Friday, September 5, 2014



MCHEZAJI MPYA wa Manchester United Marcos Rojo sasa amepatiwa Viza ya kufanya kazi Nchini Uingereza na hivyo yuko huru kuichezea Klabu yake hapo Septemba 14 itakapoivaa QPR Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Nyota huyo wa Argentina mwenye Miaka 24 alijiunga na Man United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno Siku 16 zilizopita lakini alikwama kuichezea.
Iliripotiwa kuchelewa kupewa Viza hiyo ya Kazi kunatokana na kukabiliwa na Kesi huko Nchini kwao Argentina ya kugombana na Jirani yake Mwaka 2010.
Awali ilidhaniwa kuwa Rojo amekwama kucheza kutokana na Umiliki wa Haki za Biashara za Mchezaji huyo kuwa chini ya pande mbili lakini FA, Chama cha Soka England, kilitoboa kuwa Mchezaji huyo ashapewa Hati ya Kimataifa ya Uhamisho na wao kumruhusu kuichezea Man United.

Lakini hii Leo, Man United imetoboa Mchezaji huyo sasa hana kikwazo chochote kucheza Soka lake.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog