Sunday, October 18, 2015



Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo

NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na kutwaa kombe.
Akitoa nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.

Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia a ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.

“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.

Katika pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani safi wapenzi wa soka.

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili kushoto).

Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo

Chikawe, akisalimiana na Alex Lugendo

"Ball Boys" wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani



Dkt. Magufuli (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (pichani kulia) Ndugu Stanslaus Mabula mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza waliohojiwa na Globu ya Jamii walieleza na kukiri wazi kuwa haijawahi kutokea kwa mapokezi haya makubwa na ya aina yake,na kuwa Magufuli ndiye anaetosha kuvaa viatu vya Urais.

Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula

Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula na Stanslaus Mabula ambaye anagombea ubunge Jimbo la Nyamagana.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika mithili ya Utitiri kwenye uwanja wa Furahisha jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifikakapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.



Sehemu ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake.

sehemu ya umati wa watu ndani ya viwanja vya furaisha jijini Mwanza jioni ya leo.

Wananchi wakiuzuia msafara wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli uliokuwa ukisindikizwa na umati wa watu kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwenda kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.



Pascal wawa akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande).

Kocha wa Yanga, Hans Pruijm akitoa maelekezo kwa Salum Telela.

Mshambuliaji wa Yanga, malimi Busungu akiwatoka wachezaji wa Azam FC.

Beki wa Azan FC, Pascal Wawa akimiliki mpira huku akizongwa na Salum Telela.

Beki wa Azam FC, Agrey Morris akipiga tiktak kuokoa moja ya hatari langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Sioka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Mshambuliaji wa Azam FC, Himid Mao (kushoto) akichuana na kiungo wa Yanga, Mbuyu Twite wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Azam FC.

Mashabiki wa Yanga.



BAO za Arsenal zimefungwa na Sanchez, Giroud na Ramsey na zote zikifungwa kipindi cha pili
Alexis Sánchez dakika ya 62'

waliotembelea blog