Friday, September 5, 2014



Neymar kulia akishangilia bao lake la ushindi dhidi ya  Colombia leo hii Ijumaa walipoichabanga bao 1-0

Neymarakikimbiza na  Juan Zuniga huko Miami

Radamel Falcao kwenye patashika akikabwa
Wakicheza hii Leo huko Sun Life Stadium, Miami ikiwa ni Mechi yao ya kwanza chini ya Kocha Dunga na pia hii ikiwa ni Mechi ya kwanza kwa Neymar kuichezea Brazil tangu avunjwe Mfupa wa Mgongoni na Juan Zuniga wa Colombia kwenye Mechi ya Robo ya Kombe la Dunia Mwezi Julai, Brazil wameifunga Colombia Bao 1-0.
Hadi Mapumziko, Bao zilikuwa 0-0.
Dakika ya 51 Colombia walibaki Mtu 10 baada ya Cuadrado kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu alipopata Kadi ya Njano ya Pili baada kumchezea Rafu Neymar.
Kwenye Kipindi hicho cha pili, Brazil ilimuingiza Mkongwe wao Robinho ambae hajaichezea Nchi hiyo Siku nyingi na Colombia wakamwingiza Straika wao, Falcao, ambae ni Mchezaji mpya wa Manchester United na ambae hakucheza huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuumia Goti.Neymar kwenye patashika dhidi ya wachezaji wa Colombia  Aldo Leao Ramirez

Neymar akifanya yake ndani ya Uwanja wa  Miami Sun Light

Jina mpya wa Aston Villa Carlos Sanchez akichuana na Diego Tardelli

Frikiki murua ya Dakika ya 82 iliyopigwa na Neymar ndio iliwapa Brazil Bao lao moja na la ushindi.
Brazil watacheza Mechi nyingine ya Kirafiki huko Marekani hapo Jumatano dhidi ya Ecuador.

MECHI ZA KIMATAIFA ZA IRAFIKI
RATIBA/MATOKEO:

Ijumaa Septemba 5
Japan 0 vs Uruguay 2
Jumamosi Septemba 6
Brazil 1 Colombia 0
Jumapili Septemba 7
05:00 Chile v Mexico
2145 Serbia v France
Jumatatu Septemba 8
14:00 South Korea v Uruguay
23:00 Saudi Arabia v Australia
Jumatano Septemba 10
03:00 Chile v Haiti
05:00 Brazil v Ecuador
05:00 Mexico v Bolivia



Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Priomotions ambao ndio waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana kuahirisha onyesho hilo mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.

Kuaihirishwa huko kunafuatia ajali mbaya na ya aina yake iliyopelekea simanzi na majonzi makubwa wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.Waandaji wa tamasha hilo pamoja na Wasanii pia walipeleka vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo,Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu sambamba na Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii Shilole sambamba na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba wakikabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Samsoni Winani.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani akifafanua jambo kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika kijiji cha SabaSaba,nje kidogo ya mji wa Musoma mchana huu.Ambapo DK Samsoni alisema kuwa ajali hiyo ni aina yake na haijawahi tokea tangu ajali ya aina hiyo ilivyotokea mnamo mwaka 1996.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akimpa pole Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika katika kijiji cha eneo la SabaSaba,nje kidogo ya mji wa Musoma mchana huu.


KOCHA wa Brazil Dunga amemteua Neymar kuwa Kepteni wa Brazil ambayo baadae Usiku huu itapambana na Colombia huko Marekani na hii ni Mechi ya kwanza kwa Neymar kuichezea Brazil tangu avunjwe Mfupa wa Mgongoni na Juan Zuniga wa Colombia.
Neymar, mwenye Miaka 22, alianza vyema na Nchi yake Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizochezwa Nchini humo Mwezi Juni na Julai lakini kwenye Mechi ya Robo Fainali Fowadi huyo wa Barcelona aliumizwa vibaya Mgongoni na Mchezaji wa Colombia Juan Zuniga na kumfanya ashindwe kuendelea kucheza Kombe la Dunia.

Expectation: Neymar has been viewed as a Brazilian saviour and he will have to carry the weight of a nationKwenye Mechi iliyofuatia ya Nusu Fainali, Brazil, bila ya Neymar, ilibandikwa Bao 7-1 na Germany ambao walitinga Fainali na kutwaa Kombe la Dunia kwa kuifunga Argentina 1-0.
Neymar amepewa utepe wa kuiongoza Brazil ndani ya Sun Life Stadium huko Miami baada kuumia Nahodha Thiago Silva alieteuliwa na Kocha aliepita Luiz Felipe Scolari.
Akizungumzia uteuzi wa Neymar, Dunga amesema walishaamua na kuongea nae mapema kumwandaa kwa hili.
Dunga ametamka: “Ni Mchezaji mwenye kipaji na licha ya umri wake anao uzoefu. Kepteni anatakiwa kuweka viwango kwa wenzake.”
Mwenyewe Dunga amewahi kuwa Nahodha wa Brazil iliyotwaa Kombe la Dunia Mwaka 1994.


MECHI ZA KIMATAIFA ZA IRAFIKI
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Septemba 5

13:45 Japan v Uruguay
Jumamosi Septemba 6
04:00 Brazil v Colombia
Jumapili Septemba 7
05:00 Chile v Mexico
21:45 Serbia v France
Jumatatu Septemba 8
14:00 South Korea v Uruguay
23:00 Saudi Arabia v Australia
Jumatano Septemba 10
03:00 Chile v Haiti
05:00 Brazil v Ecuador
05:00 Mexico v Bolivia


Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kutocheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.

Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.



Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao huku wakiongozwa na Mary Lucos (kushoto) katika show zao za kila Ijumaa kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar bila kusahau leo pia watakuwepo kuanzia saa tatu usiku.

Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi hiyo.

Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akifanya yake jukwaani huku kushoto na kulia akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos


Pichani juu na chini ni washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 litakalofanyika Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro wakitambulishwa mbele ya mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 wakijimwaga uwanjani na burudani ya Skylight Band ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
Pichani juu ni walimbwende wa shindano la Miss Ilala 2014 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Skylight Band ambapo Jumamosi hii atapatikana mshindi wa taji hilo ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro jijini Dar.

Wanamanyoya wakiwakilisha vilivyo kwa ukodak.


Rant: England boss Roy Hodgson has hit back at critics of his side following their win against Norway
Katukana: Bosi wa England, Roy Hodgson amejibu mapigo kutokana na kitendo cha kukosolewa baada ya kuonesha kiwango cha chini dhidi ya Norway

ROY Hodgson  amegeuka 'mbogo' baada ya kukosolewa kwa kitendo cha England kuonesha kiwango 'mbofumbofu' katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway katika dimba la Wembley.
Kocha huyo aliulizwa kutoa maoni yake kutokana na timu yake kupiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango katika mechi hiyo, na ndipo alipowaka mno akisema; "Sitaweza kuzungumzia hilo kwasababu kuna mtu ataniambia, "sawa, ulikuwa na mashuti mawili tu yaliyolenga lango" mie naona ni  f****** b*******, samahani." (hatujaona haja ya kutafsiri maneno hayo kwasababu za kimaadili).
Hodgson alionesha kisikitishwa na kiwango cha England katika uwanja wa Wembley na alikiri kuwa itawachukua miaka mingi kurudi katika kiwango cha zamani cha 'Simba watatu' wa ukweli.
Relief: Wayne Rooney's penalty earned England a slender win at Wembley
Mwokozi: Penalti aliyofunga Wayne Rooney iliwaokoa England wakiwa uwanja wa nyumbani wa Wembley
Spot on: Rooney's below-par display didn;t stop his burying the penalty kick
Kitu kambani: Rooney akimimina mpira nyavuni kwa mkwaju wa penalti.

Moyo wa Hodgson upo katika maandalizi ya mechi ya jumatatu ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Uswizi mjini Basle.
Hodgson amekuwa katika presha kubwa kutokana na mashabiki kukikosoa kikosi chake kwa kufanya vibaya katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil ambapo waliambulia pointi moja tu katika michezo mitatu ya makundi.
Mashabiki 40,181 walihudhuria mechi ya jumatano-na hii ndio idadi ndogo zaidi kuwahi kutokea katika uwanja huo mpya tangu ulipozinduliwa mwaka 2007.


Zlatan Ibrahimovic alifunga bao lake la 50 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Estonia

MSHAMBULIAJI wa PSG, Zlatan Ibrahimovic ameweka rekodi ya kuwa mfalme wa ufungaji wa mabao wa wakati wote wa Sweden.
Nyota huyo mwenye miaka 32 alifunga bao safi katika mechi ya kirafiki baina ya Sweden na Estonia na kufikisha mabao 50, akivunja rekodi ya Sven Rydell ambaye kwa mara ya mwisho alifunga mabao 49 dhidi ya Finland mwaka 1932.
Baada ya kuvunja rekodi, Ibrahimovic alivua jezi yake kutoa ujumbe kwa mashabiki. Ilisomeka: 'Ni gjorde det mojligt,' au: 'You made it all possible.' kwa tafsiri isiyo rasmi; "mumefanikisha hili kuwezekana".


Sasa amevunja rekodi ya Rydel aliyeifungia Sweden mabao 49 katika mechi za kimataifa. WAFUNGAJI 10 BORA WA SWEDEN
1. Zlatan Ibrahimovic - Magoli 50 katika mechi 99
2. Sven Rydell - Magoli 49 katika mechi 43
3. Gunnar Nordhal -Magoli 43 katika mechi 33
4. Henrik Larsson - Magoli 37 katika mechi 106
5. Gunnar Gren - Magoli 32 mechi 57
6. Kennet Andersson - Magoli 31 mechi 83
7. Marcus Allback - Magoli 30 mech 74
8. Martin Dahlin - Magoli 29 mechi 60
9. Tomas Brolin - Magoli 27 mechi 47
10. Agne Simonssen - Magoli 27 katika mechi 51


Baada ya kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa mwaka 2001, Ibrahimovic alifunga bao la kwanza katika mechi yake ya kwanza ambayo walishinda mabao 3-0 dhidi ya Azerbaijan katika fainali za kombe la dunia.
Katika michuano ya Ulaya mwaka 2004, wakati huo akiwa Ajax, mshambuliaji huyo alifunga bao la mashindano.
Juhudi zake pia zilimfanya afunge bao dhidi ya Italia na kuongeza ukali wake na hatimaye kusajiliwa na Juventus.
Lakini bao lake kali la kimataifa linalokumbukwa sana alifunga mwaka 2012.
Akiwa tayari ameshafunga mabao matatu dhidi ya England,Ibrahimovic alifunga bao kali akiwa umbali wa mita 35 kwa tiki taka matata na kumuacha Joe Hart akizubaa langoni na alishinda tuzo ya FIFA ya 2013 ya bao bora la mwaka.


Zlatan Ibrahimovic alifunga bao matata dhidi ya Italia na kusajiliwa na Juventus
Baada ya Joe Hart kutoka langoni kuokoa mpira, Zlatan alipiga mpira kwa tikitaka na kufunga goli safi mno

Ibrahimovic alishinda zawadi ya FIFA ya goli bora baada ya kufunga kwa tiki-taka matata dhidi ya England mwaka 2012

 


Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao huku wakiongozwa na Mary Lucos (kushoto) katika show zao za kila Ijumaa kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar bila kusahau leo pia watakuwepo kuanzia saa tatu usiku.

Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi hiyo.

Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akifanya yake jukwaani huku kushoto na kulia akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos


Pichani juu na chini ni washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 litakalofanyika Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro wakitambulishwa mbele ya mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 wakijimwaga uwanjani na burudani ya Skylight Band ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
Pichani juu ni walimbwende wa shindano la Miss Ilala 2014 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Skylight Band ambapo Jumamosi hii atapatikana mshindi wa taji hilo ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro jijini Dar.

Wanamanyoya wakiwakilisha vilivyo kwa ukodak.



MCHEZAJI MPYA wa Manchester United Marcos Rojo sasa amepatiwa Viza ya kufanya kazi Nchini Uingereza na hivyo yuko huru kuichezea Klabu yake hapo Septemba 14 itakapoivaa QPR Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Nyota huyo wa Argentina mwenye Miaka 24 alijiunga na Man United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno Siku 16 zilizopita lakini alikwama kuichezea.
Iliripotiwa kuchelewa kupewa Viza hiyo ya Kazi kunatokana na kukabiliwa na Kesi huko Nchini kwao Argentina ya kugombana na Jirani yake Mwaka 2010.
Awali ilidhaniwa kuwa Rojo amekwama kucheza kutokana na Umiliki wa Haki za Biashara za Mchezaji huyo kuwa chini ya pande mbili lakini FA, Chama cha Soka England, kilitoboa kuwa Mchezaji huyo ashapewa Hati ya Kimataifa ya Uhamisho na wao kumruhusu kuichezea Man United.

Lakini hii Leo, Man United imetoboa Mchezaji huyo sasa hana kikwazo chochote kucheza Soka lake.


MCHAMBUZI na Mtaalam wa Soka la Spain, Paul Breen-Turner, anaamini Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anajisafishia njia ya kurudi Klabu yake ya zamani Manchester United.
Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, aliihama Man United Mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid lakini Siku zote amekataa kukanusha kwamba hatarudi Old Trafford ambako ndiko Ustaa wake ulichipukia.

Breen-Turner amedai hivi sasa Ronaldo amekerwa na Sera ya kuuza Wachezaji ya Real ambako hivi karibuni walimuuza Angel Di Maria huko Man United kwa Dau la Rekodi ya Uingereza na pia Xabi Alonso kwenda Bayern Munich.
Mchambuzi huyo amesema: “Hivi karibuni alihojiwa na Wanahabari na kutamka: ‘Ningekuwa nashughulikia Uhamisho, nisingefanya vitu namna hii kama walivyofanya!’ Na kauli hii imemuudhi Rais wa Real Florentino Perez!” Mwaka Jana Ronaldo alikerwa na kuuzwa kwa Mesut Ozil kwa Arsenal na Breen-Turner ameeleza Ronaldo alimfuata Perez na kumueleza kuhusu kutofurahishwa kwake na safari hii pia Ronaldo alikwenda kumuona Rais huyo baada ya kuuzwa Di Maria.
Breen-Turner amedai, safari hii, Ronaldo alifuatana na Sergio Ramos kumwona Perez na kutaka Di Maria asiuzwe lakini hawakusikilizwa na hilo limemuudhi sana Ronaldo.
Breen-Turner ameeleza: “Hivi sasa Ronaldo hana furaha. Kitu kingine ni ule msimamo wake wa kila Siku kuisifia Man United na hivi Juzi kusifia sana kwa United kumsaini Falcao na kudai huo ni usajili kabambe. Kila kitu anachosema, kila kitu anachofanya ni kusafisha njia ya kurudi Man United!”


Sir Alex Ferguson akizungumza na Carlo Ancelotti na Arsene Wenger katika mkutano wa makocha mjini Nyon MKUTANO wa mwaka wa makocha wa kiwango cha juu umeanza jana jumatano na kumalizika leo, makao makuu ya UEFA, mjini Nyon, Uswizi.
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo akiwa kama balozi wa makocha wa UEFA , wakati naye Rais Michele Platini alikuwepo. Ferguson alinaswa na kamera akitaniana na aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Arsene Wenger, wakati bosi wa Manchester City, Manuel Pellegrini naye alikuwepo katika tukio hilo. Wakizungumzia mchezo mzuri: Rais wa UEFA Michele Platini akizungumza na Ancelotti na Ferguson leo alhamisi. Picha ya pamoja ya makocha katika makao makuu ya UEFA leo nchini Uswizi. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akiwa amekaa na kocha wa zamani wa Stamford Bridge, Carlo Ancelotti
Mourinho akizungumza na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya UEFA leo.

Hata hivyo, kocha wa mashetani wekundu, Manchester United, Louis van Gaal - ambaye ni mshindi wa Bundesliga, La Liga na Eredivisie - hakuwepo katika mkutano huo kwasababu timu yake haishiriki michuano ya UEFA mwaka huu.

Louis van Gaal hakuhudhuria mkutano huo.

MAKOCHA WALIOHUDHURIA MKUTANO WA MAKOCHA MWAKA 2014 MAKAO MAKUU YA UEFA NI:-

Michele Platini - UEFA President
Sir Alex Ferguson
Gianni Infantino - UEFA General Secretary
Ioan Lupescu - UEFA Chief Technical Officer
Giorgio Marchetti - UEFA Competition Director
Pierluigi Collina - UEFA Chief Refereeing Officer
Laurent Blanc - PSG manager
Manuel Pellegrini - Man City manager
Nuno Espirito Santo - Valencia manager
Jens Keller - Schalke manager
Mircea Lucescu - Shakhtar Donetsk manager
Jorge Jesus - Benfica manager
Unai Emery - Valencia manager
Jurgen Klopp - Borussia Dortmund manager
Roger Schmidt - Bayer Leverkusen manager
Andre Villas-Boas - Zenit St Petersburg manager
Miguel - Olympiakos manager
Rafael Benitez - Napoli manager
Carlo Ancelotti - Real Madrid manager
Pep Guardiola - Bayern Munich manager
Luis Enrique - Barcelona manager
Arsene Wenger - Arsenal manager

waliotembelea blog