Bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao anatarajia kufanyiwa upasuaji wa bega la mkono wa kulia, ikiwa ni siku tatu zimepita baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya bondia Floyd Mayweather wa nchini Marekani.
Kwa mujibu wa tovuti ya ESPN bondia huyo alipambana na Mayweather huku akiwa na maumivu makali ya bega.
Vipimo vya MRI alivyofanyia Pacquiao, mara baada ya pambano hilo vimeonyesha anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje ya ulingo kwa muda wa miezi tisa hadi kumi na mbili.
Hata hivyo ilidaiwa kwamba, Pacquiao alidhamiria kujiondoa katika pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lililofanyika May mbili, lakini ombi lake lilikataliwa na kamisheni ya michezo ya Nedava, na pia alinyimwa nafasi ya kuchoma sindano ya ganzi kabla ya kupanda ulingoni ili kupunguza maumivu.
Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Pacquiao, hakufanya mazoezi kwa siku kadhaa kutokana na maumivu ya bega ambayo aliyatonesha kutokana na maandalizi makali ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.
0 maoni:
Post a Comment