|
Mashindano
ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa
rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika
viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.
Mashindano
hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga
Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya
Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha timu 17 za kata zote za manispaa hiyo na timu ya polisi Shinyanga.
Mashindano
ya Kombe la Meya Shinyanga yakihusisha mpira wa miguu yataendelea
kufanyika hadi tarehe 25,Julai 2015 na yatakuwa yanafanyika siku tatu
kwa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.
Mshindi
wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi
milioni moja na laki tano,kombe na medali ya dhahabu,wa pili shilingi
milioni moja,kombe dogo na medali ya fedha na wa tatu shilingi laki
tano,kombe dogo na medali ya shaba.
Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa uzinduzi huo,Kadama Malunde,ametuletea picha kutoka eneo la tukio....
|
|
Mstahiki
meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati
wa ufunguzi wa Pepsi Meya Cup Shinyanga 2015,ambapo alisema lengo la
mashindano hayo ya mpira miguu kwa vijana yatakayoshirikisha timu 18 za
manispaa ya Shinyanga ni kwa ajili ya burudani,ajira na kusaka vipaji
kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.
|
|
Meya
wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh alisema mashindano hayo yatakuwa
yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na yatafanyika mara tatu kwa wiki
katika viwanja vitatu vya Shycom,Kambarage na Polisi mjini Shinyanga.
|
|
Mashindano hayo yameanza leo Juni 26,2015 yatafikia tamati Julai 25,2015
|
|
Meza kuu wakiwa eneo la tukio.
|
|
Meneja
mauzo wa Kampuni ya vinywaji baridi Pepsi kanda ya Ziwa Seni Makwaya
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015 ambapo
alisema katika mkoa wa Shinyanga ndiyo mara ya kwanza kwa kampuni ya
Pepsi kudhamini mshindano ya meya,ingawa huu ni mwaka wa tatu nchini
Tanzania tangu waanze kudhamini mashindano ya namna hiyo.
|
|
Meneja mauzo wa kampuni ya vinywaji baridi SBC Tanzania Limited (Pepsi) bwana Promod Nair
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kombe la meya Shinyanga
2015 ambapo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuinua
vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.
|
|
Meneja
mauzo kampuni ya Pepsi mkoa wa Shinyanga bwana Benson Tweve akizungumza
katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alizitaka timu za
Stand United na Mwadui FC kutumia fursa ya mashindano hayo ya Meya Cup
kuchukua vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuinua mkoa wa Shinyanga
kimichezo.
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015,ambapo
pamoja na mambo mengine aliwataka vijana wa Shinyanga kutumia fursa ya
mashindano hayo kuonesha vipaji vyao kwani michezo ni ajira.
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro
akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Masekelo
yenye Timu ya Masekelo fc iliyocheza mechi ya ufunguzi na Ngokolo fc
kutoka kata ya Ngokolo.
|
|
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi zawadi kwa mshindi
wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli Kulwa Ntyuki uliofanyika
mjini Shinyanga wakati wa ufunguzi wa kombe la meya Shinyanga.
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro
akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo.
|
|
Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakikagua wachezaji wa timu ya Masekelo FC na Ngokol0 FC.
|
|
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Masekelo FC kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo FC na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga .
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua
timu ya Ngokolo fc kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo fc na
Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga.
|
|
Waamuzi wa mchezo wakiwa uwanjani.
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akizungumza
na wachezaji wa timu ya Ngokolo fc na Masekelo fc na Ngokolo FC
|
|
Mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro
akijiandaa kupiga penati huku meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh
Mukadam akiwa golini.
|
|
Meya
wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akihangaika golini baada
ya kufungwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
|
|
Mechi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc ukiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo,Masekelo fc bao 2,na Ngokolo fc bao 2.
|
|
Wakazi wa Shinyanga wakishuhudia mechi.
|
|
Wengine walipaki na baiskeli zao uwanjani kujionea kilichokuwa kinajiri uwanjani.
|
|
Tunafuatilia kinachoendelea....
|
|
Wachezaji wa Masekelo fc wakishangilia goli lao la kwanza.
|
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa juu ya ukuta wakifuatilia mechi.
|
|
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam(mwandaaji wa Kombe la Meya Shinyanga 2015) akiteta jambo na Meneja mauzo SBC Tanzania Limited Pepsi bwana Promod Nair( wadhamini wa kombe la meya Shinyanga 2015).
|
|
Meya
wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiteta jambo na
msimamizi wa kituo cha Shycom bwana Geofrey Tibakenda,na mratibu wa
Kombe la Meya bwana Paul Mganga,ambaye ni mkurugenzi wa Myklay
Entertainment(katikati).
Picha zote na Kadama Malunde.
|
|