Thursday, September 10, 2015



SASA ndiyo imekuwa gumzo, binti wa Hans van der Pluijm na Jose Mourinho, nani mkali?


Makocha wote wawili ni raia wan chi za bara la Ulaya, Ureno na Uholanzi. Wote timu zao ni mabingwa wa nchi.

Jose Mourinho ambaye aliingoza Chelsea kutwaa ubingwa wa England msimu uliopita anaonekana akiwa katika picha akiwa na binti yake walipokwenda kuhudhuria tuzo.

Pluijm, anaonekana pia akiwa na binti yake siku ambayo Yanga ilibeba Ngao ya Hisani kwa kuitwanga Azam FC kwa mikwaju ya penalti.

Wengi wanasifia muonekano wa binti wa Pluijm ambaye mama yake ni Mwafrika raia wa Ghana.
Lakini wako wanaovutiwa zaidi na vazi la binti wa Mourinho.


Hata hivyo ni vigumu kujua nani kashinda kwa kuwa hakuna sehemu ambayo kura zinahesabiwa na picha hizo zimekuwa zikisambaa sehemu mbalimbali.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog