Monday, August 3, 2015


Arsenal Mabingwa 2015  FA Community Shield
Alex Oxlade akipeta baada ya kufunga baoChamberlain akishangilia vikali juu kwa juuMbele ya MashabikiMsimu mpya wa Soka huko England umeanza rasmi hii Leo kwa Mechi maalum ya kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa England Chelsea na waliobeba FA CUP Arsenal Uwanjani Wembley Jijini London na Arsenal kuibuka kidedea kwa kuifunga Chelsea 1-0 ikiwa ni ishara maalum Msimu huu wametangaza nia ya kutwaa Ubingwa.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Arsenal, chini ya Meneja Arsene Wenger, dhidi ya ya Chelsea, chini ya Meneja Jose Mourinho, ambao washakutana uso kwa uso mara 13 na Chelsea kushinda mara 7 na Sare 6.
Alex Oxlade-Chamberlain alifunga Bao pekee na la ushindi kwa Arsenal katika Dakika ya 24 alipopokea pande zuri toka kwa Theo Walcott na hilo ni Bao la kwanza kabisa dhidi ya Chelsea, chini ya Meneja Jose Mourinho, tangu 2007.Alex Oxlade Chamberlain akipongezwaCazorla na ChamberlainKocha wa Timu ya Chelsea Jose Mourinho akijionea Vijana wake WembleyTheo Walcott akigombea mpira wa Kichwa dhidi ya kipa wa ChelseaMonreal nae kwenye patashika mpira wa kichwaChupuchupu langoni mwa Arsenal Petr Cech akiokoa

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog