Tuesday, October 21, 2014


By Aidan Charlie Seif
FC Barcelona leo wanakutana na Ajax fc ya Uholanzi katika mechi ya ligi ya mabingwa wa ulaya – huku wakiwa wanataka kurudisha hali yao ya ushindi baada ya kupoteza mechi yao iliyopita dhidi ya Paris Saint-Germain.

637758
De Boer – Cocu na Enrique wakati walipokuwa wakiicheza FC Barcelona
Mechi hii inawakutanisha watu ambao falsafa za mchezo wa zinafanana – makocha wa timu hizi waliwahi kucheza pamoja katika kikosi cha FC Barcelona takribani miaka 15 iliyopita chini ya Louis Van Gaal.
Mechi za Nyuma
• Klabu hizi zilikutana kwa mara ya kwanza msimu uliopita, Barcelona walishinda 4-0 kwenye dimba la Camp Nou ambapo Lionel Messi alifunga hat trick – Ajax wakarudisha kisasi kwa kushinda 2-1 jijini  Amsterdam.
• Vikosi vilipangwa hivi msimu uliopita:
Barcelona: Valdés, Alves, Mascherano, Piqué (Bartra 80), Adriano, Busquets, Fàbregas (Xavi 71), Iniesta, Sánchez, Messi, Neymar (Pedro 72).
Ajax: Vermeer, Van Rhijn, Denswil, Moisander (Van der Hoorn 73), Blind (Schöne 78), Duarte, Poulsen, De Jong, Bojan, Sigthórsson, Boilesen.
TAKWIMU
Barcelona
• Kipigo cha Barcelona September 30 dhidi ya PSG ndio kilikuwa kipigo chao cha mapema zaidi katika Champions League tangu mwaka 2001.
• Barcelona wamepoteza mchezo mmoja tu wa nyumbani katika mechi 28 zilizopita za UEFA Champions League .
• The Blaugrana hawajahi kupoteza mechi ya nyumbani dhidi ya timu ya Uholanzi. Rekodi yao ipo hivi –  W4 D3 L0.
Ajax
• Baada ya kutoka droo ya 1-1 na APOEL, Ajax sasa wameshindwa kushinda mechi hata moja katika za ugenini Champions League – mara ya mwisho kushinda kwenye UCL ilikuwa ushindi wa  2-0 GNK Dinamo Zagreb October 2011.
• Frank de Boer alikuwa akicheza – na kaka yake Ronald alifunga – mara ya mwisho Ajax waliposhinda mechi ya UCL katika ardhi ya Spain baada ya kuifunga  3-2  Club Atlético de Madrid kaytika msimu wa 1996/97 UEFA Champions League hatua ya robo fainali.
• Ajax wamepoteza mechi zao 6 kati ya saba za mwisho walizocheza nchini Spain, wakitoa sare moja. Ushindi wao wa nyumbani dhidi ya FC Barcelona msimu uliopita ulikuwa ndio wa kwanza dhidi ya klabu ya Hispania tangu mwaka  2003/04.


Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa, alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.

Mahabiki wa timu ya Simba
Mashabiki wa timu ya Yanga
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.
Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.(P.T)
Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.



Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo
"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.
Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.


Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi wake.

Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.

Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari.


Kipindi cha Pili Man United walianza kwa kumtoa Ander Herrera na kumwingiza Marouane Fellaini ambae aliwapa manufaa makubwa kwa kusawazisha kwa Bao safi katika Dakika ya 48 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man United katika Ligi.
Lakini udhaifu wa Difensi ya Man United, wakati wakiwa wanatawala Gemu, uliwapa WBA mwanya mkubwa kupiga Bao la Pili Dakika ya 66 kupitia Saido Berahino.
Man United waliweza kusawazisha Dakika ya 87 baada ya Krosi ya Rafael kuokolewa na kumkuta Daley Blind aliepiga kiakili kufunga. Sare hii imewaweka Man United Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea ambao Jumapili ijayo watatua Old Trafford kuivaa Man United katika mtanange unaongojewa kwa hamu.Fellaini akishangilia na Van Persie jana walipoingia na kutupia bao la kusawazisha..



Na Faustine Ruta, Bukoba
Mh.Mbunge wa Jimbo la Bukoba VijijiniJason Rweikiza ameendelea na Ziara katika Jimbo lake lenye kata 39 kuunga mkono tamko la Rais Jakaya Mrisho Kikwete  la kujenga Maabara katika kila Kata kwa ajili ya Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi. Mh. Rweikiza anaendesha Mwenyewe Helkopta akisaidiana na Rubani mwenzake amesema kutokana na Muda kubana imebidi atumie usafiri wa Helkopta ili aweze kukimbizana na muda wa kufanya kazi za Wananchi wa Jimbo lake. Amewaomba Wananchi kuunga mkono jitihada za Rais Kikwete kuchangia ujenzi wa Maabara kwa ajili ya Wanafunzi. Mbali na kuchangi mambo mengine ya Maendelea kila Kata Mh. Rweikiza anachangia kiasi cha Milioni tatu katika Kata 39 kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara, Pia amewataka Wananchi kuunga mkono na kuipigia kura ya ndio Rasimu ya Katiba wakati wa kura za maoni ya Wananchi.
Katika Kata tano za Katoma, Karabagaine, Maruku, Kanyagereko na Kemondo amechangia kiasi cha Millioni 37,750,000/= kwa ajili ya Maabara na Miradi Mingine.

waliotembelea blog