Friday, May 15, 2015

KEPTENI wa Liverpool Steven Gerrard Jumamosi ataichezea Klabu yake kwa mara ya mwisho Uwanjani kwao Anfield na Tiketi za Mechi hiyo zimefika Bei ya Shilingi Milioni 4, 090, 680/=.
Jumamosi Liverpool watacheza Mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England Msimu huu Uwanjani kwao Anfield dhidi ya Crystal Palace.


Hii Leo mtandao unaouza Tiketi kwa ajili ya Mechi hiyo, www.ticketbis.net umeanika Bei za Tiketi za kuanzia Pauni 100 hadi 1,324.64 ikiwa ni takriban Shilingi 314,727 hadi Shilingi 4,166, 985.

Kwa Mechi ya kawaida kwenye Jukwaa Kuu la Anfield Tiketi huuzwa Pauni 47 yaani Shilingi 147,922.
Gerrard, mwenye Miaka 34, anastaafu kuicheza Liverpool Msimu huu baada ya kuwa nao kwa Miaka 17 na Mechi yake ya mwisho kabisa itakuwa Wiki ijayo Ugenini wakicheza na Stoke City.
Hata hivyo, Gerrard ataendelea kusakata Soka huko Marekani akichezea Ligi ya MLS na Klabu ya LA Galaxy.
Zipo habari zinasema Gerrard atawekewa Gwaride la Heshima na WAchezaji kabla ya Mechi ya Jumamosi kuanza kati ya Liverpool na Crystal Palace.

 Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
 Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
 Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .

waliotembelea blog