Wednesday, May 6, 2015



PUNDE Azam FC uso kwa uso na Mabingwa Young Africans katika Uwanja wa Taifa mechi ambayo endapo Azam itashinda itajihakikishia nafasi ya pili. Young Africans baada ya mchezo huu watakabidhiwa kombe la Ubingwa #VPL2015.

MSIMAMO WAKE ULIVYO KWA SASA KABLA YA MTANANGE HUU



Mabingwa wa Italy, Juventus, wakiwa kwao Juventus Arena Jijini Turin Nchini Italy, wameanza vyema Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI walipowafunga Mabingwa Watetezi Real Madrid Bao 2-1.
Juventus walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 8 kutokana na pasi safi ya Marchisio kumkuta Carlos Tevez ambae Shuti lake lilitemwa na Kipa wa Real Casillas na kumkuta Alvaro Morata aliekwamisha Mpira wavuni.
Real walisawazisha Dakika ya 27 kwa Bao la Kichwa la Ronaldo kufuatia krosi ya James Rodriguez.
Hadi Haftaimu Magoli yalikuwa 1-1.

Kipindi cha Pili, Juve walifunga Goli la Pili baada ya kuokoa Kona ya Real na kuanza kaunta ataki kupitia Morata ambae alimpenyezea Tevez alieangushwa na Carvajal na Refa wa England Martin Atkinson kutoa Penati.
Tevez alifunga Penati hiyo na Juve kutangulia 2-1.
Álvaro Morata dakika ya 8 kipindi cha kwanza akipongezwa baada ya kuifungia bao la mapema Juve.Ronaldo akiwaomba wenzake Real Madrid kuwa makini baada ya kusawazisha bao kipindi cha kwanzaRonaldo akipongezwa1-1Hadi Nyavuni!Álvaro Morata dakika ya 8 kipindi cha kwanza anaipachikia bao la kwanza Juventus na kufanya 1-0 dhidi ya Real Madrid. Pongezi        Dakika ya 27 Cristiano Ronaldo aliwasawazishia bao Real Madrid kwa kufanya 1-1 na mtanange kwenda mapumziko kwa sare.


Tevez akisonga na mpiraRonaldo akiendesha
Baada Juve kwenda 2-1 mbele wakabadilisha Mfumo na kuanza kutumia 5-3-2 walipomtoa Sturaro na kumwingiza Barzagli ili kuweka ngoime ya Masentahafu Watatu ili kutetea uongozi wao kwa kujihami zaidi na kuvizia mashambulizi ya kushtukiza.
Timu hizi zitarudiana tena Mei 13 huko Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu.
Meneja wa Real Carlo AncelottiMashabiki wa RealMashabiki wa Juve!


BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisaa baada ya kutoka jera ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutokaThailand mpambano uho wa raundi kumi utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam.
Akizungumzia matayarisho ya mpambano huo promota Kaike Siraju amesema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa ivi sasa ambapo mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii.
Pambano utasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwa
wamesema kuwa wao wako tayari kwa mpambano huo na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya mpambano ambao utavuta hisia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi nchini
Pia soku hiyo bondia Vicent Mbilinyi 'Sugu' atavaana na Keis Amal


Zimeibuka ripoti kuwa Manchester United wameshinda kukurukakara za kumsaini Straika kinda wa Serbia anaechezea Klabu ya Anderlecht huko Ubelgiji.
Straika huyo, Aleksandar Mitrovic mwenye Miaka 20, awali aliripotiwa kwenda Newcastle huku Arsenal na Swansea City zikimwania.
Lakini habari zilizoibuka toka Italy zimedai sasa Straika huyo ambae ana Goli 20 na Anderlecht Msimu huu yupo njiani kutua Old Trafford baada ya Man United kulipiga kumbo Dau la Pauni Milioni 15 la Newcastle.

Mitrovic alijiunga na Anderlecht Mwaka 2013.na kucheza Mechi 65 akiwa na Bao 33 na pia huichezea Timu ya Taifa ya Serbia ambayo alianza 2013 na kucheza Mechi 11 na kufunga Bao 1.
Wakati alipokuwa na Miaka 18, Jopo la Wataalam wa Soka wa UEFA lilimteua kuwa ni mmoja Wachezaji 10 walio chini ya Miaka 19 wenye Vipaji Bora na vya juu Barani Ulaya.

Kama ilivyo kawaida yao, Man United haijazungumza lolote kuhusu Uhamisho wa Aleksandar Mitrovic.



Bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao anatarajia kufanyiwa upasuaji wa bega la mkono wa kulia, ikiwa ni siku tatu zimepita baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya bondia Floyd Mayweather wa nchini Marekani. 
Kwa mujibu wa tovuti ya ESPN bondia huyo alipambana na Mayweather huku akiwa na maumivu makali ya bega.
Vipimo vya MRI alivyofanyia Pacquiao, mara baada ya pambano hilo vimeonyesha anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje ya ulingo kwa muda wa miezi tisa hadi kumi na mbili.
Hata hivyo ilidaiwa kwamba, Pacquiao alidhamiria kujiondoa katika pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lililofanyika May mbili, lakini ombi lake lilikataliwa na kamisheni ya michezo ya Nedava, na pia alinyimwa nafasi ya kuchoma sindano ya ganzi kabla ya kupanda ulingoni ili kupunguza maumivu.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Pacquiao, hakufanya mazoezi kwa siku kadhaa kutokana na maumivu ya bega ambayo aliyatonesha kutokana na maandalizi makali ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.


Mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote amesema kuwa bado anataka kuinunua kilabu ya Arsenal licha ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010 alipotaka kununua hisa za kilabu hiyo.
Bilionea huyo kutoka Nigeria ni tajiri mara nane ya alivyokuwa wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo na kwamba shabiki huyo wa Arsenal bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka kuinunua kilabu hiyo ya Landon Kazkazini.
''Bado nina matumaini kwamba siku moja nitainunua timu hiyo',' alisema Dangote mwenye umri wa miaka 58.''Naweza kuinunua bei ambayo wamiliki wake itakua vigumu kukataa'', huku akiongezea kuwa ''najua mpango wangu''.
Mmiliki wa klabu ya Arsenal Stan Kroenker mwenye asilimia 67 ya hisa zote

La kushangaza ni kwamba Dangote ametaja hadharani kwamba Arsene Wenger anafaa kubadilisha mbinu yake akisema kuwa timu hiyo inahitaji mwelekeo mpya.
Dangote ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 ni tajiri zaidi ya Stan Kroenke ambaye anamiliki hisa nyingi katika kilabu hiyo na Bilionea raia wa Uzbek Alisher Usmanov ambao wamekuwa wakipigania udhibiti wa kilabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.


KUHUSU ALIKO DANGOTE
Born:
Kano, Nigeria
Age: 58
Occupation: Chairman and CEO of Dangote Group, a diversified conglomerate with interests in cement, sugar, flour, salt, pasta, beverages and real estate.

Estimated fortune of £10.4billion


Ranked by Forbes magazine as the 67th richest person in the world 


Named Forbes Africa Person of the Year 2014

waliotembelea blog