Mkurugenzi
wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao
Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa Airtel
Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi
katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika
Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya
makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam
jana. Anayeshuhudia (katikati), ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
Meneja
Masoko wa Airtel, Anet Muga. akiongea wakati wa tukio la kumuaga na
kumkabithi bendera ya taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika
fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi
Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya
makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam
jana. pichani katikati ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua akifatiwa na mshindi wa
Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi.
mshindi
wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika bendera mara
baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika
mashindano ya muziki ya Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika
Jumamosi hii nchini Kenya.
Barasa
la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindano la
Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi
kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha
washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku ya
Jumamosi tarehe 28 March 2015.
Mayunga
aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa vipaji vya
mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music lililozinduliwa na kampuni
ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi na kushirikiksha washiriki
mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo fainali ya kumsaka
mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa februari na kumwezesha Mayunga
kuwashinda washindani wengine watano na katika fainali hizo na kuondoka
na kitita zawadi ya shilingi million 50.
Akiongea
wakati wa kukabithi bendera hiyo, Mkurugenzi wa ukuzaji sanaa na Masoko
wa BASATA bi Nsao Shalua alisema” kwanza tunachukua fulsa kuwapongeza
Airtel kwa kuanzisha shindano hili na kwa kufata taratibu zote za
kuratibu mashindano. Airtel leo wameonyesha mfano kwa kumleta mshindi
hapa ofisini, kuaga rasmi na kupatiwa kibali cha kusafiri kutoka baraza
la sanaa Tanzania kitu ambacho hakifanywi na makampuni mengi na hata
wasaani wengi nchini. Huu ni mfano wa kuigwa na natoa wito kwa watu wote
wanaoondoka nchini kwaajili ya kwenda kufanya shughuli za sanaa
kuhakikisha wanafata utaratibu kwa kutufahamisha na kupata hati maalumu
ya kushiriki shughuli na kuiwakilisha nchi yetu nje ya nchi.
Aidha
napenda kumpongeza Mayunga kwa kuibuka kuwa mshindi na kupata nafasi ya
kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika, tunapenda kumwomba
atumie fulsa hii vizuri na kwa kufanya hivyo basi tunaamini atafanya
vyema. Tunamtakia safari njema na mashindano mema, tunaamini Mayunga
atatuwakilisha vyema na kutangaza nchini yetu katika angaza za muziki
kwa ujumla.
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga alisema” Leo
tunamuwezesha Mayunga kwenda kushiriki na kuiwakiisha nchi yetu katika
mashindano ya Afrika Tunamwezesha kujiwekea umaarufu na kuonyesha kipaji
chake kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na Mayunga
tunawawezesha vijana wengi barani Afrika kwa ujumla kuzifikia ndoto zao.
Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi , jijini Naivasha Kenya
ambapo washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika watachuana vikali. Mshindi
wa Airtel Trace Afrika atapata nafasi ya kwenda nchini marekani na
kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya R&B , Akon na
kuweza kurekodi nyimbo zake.
Natoa
wito kwa watanzania kumpigia kura Mayunga kwa ku tuma SMS, yaani ujumbe
mfupi andika neno YUN kwenda 15594, Alhamisi ni siku ya mwisho ya kupiga
kura, asiliimia 25 ya ushindi inatoka kwenye kura yako hivyo kura yako
ni ya muhimu sana. Aliongeza Aneth.
Akiongea
mara baada ya kukabithiwa bendera Malimi Mayunga alisema” namshukuru
sana mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii, nawaahidi
watanzania kuwawakilisha vyema, pamoja na hayo nawaomba sana watanzania
waniunge mkono kwa kunipigia kura ili nipate nafasi ya kuweza kuibuka
kuwa mshindi.
Hii
kwangu ni nafasi ya pekee sana na namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha
na Airtel kwa kuwawezesha vijana kama mimi kuonyesha vipaji vyao na
kuzifikia ndoto zao kupitia mashindano mengi kama haya Mashindano ya
Airtel Trace Music Star yalianzishwa kwa lengo la kuonyesha vipaji vya
vijana kimuziki na nakuwapatia fulsa ya kukua kimuziki.