Wednesday, June 4, 2014


Rais Roussef ametetea vikali maandalizi ya kombe la dunia Brazil
Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea jinsi ambavyo taifa lake limetayarisha Kombe la Dunia litakaloanza juma lijalo jijini Sao Paulo.
Alisema kuwa michezo hiyo itakuwa yenye ufanisi mkubwa ijapokuwa kumekuwepo na kukosolewa kwa kuchelewa kwa nyanja na miundombinu mbalimbali.
Aliwaambia wanahabari kuwa matatizo ya aina ile ni ya kawaida kila mahali.
Bi Rousseff ambaye huenda akakumbwa na maandamano mapya ya kupinga serikali, alisema kuwa hawataruhusiwa kuvuruga mashindano hayo.
'Gharama ya demokrasia'
Maandamano ya kupinga gharama ya kuandaa michuano ya kombe la dunia Brazil

''Kila mahali duniani, miradi mikubwa ya uhandisi mara kwa mara hutatizika,” bi Rousseff aliwaambia wanahabari kutoka katika mataifa ya kigeni katika makazi ya rais jijini Brasilia.
Alisema kuwa hakuna anayeweza kutengeneza reli za chini ya ardhi isipokuwa labda Uchina.
Hayo aliyasema kuhusu kuchelewa kwa miradi ya miundombinu, jambo ambalo limewakera wananchi wengi wa Brazil waliotarajia kunufaika kutokana na kuboreswa kwa miundombinu hiyo.
Mifumo ya usafiri katika miji ya Cuiaba, Salvador, Recife na miji mingine mingi haijakamilishwa kwa kuwa juhudi zote zilielekezwa katika kukamilika kwa nyanja za kandanda zitakazotumika katika mashindano hayo.
Rais huyo alitaja kuchelewa huko kama ''gharama ya demokrasia yetu.''
Akizungumzia maandamano ya kupinga Kombe la Dunia la hivi majuzi- ambayo baadhi yaligeuka kuwa vurugu- rais alisema kuwa ingawa maandamano yaliambatana na demokrasia, maelfu ya polisi na askari zaidi watatumiwa kuhakikisha kuwa haitavuruga Kombe la Dunia.
''Tunawahakikishia watu wote usalama,” alisema.
'Uangalifu wa karibu'
Uwanja wa Sao Paulo

Zaidi ya watu milioni moja waliingia mitaani wakati wa michezo ya Confederation kuandamana kupinga ufisadi na kile wanachodhani ni matumizi ya kupindukia katika kutayarisha Kombe la Dunia.
Maandamano hayo ambayo mwanzo yalianza kama makusanyiko madogo ya watu waliopinga kuongezeka kwa naulikatika usafiri wa umma ulianza kuwa baada ya polisi kutumia mbinu nzito kuwatawanya waandamanaji.
Bi Rousseff alisema kuwa vikosi vya usalama vitafanya kazi kwa uangalifu wakati huu.
Kikundi kidogo chenye waandamanaji wanaopinga serikali kililenga mechi ya kirafiki iliyokuwa ikichezwa baina ya Brazil na Panama katikati ya jiji la Goianiasiku ya Jumanne.
Waandamanaji hao waliokusanyika karibu na uwanja walikemea gharama kubwa ya michezo hiyo huku wakisema kuwa pesa nyingi ingetumiwa kugharamia huduma za umma ili kupunguza kukosekana kwa usawa.
Michezo hiyo itaanza tarehe 12 mwezi Juni huku wenyeji Brazil wakichuana na Croatia jijini Sao Paulo.



GROUP A
BRAZIL
CROATIA
MEXICO
CAMEROON

GROUP B
SPAIN
HOLLAND
CHILE
AUSTRALIA

GROUP C
COLOMBIA
IVORY COAST
GREECE
JAPAN

GROUP D
URUGUAY
COSTA RICA
ENGLAND
ITALY
World Cup trophy on display in Brazil

GROUP E
SWITZERLAND
ECUADOR
FRANCE
HONDURAS

GROUP F
ARGENTINA
BOSNIA-HERZEGOVINA
IRAN
NIGERIA

GROUP G
GERMANY
PORTUGAL
GHANA
USA

GROUP H
BELGIUM
ALGERIA
RUSSIA
SOUTH KOREA
Here she comes: Fernanda Lima takes to the stage
On stage: Sepp Blatter, addressing the audience, is flanked by Fernanda Lima
Here she comes: Brazilian actress Fernanda Lima takes to the stage as Sepp Blatter addresses the audience


Wachungaji wakiongoza ibada ya kumuaga marehemu Mweisigwa Blandesi aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Oakland, California iliyofanyika siku ya Jumamosi May 31, 2014 Oakland, California..
 Balozi wa Heshima Bwn. Ahmed Issa akiongea machache jinsi gani alivyokuwa anamfahamu marehemu kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao Mwesigwa Balnde  iliyofanyika siku ya Jumamosi May 31, 2014 Oakland, California..
 Mmoja ya watu mbalimbali waliohudhuria ibada ya kumuaga mpndwa wao Mwesigwa Blandesi akiongea machache kwenye ibada ya kumuaga marehemu  iliyofanyika siku ya Jumamosi May 31, 2014 Oakland, California..
 Watanzania wa California na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao Mwesigwa Balandesi iliyofanyika siku ya Jumamosi May 31, 2014 Oakland, California..
Mamia ya Watanzania waishio California, marafiki, Viongozi mbalimbali kutoka Jumuiya nyingine za Kitanzania na nchi za Kiafrika hapa Marekani pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wajitokeza kumuaga mpendwa wao na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio "Bay area" na vitongoji vyake (TCO) marehemu Mwesigwa Blandesi.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi


Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na viongozi wa Jumiya za Kitanzania zilizopo Toronto, Canada siku ya Ijumaa May 30, 2014. Rais Dkt Jakaya Kikwete alikuwa Canada wiki iliyopita kuhudhuria kikao cha “Improving the Lives of Women and Children: Maternal, Newborn and Child Health “ Viongozi wa ZANCANA walipata fulsa ya kumweleza Mheshimiwa Rais Jumuiya yao inavyojitahidi kusaidia nyumbani Tanzania katika sekta mbalimbali hususan ikijikita kwenye elimu na mahospatalini kwa kupeleka misaada mbalimbali mashuleni na kwenye Wizara ya Afya na ustawi wa jamii.
Viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Watanzania Toronto, Canada wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa akiongea nao siku ya Ijumaa May 30, 2014.,
Makamu wa Rais wa ZANCANA Jamal Jiddawy katika picha yaa pamoja na Rais Dkt. Jakaya Kikwete
Executive Manger Bishara na Boardmember Zamil ZANCANA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Dkt Jakaya Kikwete


Smithsonian’s National Museum of African Art picha katika  maadhimisho ya kutimiaza miaka 50 tangu kufungiliwa kwa Museum hiyo iliopo Mjini Washington, DC

National Museum of African Art siku ya Jumanne June 3, 2014 wamesherehekea maadhimisho ya kutimiaza miaka 50 tangu kufungiliwa kwa Smithsonian’s National Museum of African Art, Mjini Washington, DC
Sharehe hizo zilianza rasmi mida ya Saa Nne Asubuhi na kumalizika saa Kumi na Moja Jioni kukiwa na ngoma za kitamaduni zilizotumbuizwa na kundi zima la  Farafina Kan, pamoja na  Ethiopian Coffee Ceremony, Henna Paint pamoja na chakula cha  Nando's Peri-Pari
Msimamizi  wa NPR Show  ''Tell me more'' Michel Martin akiendesha mazungumzo dhidi ya wawakilishi. 

Aidha  wawakilishi wa National Museum of African Art, walizungumzia kuhusu historia ya kumbukumbu ya miaka 50 ya kuazishwa juu ya makumbusho hayo. Katika mazungumzo hayo mbayo yalikuwa chini ya  msimamizi  wa NPR Show  ''Tell me more'' Michel Mc , Queen Martin, Dr Johnnetta Betsch Cole (Directoct of National)  Lady  Putrecelli, Dr. Alan Brody (Warren Robbins-Founder of Museum's Nephew) Pesident of the Center for Cross Cultural Communications, Asif Shaik na Bryna Freyer Senior curator at African Art.
Wageni mbalimbali wakisikiliza historia ya  kutimiaza Miaka 50 ya Smithsonian’s National Museum of African Art Kikundi cha Farafina Kan kikitumbuiza goma za kitamaduni katika sherehe za maadhimisho ya kutimiaza miaka 50 yaSmithsonian’s National Museum of African Art

SA_8fb8b.jpg
Je unafahamu kuwa...
Waamuzi 25 wa FIFA watachezesha mechi za Kombe la Dunia. Waamuzi hao wanatoka katika mabara yote sita, na wote watachezesha angalau mechi isiyopungua moja. Waamuzi hao na wasaidizi wao watakuwa wakifuatiliwa kwa karibu na kupewa kila msaada wanaohitaji na FIFA ili waweze kuchezesha kwa haki.
Afrika kupitia CAF inawakilishwa na Noumandiez Doué (Ivory Coast), Bakary Gassama (Gambia) na Djamel Haimoudi (Algeria). Mwamuzi aliyechezesha fainali ya mwaka 2010 Howard Webb kutoka England ni miongoni mwa waamuzi walioteuliwa kutoka UEFA.

waliotembelea blog