Katukana: Bosi wa England, Roy Hodgson
amejibu mapigo kutokana na kitendo cha kukosolewa baada ya kuonesha
kiwango cha chini dhidi ya Norway
ROY Hodgson amegeuka 'mbogo' baada ya
kukosolewa kwa kitendo cha England kuonesha kiwango 'mbofumbofu' katika
ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway katika dimba la Wembley.
Kocha huyo aliulizwa kutoa maoni yake
kutokana na timu yake kupiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango katika
mechi hiyo, na ndipo alipowaka mno akisema; "Sitaweza kuzungumzia hilo
kwasababu kuna mtu ataniambia, "sawa, ulikuwa na mashuti mawili tu
yaliyolenga lango" mie naona ni f****** b*******, samahani." (hatujaona haja ya kutafsiri maneno hayo kwasababu za kimaadili).
Hodgson alionesha kisikitishwa na
kiwango cha England katika uwanja wa Wembley na alikiri kuwa itawachukua
miaka mingi kurudi katika kiwango cha zamani cha 'Simba watatu' wa
ukweli.
Mwokozi: Penalti aliyofunga Wayne Rooney iliwaokoa England wakiwa uwanja wa nyumbani wa Wembley
Kitu kambani: Rooney akimimina mpira nyavuni kwa mkwaju wa penalti.
Moyo wa Hodgson upo katika maandalizi ya mechi ya jumatatu ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Uswizi mjini Basle.
Hodgson amekuwa katika presha kubwa
kutokana na mashabiki kukikosoa kikosi chake kwa kufanya vibaya katika
fainali za kombe la dunia nchini Brazil ambapo waliambulia pointi moja
tu katika michezo mitatu ya makundi.
Mashabiki 40,181 walihudhuria mechi ya
jumatano-na hii ndio idadi ndogo zaidi kuwahi kutokea katika uwanja huo
mpya tangu ulipozinduliwa mwaka 2007.
0 maoni:
Post a Comment