Zimeibuka
ripoti kuwa Manchester United wameshinda kukurukakara za kumsaini
Straika kinda wa Serbia anaechezea Klabu ya Anderlecht huko Ubelgiji.
Straika huyo, Aleksandar Mitrovic mwenye Miaka 20, awali aliripotiwa kwenda Newcastle huku Arsenal na Swansea City zikimwania.
Lakini habari zilizoibuka toka Italy zimedai sasa Straika huyo ambae ana Goli 20 na Anderlecht Msimu huu yupo njiani kutua Old Trafford baada ya Man United kulipiga kumbo Dau la Pauni Milioni 15 la Newcastle.
Mitrovic alijiunga na Anderlecht Mwaka 2013.na kucheza Mechi 65 akiwa na Bao 33 na pia huichezea Timu ya Taifa ya Serbia ambayo alianza 2013 na kucheza Mechi 11 na kufunga Bao 1.
Wakati alipokuwa na Miaka 18, Jopo la Wataalam wa Soka wa UEFA lilimteua kuwa ni mmoja Wachezaji 10 walio chini ya Miaka 19 wenye Vipaji Bora na vya juu Barani Ulaya.
Kama ilivyo kawaida yao, Man United haijazungumza lolote kuhusu Uhamisho wa Aleksandar Mitrovic.

0 maoni:
Post a Comment