Friday, June 19, 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.

Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.

Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.

Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.

Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.

Aidha Shirikisho la Mpirani wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa mwongozo kuwa mchezaji Mrisho Halfan Ngasa haruhusiwi kucheza CHAN kwa sababu sio mchezaji tena wa ndani, hivyo Ngasa ameondolewa kikosini

Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.

U15 KUINGIA KAMBINI JUMATATU

Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 15 (U-15) kitaingia kambini siku ya jumatatu tarehe 22/06/2015 ili kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Mbeya, mchezo utakaofanyika mjini Mbeya jumatatu ya tarehe 28/06/2015.

Kikosi hiki kinaandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na na michuano ya mtoano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyia nchini Madagascar mwaka 2017. Hatua ya mtoano wa awali itaanza mwakani 2016 mwezi Juni.

Timu itakua chini ya kocha Bakari Shime kwa muda akisaidiwa na Peter Manyika. Kocha aliyekua ameteuliwa awali kufundisha timu hiyo Adolf Rishard ameomba udhuru baada ya kupata fursa ya kwenda masomoni.

Wachezaji watakaoingia kambini na mikoa wanayotokea kwenye mabano ni Mwijuma Yahya (Tanga), David Mpakazi, Shilole Anthony (Geita),  Kibwana Shomari , Ibrahim Koba, (Morogoro), Faraji John, Kelvin Deogratius, Davison Meddy , Maulid Lembe (Dodoma), Ally Msengi (Mwanza).

Wengine ni Timoth Timothy, Juma Juma, Pius Raphael, Mohamed Ally (Dodoma), Athumani Rajabu, Juma Zubeir, Jonathan Rafael (Kigoma), Robert Philip, Jaffari Juma (Arusha), Michael Kanuti, Alex Peter, Rashid Kilongola (Kinondoni), Morris Michael (Ilala), Karim Mfaume (Lindi), Assad Juma (Unguja Magharibi), Francis Mrope, Kelvin Pius (Mara)

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za wachezaji wa ndani CHAN 2016.

Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.

Endapo Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.

TWFA KUFANYA UCHAGUZI AGOSTI 15
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA), George Mushumba ametangaza uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika agosti 15, 2015 kujaza nafasi mbalimbali.

Kwa mamlaka aliyonayo anapenda kutangaza uchaguzi mkuu wa TWFA leo kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi, uchaguzi huo utafanyika tarehe 15, Agosti 2015 katika nafasi zifuatazo:

index 

  1. Mwenyekiti
  2. Katibu Msaidizi
  3. Mweka Hazina
  4. Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.       
Fomu za kuomba nafasi hizo zitaanza kutolewa tarehe 19-23 Juni 2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba, Jacqueline Ntubaliwe , Vanessa Mdee wameamua kuungana na shiriki la kimataifa liitwalo WildAid ili  kupiga vita ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.
Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Sea Cliff na kuhudhuliwa na waziri wa Maliasili na Utali, Lazaro Nyalandu na wakiwemo mabarozi wa china na marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari Ali Kiba alisema ‘Nashukuru kwanza nilipata nafasi ya kuishi na tembo porini kwa muda wa siku wa tatu kwa hiyo kiukweli lazima uogope maana mimi ni muoga nambari moja,  ila nilichokuwa nafikiria ni tofauti na vile nilivyodhani ila tembo ni wanyama wazuri
.
.
Vile vile nilipata nafasi ya kwendaNairobi kuwatembelea watoto wa tembo yatima mama zao wameuliwa na watu wasio na imani ukifikiri kibinadamu wanyama ni viumbe kama sisi, kuna wale ambao tumeruhusiwa kula lakini sio kwa wale ambao ni fahari kwetu sisi ni vivutio vinaipa nchi yetu thamani, wageni wanakuja kuona hao hao wanyama wetu lakini watu wanawaua kwasababu unavyowatoa ndovu zao ni sawa sawa unawatesa wanaumia kiukweli mimi napiga vita hivi vya ujangili lakini kutokana na imani na kutaka Tembo hao wanapata watetezi ambao ni sisi, mimi na yoyote kwani wale ni kama raia na pia wana haki ya kuishi ndio maana tukiwa na mapenzi nao tunaenda kuwaona, kwa hiyo mimi hili suala nimelipokea kwa mikono miwili na nimefuraha kuwa balozi wa WildAid, nimetembelea sehemu nyingi kama Tarangire na bado nitaendelea kutembelea na wengine mnakaribishwa kutembelea hifadhi za wanyama.
Kwa hiyo na imani mimi na wasanii wengine ambao tunaweza tukatimia nguvu hii ya pamoja, Jacqueline Mengi na Vanessa Mdee kwakweli tuko mbele juu ya suala hili, ningependa sana watanzania tushirikiane katika jambo hilo unapoona tukio hilo limetokea basi toa taarifa mapema kwani ujangili unatuumiza sisi sote…..’alisema.
Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz yuko Afrika Kusini kwa ziara ya kimuziki ambapo mapema wiki hii alisimamia Yamoto Band kwenye video yao ya kwanza kuitengeneza kimataifa kisha tuzo za MTV alikochaguliwa lakini pia amefanya kolabo na staa wa muziki kwenye nchi hiyo aitwae Donald.
Kwenye page yake ya twitter alikua akiRT na kupost picha akiwa kwenye vituo vya Radio za South Afrika akiwa na Donald katika kuipromote hiyo single yao mpya ambapo wakati akiwa anaendelea kupost hizo picha alitokea shabiki mmoja kwenye twitter akamuandikia Ushamba huo hata interview unarusha, kina ngosha washafanya hizo kibao tu, vitu vingine vya kawaida sana wewe‘

waliotembelea blog