Matarajio yalikuwa ni kwamba Steven Gerrard atarejea
Liverpool kwa mkopo Mei, mwakani.
Lakini inaonekana hilo halitakuwepo na kiungo huyo nyota wa
zamani wa Liverpool, mwenye miaka 35 sasa, ataendelea kubaki na klabu yake mpya
ya LA Galaxy.
Kawaida wachezaji wengi wanaokwenda kucheza Marekani
wamekuwa wakirejea England kwa mkopo.
Lakini Kamishna wa Ligi Kuu Marekani (MLS), Don Garber amesema
haoni kama kuna sababu ya Gerrard kurudi Liverpool.
Tena akaongeza kwamba wachezaji kuondoka MLS kumekuwa kukiishusha hadhi akitolea mfano wa David Beckham alivyoondoka LA Galaxy na kwenda AC Mnilan.