KEPTENI
wa Liverpool Steven Gerrard Jumamosi ataichezea Klabu yake kwa mara ya
mwisho Uwanjani kwao Anfield na Tiketi za Mechi hiyo zimefika Bei ya
Shilingi Milioni 4, 090, 680/=.
Jumamosi Liverpool watacheza Mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England Msimu huu Uwanjani kwao Anfield dhidi ya Crystal Palace.
Hii Leo mtandao unaouza Tiketi kwa ajili ya Mechi hiyo, www.ticketbis.net umeanika Bei za Tiketi za kuanzia Pauni 100 hadi 1,324.64 ikiwa ni takriban Shilingi 314,727 hadi Shilingi 4,166, 985.
Kwa Mechi ya kawaida kwenye Jukwaa Kuu la Anfield Tiketi huuzwa Pauni 47 yaani Shilingi 147,922.
Gerrard, mwenye Miaka 34, anastaafu kuicheza Liverpool Msimu huu baada ya kuwa nao kwa Miaka 17 na Mechi yake ya mwisho kabisa itakuwa Wiki ijayo Ugenini wakicheza na Stoke City.
Hata hivyo, Gerrard ataendelea kusakata Soka huko Marekani akichezea Ligi ya MLS na Klabu ya LA Galaxy.
Zipo habari zinasema Gerrard atawekewa Gwaride la Heshima na WAchezaji kabla ya Mechi ya Jumamosi kuanza kati ya Liverpool na Crystal Palace.

0 maoni:
Post a Comment