Sunday, February 9, 2014


 Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) , Sharon Mariwa  Meneja wa Mahusiano OXFAM, Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB pamoja na Mkamiti Mgawe Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM, wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa katika Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula leo.
Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akielezea Mchakato mzima wa kazi ilivyokuwa kabla , wakati wa kuwatafuta washiriki wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula na kutaja rasmi majina ya waliochaguliwa katika usahili huo.

   Meneja wa Mahusiano OXFAM Sharon Mariwa  akielezea utaratibu utakao fuatia baada ya kutangazwa rasmi majina ya waliochaguliwa katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
 Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB akitilia mkazo baadhi ya mambo wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa kuingia Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
 Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akijibu Maswali yaliyo ulizwa na waandishi wa Habari.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na wadau Mbalimbali wakiwa wanasikiliza kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.




*************
Majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa Mama Shujaa wa Chakula / Maisha Plus 2014.
Usaili:
Mama Shujaa watapigiwa kura mtandaoni ili kupata washiriki 20 ambao wataingia kijijini Maisha Plus. Zoezi la kuwapigia kura litafanyika baada ya uhakiki ‘verification’ pamoja na upigaji picha kuthibitisha taarifa walizojaza kwenye fomu.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. INALIPA.
Vijana wa Maisha Plus watagawanywa katika makundi mawili ya watu 20 na kupelekwa katika vijiji vilivyochaguliwa Iringa na Zanzibar, huko wataishi pamoja na familia zilizochaguliwa na kutakiwa kuishi maisha sawa na familia hizo. Zoezi kuu litakuwa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa vijiji hivyo kama changamoto za maji, n.k.
Baada ya siku 7 wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura vijana hao ili kupata jumla ya vijana 18 watakaopelekwa katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na wenzao 12 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni Maisha Plus REKEBISHA.

Majina

Mama Shujaa wa Chakula
  1. Amina Kupela Chikaponya – Mtwara
  2. Anna James Yuda – Morogoro
  3. Anna Mwanilyela Chrisant – Katavi
  4. Bahati Muriga –Mwanza
  5. Clara Ancilla Ibihya – Pwani
  6. Cristina Kurwa Malale – Zanzibar
  7. Dina Rusoti – Mara
  8. Dionisia Rashidi Karata – Tanga
  9. Doricus Msafiri Shumbi – Singida
  10. Edina Jamas – Mbeya
  11. Elinuru Moses Pallangyo – Arusha
  12. Elizabeth Matayo – Geita
  13. Elizabeth Simon – Morogoro
  14. Ezeleda Chedego – Dodoma
  15. Fredina M. Said – Shinyanga
  16. Gladness Ebenezery Mmary – Kilimanjaro
  17. Grace G.D. Mahumbuka – Kagera
  18. Janeth Niima – Manyara
  19. Kuruthumu Ramadhani Mwengele – Tanga
  20. Leah Dominick Mnyambugwe – Dodoma
  21. Mary Athanaz Ndasi – Rukwa
  22. Mary John Mwanga – Singida
  23. Mary Kessy – Dar es salaam
  24. Neema Robert – Simiyu
  25. Nyachum Haji Ame – Zanzibar
  26. Pendo Musa – Morogoro
  27. Santina Mapile – Njombe
  28. Thereza Kitinga – Mwanza
  29. Zaituni Shedrack Kalenbi – Kigoma
  30. Zamda Daniely Mgonganga – Iringa

Vijana wa Maisha Plus

  1. Adolph Anacleth - Mwanza
  2. Agatha Kalesu – Rukwa
  3. Ally Thabit - Mwanza
  4. Anastazia John – Mara
  5. Asumta Mwingira – Dar es salaam
  6. Ausi Abdul Moyo – Ruvuma
  7. Bakari Khalid – Shinyanga
  8. Boniphace Meng’anyi Nyankena – Dar es salaam
  9. Charles Daniel – Simiyu
  10. Douglas Said Msalu - Arusha
  11. Ellymathew Kika – Njombe
  12. Elizabeth Joachim - Tabora
  13. Fahamni Kaite Mwadini – Zanzibar
  14. Farida Ally – Pwani
  15. Fadhili Isanga - Kilimanjaro
  16. Flora John - Singida
  17. Frederick Joseph Ndahani – Singida
  18. Hyasinta T. Hokororo - Mtwara
  19. Jane Julio Kalinga – Iringa
  20. John Sylvester Malima - Geita
  21. Joyce Jacob Mushy - Arusha
  22. Marriam Mosses - Shinyanga
  23. Mary Nicholaus Kavishe – Manyara
  24. Mbonimpaye N. Nkoronko – Rukwa
  25. Mohammed Selemani Lipemba - Lindi
  26. Moureene K. Daud - Kagera
  27. Nelson Daniel – Dar es salaam
  28. Ngoma Abdallah – Kigoma
  29. Osama Norman – Mbeya
  30. Otilia Selestin Simime - Mbeya
  31. Said Salum – Katavi
  32. Salumu Saidi Johari – Mtwara
  33. Scholastica Deusidedith – Geita
  34. Seif Mohamed Salum - Tabora
  35. Shaaban Masoud Shaaban – Zanzibar
  36. Shida Keneth Mganga – Dodoma
  37. Shishira G. Mnzava - Morogoro
  38. Thomas P. Mgazwa – Dodoma
  39. Yassini Hamisi Suddi – Dar es salaam
  40. Zaharani Yusuph Hossen – Tanga

Bosco Ntaganda
Kesi dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, inatarajiwa kuanza hii leo katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
Mahakama hiyo inatarajiwa kuamua ikiwa Bosco Ntaganda atafunguliwa mashtaka ya mauaji, ubakaji, utumwa wa ngono na kuwasajili watoto jeshi.
Mshukiwa huyo ambaye pia anafahamika kama ''The Terminator'' ni mwanzilishi kwa kundi la waasi la M23, ambalo lilishindwa na utawala wa Kinshasa mwaka uliopita, baada ya miezi kumi na nane na mapigano makali, katika eneo la Kivu ya Kaskazini, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Lakini atakapofika mbele ya mahakama hiyo, Ntaganda atafunguliwa mashtaka kumi na tatu ya uhalifu wa kivita na mengine matano ya ukatili wa kibinadam, uhalifu uliotekeelzwa zaidi ya miaka kumi iliyopita wakati alipokuwa mbabe wa kivita katika eneo la Ituri, Kaskazini mwa Congo.
Zaidi ya watu 800 waliuawa
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Fatouh Bensouda, amesema kuwa takriban watu mia nane waliuawa na wapiganaji wa Patriotic Foces for Liberation of Congo, FPLC, walioongozwa na Bwana Ntaganda.

Wengi wa wapiganaji wake walitoka kabila la Hema ambao walikuwa wakipambana na wapiganaji wa wa Lendu, kuthibiti maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa na Bensouda katika mahakama hiyo, Ntaganda aliongoza na kuidhinbisha mashambulio kadhaa dhidi ya watu wa kabila la Lendu.
''Wanjaeshi wa Ntaganda walishambulia vijiji kadhaa kwa kutumia silaha nzito nzito na kuwafukuza watu, huku wakifanya msaka wa nyumba hadi nyumbana pia katika misitu iliyokuwa katika eneo hilo'' Alisema Bensouda.
Kiongozi huyo wa zamani wa waasi anatuhumiwa kuharibu mali ya raia kwa kuteketeza makaazi yao baada ya kupora mali.
Atuhumiwa kusajili watoto jeshini
Ripoti zinasema Ntaganda alizuru kambi kadhaa ambako watoto walio na chini ya umri wa miaka kumi na mitano walipewa mafunzo ya kijeshi na kuwa alifanya mashambulio pamoja nao.
Katika kikao chake cha kwanza katika mahakama hiyo mwezi Machi mwaka uliopita, Ntaganda aliwaambia majaji hao wa ICC kuwa '' Nimefahamishwa kuhusu mashtaka ya uhalifu yanayonikabili na kuwa anakiri kuwa hana hatia''
Majaji wa mahakama hiyo ya ICC wana muda wa wiki mbili kuamua ikiwa kesi dhidi ya Bwana Ntaganda itaendelea au la.
Mshukiwa mwingine ambaye alifunguliwa mashtaka kwa pamoja na Ntaganda alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na minne gerezani.
Ntaganda ni mshukiwa wa kwanza ambaye alijisalimisha kwa mahakama ya ICC, baada ya kujisalimisha kwa ubalozi wa Marekani mjini Kigali miezi kumi na moja iliyopita na kuomba awasilishwe kwa mahakama ya ICC.
Ntaganda alijisalimisha kwa nia gani?
Wachanganuzi wanasema kuwa Ntaganda alihofia maisha yake kama mtoro kutoka kwa viongozi wengine hasimu wa M23 lakini hadi sasa dhamira ya kujisalimisha kwake haijajulikana.
Mahakama ya ICC ilitoa vibali vya kukamatwa kwa Ntaganda mwaka wa 2006 na nyingine iliyokuwa na mashtaka zaidi mwaka wa 2012.
Ntaganda ambaye alizaliwa mwaka wa 1973, ni Muafrika wa tano ambaye anazuiliwa na mahakama hiyo ya Kimataifa ya Jinai.
Kiongozi huyo wa waasi alikwea kukamatwa wakati vibali hivyo vilitolewa kwa kuwa alikuwa afisa mwandamizi jeshini.
Mwaka wa 2006, aliteuliwa kiongozi wa CNDP, kundi lingine la waasi la watu wa kabila la Watutsi lililoongozwa na Laurent Nkunda.
Mapigano nchini Congo yalimalizika kufuatia mkataba wa amani ulioidhinisha waasi hao kuteuliwa kujiunga na jeshi la serikali.
Ntaganda naye akateuliwa kuwa generali katika jeshi la serikali na mara tu akaanza kuunda kikosi chake ndani ya serikali.

Kwa mara nyingine tena alifufua mitandao yake na mwaka wa 2012 aliunda kundi la M23, wakati rais Joseph Kabila alipoonyesha ishara kuwa yuko tayari kutekeleza agizo la mahakama ya ICC ya kumkamata na kumuwasisha mbele ya mahakama hiyo.
Umoja wa Mataifa umeishutumu Rwanda kwa kumfadhili Ntaganda na kundi lake la M23, madai ambayo yamepingwa vikali na utawala wa rais Paul Kagame.
bent_1_f64bd.jpg
Darren Bent alifunga bao dakika za mwisho mwisho na kumhakikishia kocha wao Rene Meulensteen matokeo muhimu wakati wa mechi kati ya Fulham na Manchester United iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Fulham licha ya kushikilia nafasi ya mwisho kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ilitoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na mabingwa watetezi Manchester United.
benti_2_c3a0d.jpg
Fulham ndio iliyokuwa ya kwanza kuona lango la Manchester United, katika kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha wake Steve Sidwell.
bent_3_a5fc2.jpg

Hata hivyo wenyeji walijikakamua kipindi cha pili ambapo walimiliki mpira kwa asilimia kubwa kabla ya Robin Van Persie kusukuma kombora kali lililomuacha kipa wa Fulham kinywa wazi.
Dakika mbili baadaye Michael Carrick vile vile alivurumisha kombora lingine ambalo liliwaacha wachezaji wa Fulham wakishangaa.
Kutangulia sio kufika
Kadri muda ulivyoendelea kusonga mashabiki wa Manchester United, walikuwa wameanza kusherehekea huku baadhi yao wakimsifu kocha wao David Moyes.
Kama wahenga walivyonena, usikate kanzu kabla ya mtoto kuzaliwa, uwanja wa Old Trafford ulitulia kama kaburi, pale mchezaji wa ziada wa Fulham Daren Bent, alipofunga bao kwa kichwa baada ya kipa wa Man United David De Gea kutema mkwaju wa Kieran Richardson.
Huzuni ilitanda katika uwanja wa Old Trafford baada ya vijana hao wa Moyes kupoteza alama mbili muhimu na hivyo kudidimiza matumaini ya United ya kuhifadhi kombe hilo au hata kumaliza katika nafasi ya kwanza nne.
United ilifanya mashambulio mengi na wakati wa mechi hiyo iliandikisha krosi 81, kiwango ambacho ndicho kubwa zaidi kuwahi kuandikishwa na klabu yoyote tangu mwaka wa 2006.
United ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya saba kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier imepangiwa kutoana jasho na Arsenal siku ya Jumatano na kocha David Moyes atakuwa na kibarua kigumu kutuliza nyoyo za mashabiki wao.
Chanzo, bbcswahili.com



Emmanuel Adebayor amefunga bao la sita katika mechi tisa dhidi ya Everton leo
BAO pekee la Emmanuel Adebayor dakika ya 65 limeipa ushindi muhimu wa 1-0 Tottenham dhidi ya Everton katika vita ya kuwania kumaliza ndani ya ne bora Ligi Kuu England.
Spurs sasa inatimiza pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 na inakaa katika nafasi ya tano, nyuma ya Liverpool yenye pointi 50,ambayo jana imeifunga Arsenal 5-1.




Kipindi cha Pili, Man United walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza kina Valencia, Januzaj na Chicharito na hii ilileta uhai na waliweza kufunga Bao 2 katika Sekunde 90.


 
Michael Carrick akijiuliza kwa kile kilichotokea...
 
 
 

t Bao la Fulham limefungwa na Steve Sidwell katika dakika ya 19. Bao hilo limedumu mpaka dakika mwisho kwenye kipindi cha kwanza na timu ya Fulham ndio imekwenda mapumziko kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Man United kwenye uwanja wa Old Trafford.Kipindi cha pili dakika ya 78 Van Persie akasawazisha bao na kufanya 1-1,
 
 
 
Bao likifungwa na Michael Carrick katika dakika ya Dakika ya 80.

 
 
 
Last gasp: Manchester United were less than a minute from victory when Darren Bent headed home to snatch a point for Fulham
 
Flying: Bent celebrates his dramatic equaliser at Old Trafford Bent akishangilia bao lake la kusawazisha
 
 
kipa ana rahaaaaaaaaaaaaa


POS.LOGO &TEAMPWDLGDPTS
1ChelseaChelsea2517532756
2ArsenalArsenal2517442255
3Manchester CityManchester City2517354154
4LiverpoolLiverpool2515553350
5Tottenham HotspurTottenham Hotspur251456047
6EvertonEverton2512941145
7Manchester UnitedManchester United2512581041
8Newcastle UnitedNewcastle United2511410-237
9SouthamptonSouthampton25997736
10Swansea CitySwansea City257612-327
11Hull CityHull City257612-527
12Aston VillaAston Villa257612-927
13Stoke CityStoke City256811-1426
14Crystal PalaceCrystal Palace258215-1626
15West Ham UnitedWest Ham United256712-725
16Norwich CityNorwich City256712-1825
17SunderlandSunderland256613-1324
18West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion2541110-823
19Cardiff CityCardiff City255614-2521
20FulhamFulham256217-3120


ratiba zinazokuja
Jumanne Februari 11
22:45 Cardiff v Aston Villa
22:45 Hull v Southampton
22:45 West Ham v Norwich
23:00 West Brom v Chelsea


Jumatano Februari 12
22:45 Arsenal v Man United
22:45 Everton v Crystal Palace
22:45 Man City v Sunderland
22:45 Newcastle v Tottenham
22:45 Stoke v Swansea
23:00 Fulham v Liverpool

waliotembelea blog