Tuesday, December 22, 2015

HUKU kukiwa na tetesi kuwa Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward amekuwa na Kikao mahsusi cha kujadili hatima ya Meneja wao Louis van Gaal kwenye Ofisi yao ndogo Jijini London na pia Sir Alex Ferguson kudaiwa kuombwa ushauri wa nini kifanyike, zipo habari nzito kuwa Klabu hiyo itafanya uamuzi mgumu muda si mrefu.
Zipo habari zinazodai kuwa Louis van Gaal atapewa Mechi 2 zijazo kurekebisha mwelekeo wa jahazi lakini zipo dalili pengine hata huo muda haupo.

Balaa kwa Louis van Gaal lilianza mara baada ya kuifunga Watford Bao 2-1 hapo Novemba 21 na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu England lakini tangu wakati huo hawajashinda hata Mechi 1 katika 6 walizocheza na kujikuta wakipigwa mara 3 mfululizo na pia kung’olewa kwenye 4 Bora ya Ligi.
MAN UNITED
Mechi zijazo za Ligi:
Desemba 26: Stoke City vs Man United
Desemba 28: Man United vs Chelsea
Januari 2: Man United vs Swansea City
Zipo tetesi kuwa hata Wachezaji wa Man United, hasa wale Maveterani, hawafurahishwi na uongozi wa Van Gaal huku Wachambuzi wengi wakidai Mdachi huyo sasa amepitwa na wakati na kinachomweka juu tu ni sifa zake alizozoa nyuma kwenye Historia yake.
Wapo wanaosema Van Gaal atang’oka na Msaidizi wake Ryan Giggs kupewa ukaimu hadi mwishoni mwa Msimu na Giggs akifanya vizuri katika kipindi cha ukaimu hapo ndipo atakuwa wa kudumu . 

Lakini pia zipo taarifa zinazodai Jose Mourinho, alietimuliwa na Chelsea Alhamisi iliyopita, ndie atashika wadhifa wa Umeneja wakati wowote kuanzia sasa.
Hadi sasa hamna mwenye uhakika nini kitajiri Man United na Klabu yenyewe haijazungumza chochote kama kawaida yao.
Wapo Wachambuzi wanaokumbushia jinsi David Moyes alivyotimuliwa Msimu wa 2013/14 ingawa dalili zilikuwepo kwa muda kwamba anaishi kwa Siku za kuhesabika lakini aliachwa kwenye wadhifa hadi Mwezi Aprili ilipofikia hatua kuwa Man United hawatafuzu tena 4 Bora na hivyo kutocheza UEFA CHAMPIONS LIGI na ndipo akafukuzwa.
Hadi sasa, kwa Man United, ndoto ya kumaliza ndani ya 4 Bora bado ipo hai lakini nani atakubali kila kukicha ni vipigo tu?



MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amedai ushindi wao dhidi ya Man City ambayo ni moja ya Timu inayotegemewa kutwaa Ubingwa wa England umewapa imani kubwa ya kuwa Mabingwa.
Arsenal hawajatwaa Ubingwa tangu 2004 lakini Jana Uwanjani kwao Emirates Bao za Theo Walcott na Olivier Giroud za Kipindi cha Kwanza ziliwapa ushindi licha ya City kupata Bao mwishoni kupitia Yaya Toure na kutishia kuigeuza Gemu lakini Arsenal waligangamala na kushinda 2-1.
Baadae, Wenger, mwenye Miaka 66, alisema: "Ushindi umetufanya tujiamini, umetupa nguvu na imani."

Aliongeza: "Sasa Kikosi kimekomaa na hilo lilionekana wakati wa Gemu tulipokuwa kwenye presha."
Sasa Arsenal wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 4 mbele ya Man City walio Nafasi ya 3 na wako Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City.
Hii inamaanisha Arsenal wanakwenda Krismasi wakiwa Nafasi ya Pili na mara 5 kati ya 6 walizotwaa Ubingwa wa England kwa mara ya mwisho walitwaa Ubingwa wakiwa Nafasi ya Pili wakati wa Krismasi.

Mechi zijazo za Ligi kwa Arsenal:
Desemba 26 Southampton vs Arsenal
Desemba 28 Arsenal vs Bournemouth
Januari 2 Arsenal vs Newcastle



LIGI KUU ENGLAND Usiku huu imemalizia Raundi ya Mechi zake za 17 kuelekea zile Mechi mfululizo za mwishoni mwa Mwaka kwa mtanange uliochezwa Emirates Jijini London wa Timu ambazo hasa ndizo zinapewa nafasi za kutwaa Ubingwa kwa Arsenal kuifunga Manchester City Bao 2-1.
Dakika 90 zimekamili 2-1 Arsenal waibuka kidedea...2-0

Ushindi huu umewabakisha Arsenal Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City wakati City wakiwa Nafasi ya 3 Pointi 4 nyuma ya Arsenal wakifuatiwa na Spurs na Man United ambazo ziko Pointi 3 nyuma huku kila Timu ikiwa imecheza Mechi 17.
Arsenal walitangulia kufunga katika Dakika ya 33 baada ya pasi ya Mesut Ozil kumkuta Theo Walcott Winga ya kushoto na kisha kumhadaa Fulbeki wa City, Bacary Sagna, na kuachia kigongo cha Mguu wa kushoto kilichomshinda Kipa Joe Hart na kutinga.

Dakika ya 45 Olivier Giroud aliipa Bao la Pili Arsenal baada ya kutengenezewa na Mesut Ozil
Hadi Haftaimu Arsenal 2 Man City 0.
Dakika ya 82 City walirudi kwenye Gemu na kuwa 2-1 kwa Goli la Yaya Toure kufuatia kupasiana vyema na yeye kumalizia vizuri kwa shuti la kupinda lililomhadaa Kipa Petr Cesc.
Kuanzia hapo City walikuja juu lakini Arsenal walisimama imara kulinda uongozi wao na kuibuka Washindi.

1-0Theo Walcott akipongezwa baada ya kufunga bao la kwanza.VIKOSI:
Arsenal starting XI:
Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Ramsey, Flamini, Walcott, Ozil, Campbell, Giroud
Arsenal subs: Gibbs, Gabriel, Ospina, Oxlade-Chamberlain, Chambers, Iwobi, Reine-Adelaide
Manchester City starting XI: Hart, Sagna, Otamendi, Mangala, Kolarov, Fernandinho, Toure, Delph, De Bruyne, Silva, Aguero
Man City subs: Sterling, Caballero, Bony, Jesus Navas, Clichy, Demichelis, Iheanacho

Hii ndiyo mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kabla ya sikukuu ya Krismasi. Arsenal wanakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye Uwanja wa Emirates jijini London. Mechi inasubiriwa kwa hamu kubwa, wengi wanaonekana kuipa nafasi Arsenal ingawa soka halina mwenyewe. Mechi tano zilizopita kwa kila timu, inaonekana Arsenal imeshinda mara nne na sare moja. Upande wa City, nao wameshinda mechi nne, wamepoteza moja. Si mechi ya mzaha wala hakuna anayeweza kuwa na uhakika kwa kuwa uwezo kwa timu hizo unaonekana kulingana kabisa na ndiyo zimekuwa zikibadilishana kiti cha kileleni


Funga Mwaka Concert 2015 (7)Funga Mwaka Concert 2015 (9)

Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (8)
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Funga Mwaka Concert 2015 (1)
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (3)Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.

Funga Mwaka Concert 2015 (4)
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (5)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Funga Mwaka Concert 2015 (6)
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Funga Mwaka Concert 2015 (18) Funga Mwaka Concert 2015 (19)
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Funga Mwaka Concert 2015 (20)
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (21)
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (22) Funga Mwaka Concert 2015 (23)Mashabiki wakiwa wamezingira gari la Diamond wakati akiondoka.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaahidi shoo ya nguvu mashabiki wake na kuwataka waje kwa wingi katika shoo kali ya kufunga mwaka itakayopigwa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar katika Sikukuu ya X-mas na kuwa hatawaangusha. Diamond anayetamba na ngoma ya Utanipenda ameyaongea hayo leo kwenye mkutano maalum uliofanyika Karume, Dar ambao ulihusisha waandishi wa habari na wapenzi wa muziki kwa ajili ya kuzungumzia shoo hiyo kubwa kuliko inayojulikana kama Funga Mwaka Concert. “Itakuwa ni Sikukuu ya Krismasi, sasa kwa nini tusifurahi pamoja, kama MTV wameamua kunipa tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika kwa hiyo sihitaji kuongea sana shoo itakuwaje siku hiyo, naomba mje kwa wingi kwa kweli sipendi kuwaudhi, nawaahidi sitawaangusha,” alisema Diamond au Baba Tiffah. Pia waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na kutambulisha listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku hiyo. “Mbali na Diamond pia kutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric pamoja na burudani nyingine nyingi. Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya. Shoo zitaanza asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima mpaka alfajiri,” alisema Mrisho. Viingilio ni Sh 15,000 na kwa V.I.P ni Sh 30,000 lakini wadhamini wakuu wa shoo hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel wakaamua kutoa ofa ya punguzo la bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi mpya za Airtel Money Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili mbalimbali. “Kadi za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila ya gharama yoyote tayari zipo zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala lakini kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa kwanza wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hiyo watakuwa na punguzo la Sh 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa 25,000,” alisema Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde. Habari: Hans Mloli,


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Askofu Godfrey Malassy (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22 Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua hiyo. Kulia ni Mwanakamati wa Jumuiya hiyo, Mchungaji Olivia Mallonga.
Mwanakamati wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Mchungaji Mchungaji Olivia Mallonga (kulia) akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22 Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa hayo Askofu Godfrey Malassy.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Askofu Godfrey Malassy akionyesha kitabu mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kilichozinduliwa na Jumuiya ya Makanisa hayo kinachohusu siri ya amani kwa taifa.

Mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba Akiwa anaimba mbele ya washabiki wake waliouthuria onyesho la bendi hiyo lililofanyika ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
Wanenguaji wa bendi ya Fm Academia wakifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha.
Washabiki wa bendi ya Fm Academia wakiwa wanacheza nyimbo ya heshima kwa wanawake iliyokuwa ikipigwa bendi hiyo.
Washabiki wa fm wakiwa waangalia show ya nguvu iliyokuwa inadondoshwa na bendi hiyo 
Mwanamziki wa kingombe blaise akiwa na mmoja wamashabiki wake waliouthuria show hivyo.
Washabiki wa bendi ya fm Academia wakiwa wanaendelea kucheza sebene la nguvu lilokuwa likidondoshwa na bendi hiyo.

DIAMOND (4) Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
UNATAKA kwenda shoo ya Diamond, Krismasi hii? Kama ndiyo, sasa unaweza kujipatia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo hiyo kwa kujibu maswali katika Gazeti la Uwazi kesho Jumanne pamoja na Risasi Mchanganyiko siku ya Jumatano. DIAMOND (3) 
Jinsi ya kushiriki, nunua gazeti lako la Uwazi au Risasi Mchanganyiko kisha jibu maswali kiufasaha ndani ya magazeti hayo katika kuponi maalum na washindi watano kila gazeti watajishindia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo ya Diamond itakayofanyika Krismasi katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Wanaoruhusiwa kushiriki ni wenye umri kuanzia miaka 18, shindano hili ni kwa watu waishio jijini Dar pekee.

waliotembelea blog