Mwenyekiti wa Kamati ya
Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF) Bwana Farough Baghozah amekutana na waandishi wa habari katika
hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.
Katika kamati hiyo ya Taifa
ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu,
Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac
Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.
Pia Mwenyekiti amechukua
fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:
1. Maandalizi ya timu,
zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
Mwenyekiti – Imani
Madega
Wajumbe – Msafiri
Mgoyi,Teddy Mapunda.
2. Uhamasishaji wa mchezo
(Michezo ijayo) na Masoko
Mwenyekiti – Juma
Pinto
Wajumbe – Baraka
Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim Lundenga, Maulid Kitenge,
Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon, Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti – Farough
Baghozah
Wajumbe – Teddy Mapunda,
Michael Wambura, Imani Madega,
Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses Katabaro
na Edgar Masoud.
4. Mikakati ya ushindi –
itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo
Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon
Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.
Pia kamati imetangaza kauli
mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU”
itakayoanza kutumika kuanzia leo hii. Pia Kamati imemteua Bi Teddy
Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu inatarajia kuweka kambi
Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria
Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.
Aidha Mwenyekiti alitumia
nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze
kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa
nyumbani. Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na
mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati
Bwana Farough Baghouzah.