Mahabiki wa timu ya Simba
Mashabiki wa timu ya Yanga
Mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na
Simba iliyochezwa juzi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 427,271,000.
Washabiki
49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa
sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5
ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.(P.T)
Kwa
upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000
kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo
sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh.
17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh.
100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.
0 maoni:
Post a Comment