Monday, February 23, 2015


WWW.BUKOBASPORTS.COMBAADA ya Wiki iliyopita kuchezwa Mechi 4 za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Wiki hii nayo zipo Mechi 4 za mwisho kumalizia Mechi za Kwanza za Raundi hiyo.
KESHO Jumanne Usiku zipo Mechi mbili moja ikiwa huko Etihad Jijini Manchester wakati Manchester City watakapoivaa FC Barcelona na nyingine huko Mjini Turin Nchini Italy wakati Mabingwa wa Italy na Timu inayoongoza Serie A, Juventus watakapocheza na BVB Borussia Dortmund.

Jumatano zitakamilika Mechi za mwisho za Kwanza kwa Arsenal kuikaribisha Emirates Klabu ya France AS Monaco na Bayer 04 Leverkusen ya Germany kuwa Wenyeji wa Mabingwa wa Spain Atletico de Madrid. Mechi ya Jumanne huko Etihad ni Marudio ya Mechi ya Msimu uliopita ya Raundi hii hii ya Mashindano haya wakati Man City ilipotolewa na Barcelona kwa Jumla ya Mabao 4-1 katika Mechi mbili ambazo kila Mechi City ilimaliza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao mmoja kupewa Kadi Nyekundu.
Katika Mechi hizo, Barcelona walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Etihad Bao 2-0 kwa Bao za Lionel Messi, la Penati, na jingine la Daniel Alves huku Martín Demichelis wa City akipewa Kadi Nyekundu. 

Kwenye Marudiano huko Nou Camp, Barca ilishinda Bao 2-1 Wafungaji wao wakiwa wale wale, Lionell Messi na Alves, huku Pablo Zabaleta wa City akipewa Kadi Nyekundu.
Lakini safari hii, Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini, anaamini City ipo kwenye hali njema zaidi kupita Msimu uliopita.
Wakati Jumamosi City ikiitwanga Newcastle United Bao 5-0 kwenye Ligi Kuu England, Barcelona ilichapwa 1-0 na Malaga kwenye Mechi ya La Liga iliyochezwa Nyumbani kwa Barca huko Nou Camp.



UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA - JUMATANO
Jumanne 24 Februari 2015
Juventus FC vs BV Borussia Dortmund
Manchester City vs FC Barcelona .


Jumatano 25 Februari 2015
Arsenal FC vs AS Monaco FC Bayer 04
 Leverkusen vs Atletico de Madrid.

waliotembelea blog