Sunday, November 29, 2015


Bale akipongezwa kwa bao lake la kwanza kwa Real Bale na Cristiano RonaldowakipongezanaRonaldo akishangilia PatashikaVuta nikuvute!


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam. Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.


Tottenham wameikosa nafasi ya kupanda kwenye Ligi Kuu England na kukamata Nafasi ya 4 baada ya kutoka 0-0 na Chelsea kwenye Mechi ya Dabi ya London iliyochezwa White Hart Lane.
Sare hii imewabakisha Tottenham Nafasi ya 5 na kuwaweka Chelsea Nafasi ya 14.
Katika Kipindi cha Kwanza, Kipa wa Chelsea, Asmir Begovic, ndie alisumbuka sana kwa kuokoa michomo kadhaa ikiwepo ile ya out Son Heung-min, kwa Kichwa, na Shuti la chini la Mousa Dembele.
Leo Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimpia Benchi Diego Costa na kumuanzisha Eden Hazard kama Fowadi kitu ambacho kilimkera Costa alieonekana kuvua gwanda lake la juu na kulitupa alipo Mourinho alipoona haingizwi.


Schweinsteiger aliisawazishia bao Man United katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko sare ya 1-1.
Kipindi cha kwanza dakika ya 24 Vardy anaipa bao la kuongoza Timu yake Leicester City na kuongoza bao 1-0 dhidi ya Man United.VIKOSI:
Leicester City wanaoanza XI:
Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy
Akiba: De Laet, King, Schlupp, Ulloa, Dyer, Schwarzer, Inler
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, McNair, Carrick, Schweinsteiger, Young, Mata, Martial, Rooney
Man Utd akiba: Depay, Romero, Fellaini, Schneiderlin, Rashford, Jackson, Andreas Pereira

Manchester United wametoka Sare 1-1 huko King Power Stadium walipotoka 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Man City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England.
Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje Rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu England.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger na walistahili kushinda kwenye Kipindi cha Pili kwa jinsi walivyotawala lakini tatizo lao sugu la kutokuwa na Wachezaji wenye kasi na Wafungaji liliwakisha.

waliotembelea blog