ALIEKUWA Meneja wa Southampton Mauricio Pochettino ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Tottenham Hotspur kwa Mkataba wa Miaka Mitano.
Pochettino, mwenye Miaka 42, aliteuliwa kuwa Meneja wa Southampton hapo Januari 2013 alipombadili Nigel Adkins na Msimu huu amewafikisha Nafasi ya 8 kwenye Ligi Kuu England iliyomalizika Mei 11, na kabla uteuzi huu wa Leo wa kwenda Tottenham, alijiuzulu wadhifa wake wa Southampton.
Pochettino anamrithi Tim Sherwood alietimuliwa mapema Mwezi huu.
Raia huyu wa Argentina anakuwa Meneja wa 10 wa Tottenham tangu Mwaka 2001.
Waliokuwa Wasaidizi wa Pochettino huko Southampton, Jesus Perez, aliekuwa Meneja Msaidizi, Kocha wa Timu ya Kwanza, Miguel D'Agostino, na Kocha wa Makipa, Toni Jimenez, wote wanaungana nae huko Spurs.Roberto Soldado kuuzwa?
KUHUSU POCHETTINO:
-Kazaliwa 2 Machi 1972 huko Santa Fe, Argentina
-Alichezea Klabu za Newell's Old Boys, Espanyol, PSG na Bordeaux
-Akiwa na Espanyol alitwaa Copa del Rey mara 2: 1999/2000 na 2005/06
-Ameichezea Argentina mara 20 na kufunga Bao 2
-Aliteuliwa Meneja wa Espanyol Januari 2009.
-Aliteuliwa Meneja wa Southampton hapo Tarehe 18 Januari 2013
-Alifanikiwa kuzitwanga Manchester City, Liverpool na Chelsea kwenye Ligi