Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama
cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama
hicho, aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Iringa mjini, Chiku Abwao baada ya kuhamia rasmi
ACT-Wazalendo Dar es Salaam leo mchana.
Mbunge Chiku Abwao (kulia), akionesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kukabidhiwa.
Mbunge Chiku Abwao (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT-Wazalendo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
MITAZAMO MBALI MBALI JUKWAANI
Tuachane uroho wa madaraka kwa kuwadanga na kuwahadaa wananchi. Leo
tunawaonyesha wezi na kuwafikisha mahabusu halafu kesho tunakula nao na
kuwasifia kwa kazi zao. Wengine wanasema ety ana wafuasi wengi, hivi
tunataka kushika madaraka au tunataka kuwa na serikali bora itakayolinda
na kutetea maslahi ya wananchi???
Lusifa ana wafuasi wengi sana hapa duniani hata kufikia hatua ya
kumjaribu Mungu lakini kamwe Mungu hakuwai kumfikiria kumrejesha Lucifa
kuwa malaika wa sifa kama alivyokuwa awali, Nitakuwa wa mwisho kuunga
mkono usanii na udanganyifu wa kisiasa unaotaka kutokea ndani ya nchi
yangu.
By Mesaya
#HABARI LOWASSA AKARIBISHWA RASMI UKAWA
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema umemkaribisha rasmi Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kujiunga nao katika harakati za
kuking'oa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mbatia: Tunamkaribisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward
Ngoyaye Lowasa kujiunga na UKAWA, ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa
majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale
ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki Tanzania, Mungu
ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.
Mbatia: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Mwanzoni wa mwezi wa
nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga
hatua ambayo ni nzuri
Lipumba: "Lowasa alishasema yeyote mwenye ushahidi aulete..hapa
tumekaribisha Watanzania wote kujiunga. Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama
chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano
mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga
mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF
basi ndio unazungumza na CUF.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ