Utamaduni wa wanafunzi kuwatunga majina
waalimu wao ulikuwepo toka zamani na mara nyingi mwalimu anaweza
kutungwa jina ambalo yeye halijui ila kutokana na tabia na muonekano
wake basi wanafunzi hupenda kumtunga jina linaloendana na tabia zake
kama ni mkali usishangae ukisikia akipewa jina la ajabu kama mnoko na
kadhalika.
Stori zilizotoka mtandaoni ni kuwa wachezaji wa klabu ya Manchester United wameamua kumtunga jina kocha wao raia wa Uholanzi Louis van Gaal, wachezaji wa Man United wamempa jina kocha wao la “Daisy” kutokana na tabia yake ya kuendesha gari taratibu akiwa anawasili katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Carrington na kukwepa vishimo vidogo vidogo.
Jina hilo la ‘Daisy’ linatoka katika movie iliyowahi kutamba miaka ya nyuma ya ‘Driving Miss Daisy’
wachezaji hao wamempa jina la utani kocha huyo ambaye pia wanamtaja
kama muoga na anaendesha gari taratibu sana na mwendo wa gari yake
ukifananishwa na mwendo wa Konokono. Hata hivyo Louis van Gaal ni kocha ambaye anafahamika kwa tabia yake ya ukali na misimamo.