Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la pili hapa.
Samuel Eto'o akifunga bao mpira uliotenguliwa na Michael Carrick na hatimaye kuingia langoni mwa United.
Dakika ya 17 Samwel Eto'o anaipatia bao Chelsea na kufanya 1-0 dhidi ya Man united. Bao la pili Samwel akaiongezea tena bao Chelsea katika dakika za mwishoni za kipindi cha kwanza akifunga katika dakika ya 45. Bao la tatu ni la Eto'o tena..
Sir Alex Ferguson akiteta na shabiki wa United Mick Hucknall wakati wa mtanange Stamford Bridge usiku huu.
Mzee Ferguson akishuhudia bao 2-0 alilo pigwa man u
Mmiliki wa timu ya Chelsea nae alikuwepo uwanjani leo Stamford
Samwel Eto'o akishangilia moja ya bao zake hapa..
Chelsea walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 17, bila kutegemewa kwani Man United ndio waliokuwa juu kimchezo, baada ya uzembe wa kutomkaba Samuel Eto'o ambae alipokea Mpira wa kurushwa na kumhadaa kirahisi Phil Jones kisha kupiga Shuti la Mita 20 na kumbabatiza Mchael Carrick na kumpoteza Kipa De Gea.
Bao la Pili lilifungwa kwenye Dakika ya 45 na Eto’o kufuatia ulinzi duni baada Kona kupigwa na kuokolewa na Mpira kumkuta Ramires aliempasia Cahill aliemsogezea Eto’o na kupachika kilaini.
Bao la 3 lilipigwa tena na Eto’o, ni Hetitriki kwake, kufuatia Kona ya Dakika ya 49 iliyounganishwa na Cahill na kuokolewa na De Gea na kutua miguuni mwa Eto’o ambae alimalizia kilaini kwa mara nyingine.
Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia Bao lao pekee Man United katika Dakika ya 78 kufuatia kazi njema ya Danny Welbeck kumfikia Phil Jones ambae shuti lake lilionekana kutokuwa na madhara hadi alipochomoza Chicharito.
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Nahodha wao Nemanja Vidic kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Eden Hazard.
Samwel Eto'o anakimbiza balaaSamwel anafanya yake
..
!
Moyes ...akicheki mchezoDavid Beckham hakuwa na furaha
Nemanja Vidic nje!!!
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian (Matic 85'), Oscar (Mikel 67'), Hazard, Eto'o (Torres 78'). Subs not used: Cole, Lampard, Mata, Schwarzer.
Booked: Luiz
Goals: Eto'o 17', 45', 49'
Man Utd: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra (Smalling 61'), Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young (Hernandez 56'), Welbeck.
Subs not used: Giggs, Lindegaard, Cleverley, Fletcher, Kagawa.
Booked: Young, Valencia
Sent off: Vidic
Goal: Hernandez 78'