA NZURI YA KISASA,PAMOJA NA MGAHAWA WA NYUMBANI LONGE WENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH.MIL.150 PIA ALIANZISHA MAJI YAKE YA JAY DEE AMBAYO BAADAYE YALIZUIWA.


NYUMBANI LONGE KWA NDANI

NYUMBANI LONGE KWA NDANI

MAJI YA JAY DEE


NYUMBA YA KISASA ANAYOISHI
BASI KWA AJILI YA BAND YAKE YA MACHOZI BAND
3.AY
  AY NI MSANII MKIMNYA SANA NA HUWA HAWEKI MAMBO YAKE HADHARANI SANA HASAHASA YA MAISHA YAKE.LAKINI NI MSANII MWENYE PESA NYINGI KUTOKANA NA KUFANYA SHOW NYINGI ZA KIMATAIFA ZINAZO MPATIA PESA NYINGI.ANAMILIKI MAGARI,ANA DUKA LA NGUA,PIA ANA NGUO ZAKE MAALUMU ZENYE NEMBO YA JINA LAKE.

4.PROF J 
NGULI WA MUZIKI WA BONGO FLEVA TANZANIA,ANAFANYA SHOW NYINGI ZA NJE,NI MSANII AALIYE DUMU KWA MDA MREFU,ANAMILIKI NYUMBA YA KISASA YA ZAIDI YA TSH.MIL 100, ANAMILIKI GARI,MASHAMBA
PROF.J
NYUMBA YA PROF J

MBELE YA NYUMBA
Mwanalizombe Studios Ni Recording Lebel Inayomilikiwa na Rapper Profesa Jay, Studio ipo msasani na Ameamua kuipa Jina la Mwanalizomba kwasababu Jay Ni mtu wa Ruvuma na Mwanalizombe maana yake ni Mwana Ruvuma na kufanya hivyo ameonyesha mapenzi ya mkoa wake wa Ruvuma. Producer kwenye studio hii ni Duke Touchez.
 Profesa ameshindwa kusema amewekeza kiasi gani cha fedha kwenye studio hio ila fahamu kuwa vifaa vilinunuliwa kwa wakati tofauti na ni vifaa vya hali ya juu sana.
AINA YA GARI ANAYO TEMBELEA


KWA NDANI

KWA NJE   

Profesa Jay akinionyesha jina la Saloon yake iliyoko Msasani mbele karibu
 ni mitaa ilipokuwa Irish Pub
 5.JUMA NATURE

 
MSANII WA SIKU NYINGI KATIKA GEMU,KWA JINA JINGINE NI MKONGWE KATIKA MUZIKI WA TANZANIA HUU WA KIZAZI KIPYA,ANAMILIKI GARI,MASHAMBA,PIA  NI MFANYA BIASHARA ,ANAMILIKI NYUMBA,TUNASHUKURU KWA TIMU NZIMA YA THECHOICE KWA KUFANYA UTAFITI HUU.TUTAENDELEA KUWALETEA VITU VIZURI ZAIDI KILA SIKU NA ENDELEA KUWA NASI.


STAA wa filamu za Kibongo Wema Sepetu amefunguka kuwa katika maisha yake aliwahi kufanyiwa mambo ya ushirikina(kurogwa) bila kufafanua alirogwa na nani na alipatwa na nini au ugonjwa gani.
Wema amefunguka kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa kila jumatano kupitia East African TV ambapo aliulizwa kama kama anaamini ushirikina upon a kama alishawahi kurogwa ambapo alijibu kuwa anaamini ushrikina upo ila haupi nafasi katika maisha yake kwani anamuamini Mungu.


‘Yaah!Nilishawahi kurogwa na naamini ushirikina upo ila siupi nafasi katika maisha yangu namuamini Mungu tu,’alisema Wema



KUZIMIKA kwa taa katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza juzi kulisababisha ndege ya fastjet kushindwa kutua na kulazimika kurejea jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kwamba ndege hiyo iliyopaswa kutua saa 2 usiku kwenye uwanja huo ikitokea jijini Dar es Salaam, ilishindwa

 kutua na kulazimika kuzunguka hewani mara tano, hali inayodaiwa kuleta taharuki miongoni mwa abiria.

Habari zinadai kuwa kukosekana kwa umeme katika uwanja huo kulisababisha kutokuwapo kwa mawasiliano, hivyo kuzua tafrani kubwa kwa baadhi ya abiria.

Baadhi ya abiria waliosafiri na ndege hiyo waliieleza Tanzania Daima kwamba wengi walikumbwa na hofu ya kuzama katika Ziwa Victoria.

“Tuliogopa sana baada ya kuona ndege imeanza kuzunguka zunguka angani, na tukahofia kuwa huenda tukatumbukia ziwani, maana uwanjani hakukuwa na umeme.

“Nilianza kusali huku mapigo ya moyo yakinienda mbio sana. Maana rubani angeweza kushuka ziwani kwa kuona taa za wavuvi,” alisema abiria mmoja ambaye hakutaja jina lake.

Hata hivyo, baadhi ya abiria na wadau wengine wa usafiri, akiwamo Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje na Meneja wa Shirika la Bima la Jubilee Mkoa wa Mwanza, Jared Owando, walieleza kusikitishwa na taarifa za kukatika kwa umeme kwenye uwanja wa ndege.

Walisema kwamba, kitendo hicho kinapaswa kudhibitiwa, ikiwa ni pamoja na uongozi wa uwanja huo kuwajibika kikamilifu, ili tatizo hilo lisijirudie tena, kwani hali hiyo ni hatari katika usalama wa abiria na ndege kwa ujumla: “Siku hiyo mimi nilifika Mwanza mapema usiku na ndege ya Precision kutoka Dar. Lakini baadaye nikaarifiwa kwamba kuna ndege imelazimika kurejea Dar es Salaam kwa sababu uwanja una giza. Sasa najiuliza, hakuna jenereta uwanjani hapo?” alisema Jared.

Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Easter Madale, alipoulizwa jana kwa njia ya simu kuhusiana na tatizo hilo, alikiri kutokea hitilafu ya umeme hivyo ndege hiyo kupata usumbufu ikiwa angani, na kusema hilo ni tatizo la kawaida: “Ni kweli siku hiyo kulikuwa na hitilafu ya umeme, hivyo mawasiliano yakakosekana! Umeme ulikatika na jenereta la TCAA halifiki huku kwetu…na sisi hapa jenereta yetu ni ndogo haina nguvu sana,” alisema meneja huyo.

Miaka kadhaa iliyopita iliwahi kutokea ajali mbaya, baada ya ndege ya mizigo kutoka Ulaya iliyokuja kubeba samaki kutumbukia ndani ya Ziwa Victoria, kutokana na kukosekana kwa umeme na mawasiliano uwanjani hapo.

--- via Tanzania Daima






















Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.

 
Mwingine aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji. Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.”
Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha 

Ommy Dimpoz akikamua ndani ya Dar Live.
...Mashabiki wakipagawa na Dimpoz. Joh Makini 'Mwamba wa Kaskazini' akilishambulia jukwaa la Dar Live. Wanenguaji wa Twanga wakionesha manjonjo. Mwamba wa Kigamboni, Bahati Chaz ‘Mr B’ akishusha mistari ya hip hop Dar Live. Masai wa Kigoma akifanya makamuzi.
Baadhi ya mashabiki baada ya kupandisha mizuka.
Twanga wakikamua stejini.Mwanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ 
Rama Pentagon akikamua na bendi yake.
Mtaalam wa mazingaombwe, Profesa Calabash akiichoma moto fulana.

waliotembelea blog