Mara baada ya Jana Arsenal kuibwaga Chelsea na kutwaa Ngao ya Jamii, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amelichochea bifu lake la muda mrefu na mwenzake wa Chelsea Jose Mourinho.Mara baada ya Jana Arsenal kuibwaga Chelsea na kutwaa Ngao ya Jamii, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amelichochea bifu lake la muda mrefu na mwenzake wa Chelsea Jose Mourinho.
Ushindi
wa 1-0 walioupata Jana Arsenal kwa Bao la Dakika ya 24 la Alex
Oxlade-Chamberlain ni ushindi wa kwanza kwa Wenger katika Mechi 14
walizokutana na Chelsea ya Mourinho baada kufungwa Mechi 7 na Sare 6 na
baada ya Mechi hiyo Uwanjani Wembley Jijini London, Wenger alikwepa
kupeana mkono na Mourinho.
Hata hivyo, Mourinho alipeana mkono na kila Mchezaji wa Arsenal aliekuwa akitoka nje ya Uwanja baada ya Mechi hiyo kwisha.
Pia Mourinho aliamua kumrushia Shabiki Kijana wa Arsenal aliekaa Jukwaani Medali aliyopewa kwa kuwa nafasi ya pili katika Mechi hiyo na pia kudai mbele ya Wanahabari kuwa Wenger aliitupa falsafa yake ya kushambulia na kuamua 'kupaki Basi.'John Terry
Lakini Wenger alipinga vikali madai hayo na kudai hatimae wameondoa gundu lao kwa Chelsea.Baadhi ya Wachezaji wa Arsenal wakipata picha na Kombe lao la Ngao ya Jamii