Sunday, November 2, 2014



Van Gaal aapa kuichapa Mancity
Meneja wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal anaamini kwamba timu yake itatumia fursa ya kushuka kwa soka ya kilabu ya Manchester City katika uwanja wa Etihad kuishinda kilabu hiyo.
Kilabu ya Manchester City imepoteza mechi zake mbili za mwisho baada ya kushindwa na West Ham na Newcastle.
''Kile tulichokiona katika mechi mbili za mwisho si matokeo ya kuridhisha,alisema Van Gaal.
''Tuna hisia njema kuhusu mechi hii''.''Tunahitaji matokeo mazuri na huenda yakawa dhidi ya Manchester City''.Aliongezea Van Gaal.
Timu za mancity na man United katika derby
City iko katika nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa alama sita dhidi ya Chelsea.
Tangu ipoteze kwa mabao 5-3 dhidi ya Leicester mnamo Septemba 21,Manchester United haijapoteza na huenda ikaikaribia Mancity katika nafasi ya nne iwapo itashinda mchuano huu wa 'Derby'.
Hatahivyo ushindi dhidi ya Manchester United utakuwa wa nne kati ya timu hizo mbili hatua ambayo haijaafikiwa kwa takriban miaka 44 na timu hiyo.


Wachezaji wa Man City wakishangilia na kupongezana kwa bao lililofungwa na Aguero dakika 63Smalling ameoneshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza mwishoni dakika 39Ni Shida kwenye lango la Man United.Kipa wa United De Gea bado ni shida...kwenye hii Debi!!Wayne Rooney arudi kwenye Debi ya Manchester United LEO Jumapili, Novemba 2, Uwanjani Etihad, Dabi ya Jiji la Manchester, Mechi inayongojewa na Mamilioni Duniani, itachezwa katika Mechi ya Ligi Kuu England wakati Wenyeji Manchester City watakapocheza na Mahasimu wao Manchester United.
Safari hii Man City wanatinga Uwanjani wakiwa ndio Mabingwa Watetezi na wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya Pili Southampton na Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.
Man United wao wako Nafasi ya 8 na wakiwa Pointi 4 nyuma ya Man City.

waliotembelea blog