Friday, September 5, 2014


KOCHA wa Brazil Dunga amemteua Neymar kuwa Kepteni wa Brazil ambayo baadae Usiku huu itapambana na Colombia huko Marekani na hii ni Mechi ya kwanza kwa Neymar kuichezea Brazil tangu avunjwe Mfupa wa Mgongoni na Juan Zuniga wa Colombia.
Neymar, mwenye Miaka 22, alianza vyema na Nchi yake Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizochezwa Nchini humo Mwezi Juni na Julai lakini kwenye Mechi ya Robo Fainali Fowadi huyo wa Barcelona aliumizwa vibaya Mgongoni na Mchezaji wa Colombia Juan Zuniga na kumfanya ashindwe kuendelea kucheza Kombe la Dunia.

Expectation: Neymar has been viewed as a Brazilian saviour and he will have to carry the weight of a nationKwenye Mechi iliyofuatia ya Nusu Fainali, Brazil, bila ya Neymar, ilibandikwa Bao 7-1 na Germany ambao walitinga Fainali na kutwaa Kombe la Dunia kwa kuifunga Argentina 1-0.
Neymar amepewa utepe wa kuiongoza Brazil ndani ya Sun Life Stadium huko Miami baada kuumia Nahodha Thiago Silva alieteuliwa na Kocha aliepita Luiz Felipe Scolari.
Akizungumzia uteuzi wa Neymar, Dunga amesema walishaamua na kuongea nae mapema kumwandaa kwa hili.
Dunga ametamka: “Ni Mchezaji mwenye kipaji na licha ya umri wake anao uzoefu. Kepteni anatakiwa kuweka viwango kwa wenzake.”
Mwenyewe Dunga amewahi kuwa Nahodha wa Brazil iliyotwaa Kombe la Dunia Mwaka 1994.


MECHI ZA KIMATAIFA ZA IRAFIKI
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Septemba 5

13:45 Japan v Uruguay
Jumamosi Septemba 6
04:00 Brazil v Colombia
Jumapili Septemba 7
05:00 Chile v Mexico
21:45 Serbia v France
Jumatatu Septemba 8
14:00 South Korea v Uruguay
23:00 Saudi Arabia v Australia
Jumatano Septemba 10
03:00 Chile v Haiti
05:00 Brazil v Ecuador
05:00 Mexico v Bolivia

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog