Thursday, August 27, 2015


Na Saleh Ally, Kartepe
Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa, kimeendelea na mazoezi kwenye moja ya viwanja vya The Green Park Hotel hapa katika mji huu mdogo wa Kartepe, Uturuki.


Mazoezi yalikuwa matamu na hizi ni picha 9 zilizopigwa kutoka mlimani na Saleh Ally 'Jembe' akitumia kamera yake ya kisasa kabisa, zinazoonyesha namna mazoezi yalivyokuwa nondo au shoka, ukizubaa umeumia.











Hi

 Miaka 35 iliopita nikiwa na umri mdogo sana. Wakati huo nikisoma nursery kwenye skuli ya Tanganyika... Nna kumbukumbu ya nusunusu juu ya pengine mchezo wangu rasmi wa kwanza kushuhudia wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo ilikuwa ikicheza na nchi ya Nigeria (Green Eagle's).


Nimeita kumbukumbu nusunusu sababu ya umri mdogo niliokuwa nao wakati huo. Lakini ktk nusu nnazozikumbuka. Nilipanda basi la timu ya taifa ambalo kama sikosei those dayz FAT (sasa tff) walikuwa wanalimiliki. 
STARS INAENDELEA KUJIFUA NCHINI UTURUKI

Nakumbuka timu iliondokea hoteli ya Africana na sisi tulikuwa kule for weekend na mzee ambaye inawezekana alinipigia pande kupanda basi la mashujaa wale ambao kwangu sitawasahau kamwe.

Nnazo kumbukumbu pia bendi ya DDC Mlimani Park ilitumbuiza kabla na wakati wa mapumziko katika mechi ile murua kabisa. Ingawa kwa siku zile sikujua kama wale ndio sikinde ngoma ya ukae!

Nusunusu yangu inanikumbusha kikosi kilichoanza game ile.
1-Juma Pondamali
2-Leopard Tasso Mukebezi
3-Hasan Zito Kiaratu
4-Jellah Mtagwa(C)
5-Ishaka Hassan Chukwu
6-Salim Amiri
7-Omari Hussein
8-Mohammed Rishard Adolph
9-Peter Tino
10-Mohammed Salum
11-Thuweni Ally


Kocha Mkuu alikuwa Joel Nkaya Bendera,
kwangu hii timu ambayo ilitoka kucheza fainali za mashindano ya Mataifa huru ya Afrika (Afcon) ilikuwa timu bora ya taifa kuwahi kuiona ingawa nilikuwa nusu mtu!

Timu hii ilimkosa nahodha wake mkuu Leodgar Chillah Tenga ambaye alikuwa ameumia kwenye mchezo  wa liliokuwa kombe maarufu siku hzo likiitwa Jengo Cup ambapo timu yake ya pan African ilicheza na yanga.

Bahati mbaya hyo ndiyo ilikuwa game ya mwisho rasmi kwa tenga ambaye aljeruhiwa vbaya sana goti na baba yangu mkubwa Kitwana Manara ‘Popat’.

Ifahamike hyo ilikuwa mechi ya mechi ya marudiano dhidi ya Maafrica Magharibi hao ambapo kwenye game ya kwanza kule Surulele Stadium Nigeria tulitoka suluhu bin suluhu.


Bahati mbaya kwetu wakatufunga mbili mtungi huku ikitajwa kukosekana kwa tenga kuliififisha defence line ya Stars. Siku hiyo alitumika defender chipukizi(wakati huo) Chukwu ambaye ndiye aliyeziba pengo la captain Tenga

Iwapo kama tungefanikiwa kuwatoa wala pilipili wale. Stars ilikuwa ikutane na Algeria ambao ndio waliofuzu kucheza Kombe la Dunia la Spain 1982,
Mungu jalia bahati haikuwa yetu. Lakini tulikuwa karibu kabisa na World Cup kuliko kipindi chochote cha uhai wa taifa hili!

Katika miaka yake yote ya uhai wa mataifa yetu mawili. Nchi hizi zmekutana mara tatu tu. Ukiacha game hizo za kufuzu kwa Kombe la Dunia. Stars na mwewe hawa washawahi kukutana pia kwenye mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa huru ya Africa (Afcon) pale Lagos na Stars tukalala 3-1.

Miaka ya mwishon mwa miaka ya 1990 tulicheza nao lakini ilikuwa kwenye mechi ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ambayo wachezaji wanaoruhisiwa kucheza ni wale walio chini ya miaka 23.

Mechi hizi pia wapo hao walitutoa na nakumbuka walikuja na nyota wao Tijan Babangida ambaye ni ndugu wa winga mahiri wa zamani wa ajax Amsterdam.


Nimeandika waraka huu mrefu kdogo ili itukumbushe shughuli tuliyo nayo mbeleni. Kwanza kihistoria baina yetu, pili kiuhalisia kuhusu uwezo wa kabumbu wa wapinzani wetu hawa ambao wamejaaliwa mamia ya wanasoka wanaocheza soka huko Ulaya.

Najua kwenye mpira lolote linawezekana. But tuendelee na maandalizi yetu huku tukiomba kwa Mungu pia, na hasa kheri tunaweza kuishangaza Afrika kwa kuwafunga manguli hawa wa kandanda si Afrika tu bali ulimwenguni kote.

Nimalizie kwa kuwataka radhi kwa errors mbili tatu.na kuwaomba sote kwa pamoja tuweke silaha chini kwa interest ya taifa letu



Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kilichopo kambini mjini Morogoro, kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya Morogoro mwishoni mwa wiki.

U-15 inayonolewa na kocha Bakari Shime, imeingia kambini mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya vijana hao kukutana kila mwisho wa mwezi na kucheza michezo ya kirafiki na kombaini za mikoa kwa lengo la mwalimu kutazama uwezo wa vijana wake na kuongeza vijana wengi atakaowabaini katika michezo hiyo.
Ikiwa mkoani Morogogoro, timu hiyo ya vjiana itacheza michezo miwili na kombaini ya mkoa huo ya vijana wneye umri chini ya miaka 15 siku za jumamosi na jumapili kabla ya kuvunjwa kwa kambi yao sikuya jumatatu.

TFF iliandaa utaratibu wa timu hiyo ya vijana kucheza michezo ya kirafiki kila mwisho wa mwezi ndani ya nchi, kabla ya mwezi Disemba kwenda katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa.

Lengo la kambi hiyo ni kuandaa kikosi bora cha vijana kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wneye umri chini ya miaka 17 (U17) zitakazofanyika nchini Madagascar.



Wakati Simba ikiwa kambini Zanzibar, watani wao Yanga nao wameamua kwenda visiwani humo kwa kambi ya mwisho kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.
Hilo limezua mjadala kwa nini timu hizo kongwe zenye upinzani mkubwa zimeamua kufuatana Zanzibar na imekuwa ikionekana kama huko ni maeneo ya Simba.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amezungumza na SALEHJEMBE na kuelezea sababu muhimu za Yanga kwenda Zanzibar.
"Tulichoangalia sisi ni utulivu wa kambi na uhakika wa sehemu za mazoezi. Lakini tumeangalia zaidi suala la kusogeza timu karibu na Wanayanga.
"Zanzibar ni sehemu yenye wanachama na mashabiki wengi wa Yanga, kihistoria Yanga ina mengi yanasomeka kutoka Zanzibar.
"Hata ukiangalia katika kikosi chetu tuna zaidi ya wachezaji wanne kutoka Zanzibar. Hivyo Zanzibar ni nyumbani kwa Yanga, kuweka kambi huko si tatizo hata kidogo," alisema Muro.
Yanga itafungua Ligi Kuu Bara Septemba 13 ambayo ni Jumapili kwa kuwa mwenyeji wa Coastal Union.
Mwezi April kulitokea tetemeko la ardhi Nepal, tetemeko ambalo liliua watu wapatao 9,000. Miongoni mwa watu waliokuwa wahanga wa tetemeko hilo ni kijana mwenye umri wa miaka 13 Jetin Shrestha ambaye wakati tukio hilo likitokea kijana huyo alikuwa akicheza mpira.
Ronaldo-main
August 27 Cristiano Ronaldo karudi tena kwenye headlines na hii baada ya zile headlines za kutoa msaada wa maafa hayo kwa kutoa pound milioni 7, amemtumia Jetin Shrestha jezi ya Real Madrid aliyoisaini yenye namba saba na jina lake, Ronaldo amefanya hivyo ikiwa ni miezi michache imepita toka atoe pound milioni 7 kwa wahanga wa tetemeko hilo.
“Nampenda Cristiano Ronaldo naipenda Real Madrid siku moja ningependa kucheza Real Madrid kwa sababu napenda mpira”>>> Jetin Shrestha
Cristiano-Ronaldo-sends-shirt (3)
Cristiano-Ronaldo-sends-shirt (2)
Cristiano-Ronaldo-sends-shirt (1)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli ambaye huwa ni kawaida kuwa katika headlines mbalimbali kutokana na tabia yake na matukio yake ambayo anafanya, August 27 kaongea sababu zilizomfanya asifanye vizuri akiwa Liverpool.
Mario BalotelliBalotelli alikuwa na maisha magumu Liverpool kwani msimu uliomalizika aliishia kucheza mechi 16 na kufunga goli moja pekee. Balotelli analaumi mbinu za kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ndio zimemfanya ashindwe kufanya vizuri msimu uliopita.
“Lazima nikubali makosa yangu, mfumo uliyokuwa umechaguliwa na Rodgers haukuendana na mimi, wakati naanza nilikosa nafasi kadhaa za wazi, nilikuwa na nafasi chache za kufunga kwa bahati mbaya ukichanganya na majeruhi, sikulalamika niliheshimu maamuzi ya mwalimu na nilijiheshimu kama mchezaji professional”>>> Balotelli
Liverpool v West Bromwich Albion - Barclays Premier League...Football - Liverpool v West Bromwich Albion - Barclays Premier League - Anfield - 4/10/14 Liverpool's Mario Balotelli looks dejected Mandatory Credit: Action Images / Carl Recine Livepic EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or "live" services. Online in-match use limited to 45 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications. Please contact your account representative for further details.
“Tabia zangu sio tu kwa sababu nimekuja Milan hata wakati nipo Liverpool mfumo wa maisha yangu na tabia zangu zilikuwa kawaida, kwa mfano mwaka uliopita sikuwa na tatizo lolote katika maisha yangu binafsi zaidi ya kupiga picha nikiwa kwenye migahawa na kuweka Instagram lakini hiyo haikuwa na maana kuwa sikuwa nikifanya mazoezi lakini sikucheza”>>> Balotelli
Liverpool's Mario Balotelli (right) speaks with Liverpool's Daniel Sturridge and Liverpool's Jordan Henderson (centre) before taking the penalty during the UEFA Europa League match at Anfield, Liverpool. PRESS ASSOCIATION Photo. Picture date: Thursday February 19, 2015. See PA story SOCCER Liverpool. Photo credit should read: Martin Rickett/PA Wire.
“Nimeambiwa nibadilike nifuate mfumo wa Milan nitafanya hivyo bila tatizo lolote, nimekuwa na staili hii ya nywele kwa muda mrefu ila sitaendelea nayo tena, matatizo yangu hayakuwa ubora wangu ila tabia nimekuwa nikiambiwa maneno mengi sana”>>> Balotelli
Mario Balotelli amerudi AC Milan ya Italia ikiwa ni baada ya kuondoka msimu uliopita na kujiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 16 amerudi AC Milan akitokea Liverpool kwa mkopo wa muda mrefu.
Klabu ya Manchester United bado inasaka nyota kadhaa watakaojiunga na kikosi chao ili kuweza kuongeza nguvu na kucheza kwa kiwango cha juu. Man United ambayo kwa hivi karibuni ilimkosa Pedro Rodriguez baada ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kumpigia simu na kumshawishi ajiungea na Chelsea.
640x-1Sasa Man United wamerudi tena katika klabu ya FC Barcelona ila safari hii wanahitaji kumsajili nyota ambaye wengi wanaamini hawezi kuuzwa kipindi hiki. Inaripotiwa na vyombo vingi vya habari Uingereza kuwa  Man United wanataka kumsajili Neymar na wametenga kiasi cha pound milioni 240 ili kumpata nyota huyo.
 Stori zilizopo kwa sasa FC Barcelona wanajiandaa kumpatia Neymar mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya pound milioni 182, Mkataba ambao utamuweka Neymar Nou Camp hadi mwaka 2023. Mkataba wa Neymar wa sasa utamalizika mwaka 2018.

HAPA ALIAMUA KUJIFUA NA TIMU YA RUGBY ILI KUJIWEKA FITI ZAIDI.

Mtanzania Emily Mgeta sasa anajiandaa kuendelea kupasua anga katika soka la Ujerumani akiwa na kikosi chake cha Neckarsulmer.


Neckarsulmer inashiriki daraja la tano na Mgeta anaonekana taratibu kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza na wikiendi hii wanatarajia kucheza dhidi ya Schwäbisch Hall.

“Kweli tutacheza na Schwabisch Hall, mechi itakuwa ngumu kwa kuwa jamaa ni wazuri lakini tumepania kuendelea kufanya vema.

“Mazingira ya kazi hapa ni mazuri lakini yanataka umakini na kujituma sana kaka. Naendelea kujitahidi  nifanye vizuri zaidi,” alisema.
Mgeta aliwahi kuichezea Simba pia Polisi Moro kabla ya kuondoka Tanzania na kujiunga na Neckarsulmer 
.

Mgeta amesema anaamini kufanya vema kutamsaidia kusonga mbele kimataifa, hivyo hatachoka.


 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM, uliofanyika leo katika stendi ya daladala maarufu kwa jina la Samunge, jijini Arusha leo
 Sehemu ya umati wa wananchi waliofurika kwenye mkutano huo jijini Arusha leo
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Ummy Mwalimu akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
 Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha



image4
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show, linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa THT, Msami.

Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.

"Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.

Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia 'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa jina la Sanaa.".

Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.

Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.
Abdul AmadHusna Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!
Jonetha Peter
Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Mshindi wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai wakiwa na bango linalomwelezea mahindi huyo wakati walipojitokeza kumpokea wakati akirejea nyumbani kwao Mambogini Moshi.
 Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai akiwasalimia wakazi wa mji wa Moshi waliokuwa wakimpongeza wakati akirejea kwao Mambo
 Wakiendelea kumpongeza
 Wakitoa Mkono wa pongezi kwa mshindi wakati akipita kuelekea nyumbani kwao
 Akipongezwa na wadau wake
 Kwa hisia huku akifurahi
 Alipokelewa hivi na vijana wenzie
 Kila Kona walijitokeza wadau kumpongeza
 Ndugu, Jamaa na marafiki wakimpokea mshindi wao na kumpongeza kwa kuibuka mshindi na kuiwakilisha kanda ya kaskazini vyema.

waliotembelea blog