Thursday, June 25, 2015


Nathaniel Clyne yuko mbioni kujiunga na Liverpool baada ya Klabu yake Southampton kuikubali Ofa ya Pauni Milioni 12.5.
Clyne, ambae ni Fulbeki wa Kulia, anakuwa Mchezaji wa 6 kusainiwa na Liverpool katika kipindi hiki cha kuelekea Msimu mpya.
Uhamisho huu wa Clyne, mwenye Miaka 24 na ambae ameichezea England mara 5, utakamilika baada ya upimaji wa Afya yake na makubaliano ya maslahi yake binafsi.
Clyne atakuwa Mchezaji wa 4 kujiunga na Liverpool kutoka Southampton kufuatia wale waliojiunga Mwaka Jana ambao ni Adam Lallana, Dejan Lovren na Rickie Lambert.


Zipo ripoti nzito toka England zinazodai Meneja wa Manchester United Louis van Gaal na Kipa wa Tottenham Hugo Lloris wamefikia muafaka na Kipa huyo wa Kimataifa wa France ambae ameshakubaliana kuhusu maslahi yake binafsi huko Old Trafford.
Huku kukiwa na mipango ya chini chini ya Kipa Nambari Wani David de Gea kurudi kwao Spain kuidakia Real Madrid, kumchukua Hugo Lloris kunaelekea kuziba pengo hilo.Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi, Gazeti linaloheshimika huko France L'Equipe, kilichobaki sasa ni mazungumzo ya kukubaliana Ada ya Uhamisho na Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy.
L'Equipe imedai Levy amemhakikishia Lloris kuwa Klabu yeyote itakayotoa Ofa ya Pauni Milioni 18 kwenda juu basi atamruhusu kuhama White Hart Lane.Lloris, mwenye Miaka 28, alijiunga na Tottenham Mwaka 2012 akitokea Lyon ya France kwa Dau la Pauni Milioni 11.4.
Hata hivyo, Levy anasifika mno kwa ugumu wa kutoa Wachezaji wake Nyota na kama akiwaruhusu basi Dau lao huwa sio masihara.



Wakicheza kwao Estadio Nacional de Chile, Santiago, Chile wameifunga Mtu 9 Uruguay Bao 1-0 na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, COPA AMERICA.
Bao hilo la Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika Dakika ya 81 wakati Uruguay, Mabingwa Watetezi, wakicheza Mtu 10 baada ya Edinson Cavani kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 63 kufuatia Kadi ya Njano ya PIli.Cavani alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 29.
Katika Dakika ya 88 Uruguayl ilibaki Mtu 9 baada Jorge Fucile kupewa Kadi Nyekundu baada kujizolea Kadi za Njano mbili.
Kwenye Nusu Fainali, Chile watacheza na Mshindi kati ya Bolivia na Peru wanaocheza Usiku huu.
RATIBA
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24

Chile 1 vs Uruguay 0
Alhamisi Juni 25
Bolivia vs Peru (Saa 8:30Usiku)
Ijumaa Juni 26
Argentina vs Colombia (Saa 8:30Usiku)
Jumamosi Juni 27
Brazil vs Paraguay (Saa 6:30 Usiku)
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29

Chile vs Bolivia/Peru (Saa 8:30 Usiku)
Jumanne Juni 30
Argentina/Colombia vs Brazil/Paraguay (Saa 8:30 Usiku)

waliotembelea blog